Tazama Picha za Afghanistan Ambazo Huwa Huzioni

Miongo ya vita na ugaidi vimeiweka Afghanistan katika kundi la nchi hatari zaidi kuishi duniani. Pamoja na hatua za mafanikio zilizofikiwa na nchi hiyo tangu kuondolewa kwa wa-Taliban mwaka 2001, vyombo vingi vya habari vinavyoandika habari za Afghanistan kwa ujeuri tu vimejikita katika masuala hasi kama vile milipuko ya mabomu, mashambulizi ya kujitoa muhanga na kujeruhiwa kwa watu. Ripoti katika vyombo hivyo zinaonyesha picha za kuogofya ambazo husababisha watu wengi kughairi kabisa mpango wa kuitembelea nchi hiyo iliyoathirika vibaya na mapigano lakini kwa asili ikiwa ni nchi nzuri sana.

Hii ndiyo sababu kazi ya Antony Loveless, mwanablogu Antony Loveless, mwandishi huru wa habari na mpiga picha wa Ki-Ingereza, inaleta tofauti kubwa. Tangu mwezi Machi 2012, Loveless amekuwa akiweka picha anazopiga katika safari zake nchini Afghanistan kupitia mtandao wa twita, kwa kutumia alama ishara aliyoitengeneza yeye, #TheAfghanistanYouNeverSee.

Akioongea na mwandishi wa Global Voices kuhusu alama ishara hiyo ya twita, Loveless alisema:

Nina jalada lenye picha zaidi ya 2,000 zilizopigwa katika safari zangu tatu nilizofanya nchini Afghaniistan katika miaka ya hivi karibuni na ili kuweka kumbukumbu hizo, niliamua kutengeneza alama ishara ya [#TheAfghanistanYouNeverSee].

Msichana katika Ziwa. Akiogelea kujipooza mwili baada ya jua kali la mchana. Picha ya Antony Loveless, imetumiwa kwa ruhusa.

‘Eneo Kijani’'s 'nchini Afghastan', pana lenye rutuba, lililolimwa pembezoni mwa Bonde la Mto Helmand. Picha ya Antony Loveless, imetumiwa kwa ruhusa.

Uzuri usiomithilika wa Ziwa Kajaki kusini mwa Afghanistani, kama unavyoonekana ukiwa juu kwa ndege ya Royal Air Force Chinnok. Picha ya Antony Loveless, imetumiwa kwa ruhusa.

Alama ishara hiyo ya Loveless ilitumiwa pia na Sajenti Alex Ford, wa Royal Air Force (RAF), aliishi kwenye jimbo la Hilmand nchini Afghanistan kwa muda wa miezi sita mwaka 2011.

Akielezea maoni yake kuhusu alama ishara hiyo ya twita, Ford anaandikakwenye Jarida la Warfare:

Tumekuwa tukijihusisha na masuala ya Afghanistan kwa takribani miaka 11 sasa, na imekuwa kawaida kuona picha za vita kutoka hapa. Lakini picha hizo kwa ujumla huwa zinaonyesha upande hasi wa mgogoro nchini humo. Picha za majeneza yaliyofunikwa bendera yakiingizwa Wootton Bassett au kutoka brize Norton…picha za mwanajeshi anayetabasamu, lakini maelezo chini yake yakitoa tarehe alipofariki dunia. Inasikitisha sana, wengi wa wa-Ingereza wanaounga mkono wanawake na akina dada walio kwenye eneo la tukio hawana taarifa halisi za habari za vita inayoendelea kule; habari ambayo inatokana na Afghanistan yenyewe.

Watoto wa nchi hiyo wakiwa tayari kuzungumza na Paras anayeondoka eneo hilo la kutua kwa Helkopta. Picha ya Picha ya Alex Ford, imetumiwa kwa ruhusa.

Watoto wa ki-Afghanistan wakionyesha vitabu na kalamu walizopewa na UNICEF darasani kwake. Picha ya Picha ya Alex Ford, imetumiwa kwa ruhusa.

Alama ishara hiyo imekuwa maarufu kwa wale wanaosafiri kwenda Afghanistan kubadilishana picha ambazo watu nje ya nchi hiyo huziona mara chache katika vyombo vya habari.

Mtoto wa ki-Afghan akionekana tayari kutumia kamera. Picha ya Steve Blake, imetumiwa kwa ruhusa.

Hivi karibuni,Iqbal Ahmad Oruzgani, mpiga picha kutoka Afghanistan ameanza pia kuweka picha kwenye alama ishara hiyo hiyo ya mtandao wa twita kwa mtazamo tofauti.

Harusi za pamoja zilizoandaliwa kwa ajili ya kufungisha ndoa za makumi ya maarusi huko Daikundi, katikati ya Afghanistan. Harusi za pamoja zimekuwa maarufu nchini humo kwa sababu hupunguza gharama za harusi kwa kila familia ya maarusi. Picha ya Iqbal Ahmad Oruzgani, imetumiwa kwa ruhusa.

Wasichana wa ki-Afghan wakisoma kitabu cha shule mbele ya duka lililofungwa. Picha ya Picha ya Iqbal Ahmad Oruzgani, imetumiwa kwa ruhusa.

Kipindi cha baridi katika wilaya ya Behsud iliyopo katika Jimbo la Maidan Waedak. Picha ya Iqbal Ahmad Oruzgani, imetumiwa kwa ruhusa.

Kila picha iliyowekwa katika alama ishara hiyo ya twita hutwitiwa tena (retweeted) na mamia ya watumiaji wa twita, kuwawezesha wapiga picha hao kupata hadhira kubwa zaidi.

Akizungumza na Global Voices, Antony Loveless anasema:

Watumiaji wasiohesabika wa twita wanasema hayo ni matumizi mazuri zaidi ya alama ishara za twita, kuliko ilivyopata kutokea, na hivi sasa niko kwenye mazungumzo kuchapisha kitabu kinachotokea na alama habari ya twita baada ya watu wengi mno kuonyesha nia ya kukinunua ikiwa kitachapishwa.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.