Habari kuhusu Vyombo na Uandishi wa Habari kutoka Aprili, 2010
Piga kura kuchagua “Blogu Bora Zaidi”
Upigaji kura mtandaoni umeanza kwa ajili ya Tuzo ya Blogu Bora Zaidi inayotolewa na Deutsche Welle (Shirika la Habari la Ujerumani), moja kati ya mashindano ya blogu yenye hadhi kubwa kimataifa na blogu zilizotajwa kushiriki ni za lugha kumi na moja tofauti. Unaweza kuipigia kura blogu uipendayo hadi April 14, 2010.
Urusi: Habari za Mwanzo za Milipuko ya Mabomu

Utaratibu wa Jumatatu asubuhi mjini Moscow ulivunjwa leo na milipuko ya mabomu mawili mabomu ya kujiua, ambayo yaliua watu wapatao 38 na kujeruhi kwa uchache watu wapatao 70. Alexey Sidorenko anatafsiri baadhi ya taarifa za mwanzo kutoka katika ulimwengu blogu za Urusi.