Habari kuhusu Vyombo na Uandishi wa Habari kutoka Julai, 2012
Angola: Raia Wadai Kampeni za Uchaguzi za Wazi
Asasi za kiraia nchini Angola zinatoa wito wa uwazi zaidi [pt] katika maandalizi ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika tarehe 31 agosti, 2012. Moja wapo ya miradi iliyozinduliwa hivi karibuni kwa lengo...
Tanzania: Kufungiwa ‘Mwanahalisi’, uhuru wa habari mashakani?
Mnamo tarehe 30 Julai, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Msajiri wa Habari ilitangaza kulifungia kwa muda usiojulikana gazeti la Kiswahili linalotoka mara moja kila wiki la 'MwanaHalisi'. Ulimwengu wa habari umepokea taarifa hiyo kwa mshtuko mkubwa. Hivi ndivyo wanaharakati wa mtandaoni wanavyoeleza hisia zao kuhusu tangazo hilo.
Afrika: Ujuzi wa Matumizi ya Zana za Habari za Kijamii kwa Vijana Wanaoishi na Ulemavu.
Warsha ya vijana walemavu kutoka kote barani Afrika lafanyika Dakar, Senegali. Warsha hii ilipangwa na DRI na YI. Imeandikiwa na Haute Haiku.
Palestina: Makala Kuhusu Kifo cha Arafat yaibua maswali
Kituo cha habari cha Al Jazeera hivi karibuni kilionyesha makala iliyohusu kifo cha utata cha rais wa Palestina Yasser Arafat kilichotokea mjini Paris mnamo Novemba, 2004. Makala hayo yanadai kwamba kiongozi huyo hakufa kifo cha kawaida, ila aliwekewa sumu ya poloni, madai ambayo yanaibua maswali mengi.
Tazama Picha za Afghanistan Ambazo Huwa Huzioni
Vyombo vingi vya habari vinavyovipoti hali inavyoendelea nchini Afghanistan hubeba taswira mbya. Kupitia miwani yao, Afghanistan huoneshwa kama nchi inayozama kwenye vimbi la mapigano na sura ya kijeshi. Wapiga kura kadhaa wanawasaidia watu kuona nchi hiyo iliyoathiriwa na vita lakini nzuri kwa mtazamo tofauti.