Afrika: Ujuzi wa Matumizi ya Zana za Habari za Kijamii kwa Vijana Wanaoishi na Ulemavu.

Open Society Foundation, Shirika la Uwazi katika Jamii wakishirikiana na Mpango wa Haki za Walemavu (Disability Right Initiative, DRI, wameungana kuunda shirika litakalowahudumia vijana wa ki-Afrika wenye ulemavu – Shirika litakaloitwa Mtandao wa Vijana wa ki-Afrika wenye Ulemavu.

Kupitia mtandao huo, vijana wenye ulemavu kutoka sehemu mbalimbali barani humu walipatiwa ujuzi wa kutumia zana za uandishi wa kijamii na jinsi ya kufanya kazi na kuonekana kama waandishi wa habar:

[…] kwa kutangazwa, kupitishwa na kuridhiwa kwa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za walemavu. YI na DRI (vifupisho vya majina) waliona haja kubwa ya kuunda shirika mahususi kabisa la kiafrika, iliyosababisha kuundwa kwa shirika hilo la kuwahudumia vijana walemavu wa ki-Afrika. Kundi hili liliundwa ili kuwaleta pamoja vijana kutoka barani barani kwa lengo la kuunda jamii zilizopamoja ambapo watu wenye ulemavu wanaweza kuishi maisha mazuri zaidi na yenye staha na kuchangia na hata kubadili mwelekeo wa mijadala ya ndani ya kisiasa

Washiriki wa Kongamano (kushoto kwenda kulia): Boaz, Gladys na Medi. Picha kwa hisani ya Rebecca Wanjiku

Hapo awali, mwezini huu, kongamano jingine lilifanyika mjini Dakar, Senegali na nchi nyingi kama Uganda, Kenya, Zambia na Tunisia ziliwakilishwa. Watu wenye ulemavu si tu hawapewi nafasi ya kutosha katika vyombo vikuu vya habari lakini hawapati nafasi kabisa. Warsha hii iliwawezesha vijana hawa wenye ulemavu kwa kuwapatia ujuzi wa namna bora ya kufanya kazi na hata kuchukua usukani wa vyombo vya habari hasa vya kijamii pamoja na mbinu za mawasiliano na kuandika.

Rebecca, mwanablogu wa Kenya, anaandika haya kuhusu warsha hiyo:

Nimekuwa na juma jema pamoja na kikundi cha vijana; nikitoa mafunzo ya kutumia vyombo vya habari, viwe hivi vipya au vile vya zamani huwa si rahisi. Vyombo vya habari katika kila nchi kwa kawaida vina hatia ya mambo yanayofanana; havitangazi masuala yetu, vinaongeza chuki na ubaguzi na mara nyingi havina muda wa kuandika na kutangaza habari chanya.

Warsha iliwaelimisha na kuwafunza vijana wenye ulemavu kuwafanya hatimaye waweze kuwafunza wananchi wengine namna ya kutumia zana kama twita na Facebook.

Rebecca anaandika:

Wengine wenu mkifikiria mafunzo ya vyombo vipya vya habari, labda mnafikiria nafanya vitu vigumu kama kutumia picha zenye ujumbe kufanya mtandao uwe na maingiliano au jinsi ya kuwa na AVI inayocheza kwenye mtandao wa twita. La, fikiria vitu rahisi kama kufungua ukurasa katika mtandao wa Facebook, umuhimu wa kujiunga na mitandao ya twita na Facebook, namna ya kuwatafuta watu wengine wanaotumia mtandao wa Twita nchini kwako na kufahamu sababu ya kwa nini wanafuatiliwa na watu wengi na kwa nini na kipi cha kufanya ili upate wafuasi wengi.

[…] hebu fikiria umekulia sehemu za vijijini nchini Uganda, ukiwa kwenye baiskeli ya walemavu, ukipewa motisha na mama ambaye anaamini kuwa lazima uelimika na kufikia uwezo wako bila kujali hali. Fikiria kusukuma baiskeli au kile kiti kinachotumiwa na walemavu kwenye matope wakati mvua ikinyesha, lakini zaidi ya yote fikiria wanafunzi wenzako unaosoma nao shule ya msingi walioamka masaa mawili kabla ili wakusukume maili hizo mbili hadi ufike shuleni kwako.

 

Maoni ya mshiriki mmoja wa warsha hiyo, “Kutokujua kwangu kulinifanya nikaamini kuwa kutumia zana za habari za kijamii ni jambo ngumu.” Picha kwa hisani ya Rebecca Wanjiku

Naibu Katibu Mkuu wa Utawala katika Shirikisho la Vijana wa Liberia, Daintowon Pay-bayee, anasema, “Ulemavu sio kukosa uwezo.” Kisha anaendelea kwa kuuliza, “umeyasikia maneno hayo kabla lakini mtazamo wako ni upi unapokutana na mlemavu kwa mara ya kwanza?” Bi Pay-bayee anakataa kuhukumiwa kwa kuwa ni mlemavu ndiyo maana ataendelea kuitimiza ndoto yake:

Ulemavu sio kukosa uwezo. Ili kupingana na ubaguzi na kubadilisha mtazamo wa watu, inatubidi tuanze kuongea kuhusu vijana wenye ulemavu majumbani mwetu, kwa majirani zetu, na hata kwa kiwango cha nchi na pia kote duniani. Wafadhili, serikali, na vyombo vya habari wanapaswa kuchukua hatua za haraka kushughulikiwa suala hili. Mitazamo ya walemavu ni ya kudhalilisha. Tunahitaji kuwatia moyo vijana wote ili kile kilichomo ndani mwao kitimie. Nitaendelea kupigania ndoto yangu ya kuishi katika jamii yenye usawa ambapo sitakuhumiwa kwa kile nisichoweza kufanya kwa sababu ya ulemavu wa mwili bali kwa uwezo na tabia zangu.

 

Daintowon Pay-bayee, mwanaharakati wa watu wanaoishi na ulemavu wa Liberia, anakumbuka alivyopata ulemavu wake akiwa na umri wa miaka tano.

Habari zaidi kuhusu warsha hii zinapatikana kupitia Ukurasa wa OSIWA , katika mtandao wa FacebookUkurasa wa OSIWA katika mtandao wa Twita na Ukurasa wa facebook wa Shirika la Vijana wenye ulemavu AYWDN

Mratibu wa mpango ya OSIWA, Kanja Sesay alitoa maoni yake kuhusu warsha hii kwa kupitia mtandao wa twita:

@MKSesay: ” Kwenu vyombo vya habari, kisiasa si sahihi tena kuzungumzia vipofu bali watu wanaoishi na ulemavu wa macho” – Tidiane Kasse

@MKSesay: “Vijana kote duniani wanafanya mambo makubwa”… Taarifa chanya kutoka kwa wanaharakati wanaotetea haki za walemavu wanaoshiriki katika warsha nchini Senegali.

@MKSesay: # Nchi za Afrika bado ziko nyuma katika kutetea haki za walemavu, vijana wanapaswa kuziwajibisha serikali zao.

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.