Habari kuhusu Vyombo na Uandishi wa Habari kutoka Aprili, 2012
Mali: Kimya cha Wanablogu wa Nchini Humo
Wakati mtandao wa intaneti umetawaliwa na blogu, ujumbe wa twita na video kutoka nchi mbalimbali, watumiaji wa intaneti wenyeji wa Mali wangali kimya. Mji mkuu, Bamako, umeathirika kwa kukatika kwa umeme kwa kile kinachodaiwa kuwa kuadimika kwa mafuta. Katika mazingira kama haya, kipaumbele si kutuma ujumbe, bali kutafuta kutafuta taarifa kuhusu viongozi wapya wa sehemu ya Kaskazini ya Nchi hiyo.
Ukraine: Gereza la Lukyanivska – “Mahali Watu Wanapotendewa kama Wanyama”
Mnamo tarehe 2 Aprili, Televisheni ya Ukraine ya TVi ilirusha filamu iliyotayarishwa na Kostiantyn Usov kuhusu hali ya maisha na jinsi mahabusu wanavyotendewa katika gereza la Kyiv la Lukyanivska, na pia kuhusu kuenea sana kwa rushwa miongoni mwa askari magereza. Kwa uchache, wengi katika wale ambao tayari wametazama video ya Usov walishtushwa sana na yale waliyoyaona.