Misri na Aljeria: Pambano la Twita

Katika sehemu nyingi duniani, hakuna linalounganisha zaidi – au wakati mwingine kutenganisha – zaidi ya pambano la mpira wa miguu. Washabiki wa Misri na Aljeria, katika ulimwengu wote wa Waarabu na zaidi, walilidhihirisha hilo Jumamosi hii wakati timu zao zilipokwenda sambamba wakati wa kuwania kuingia fainali za Kombe la Dunia huko Afrika Kusini. Wakati vihoro vilipanda juu huko mjini Cairo, pia vilikuwa hai na katika hali nzuri kwenye uwanja yakini mtandaoni, pamoja na kwenye Twita, ambako watumiaji walitaarifu kuwa skrini zao zilijaa hisia za mpira. Mtumiaji wa Twita mbaa alituma picha ya skrini yake, ambayo ilifurika mazungumzo ya pambano hilo:

Ujumbe wa twita kutoka kwa Mmisri embee ulionyesha ushabiki uliokithiri wa baadhi ya washabiki:

Baadhi ya taarifa zinadai kuwa tiketi zote zimekwishauzwa hivi sasa! Wakati huo huo, Mmisri NoraYounis alielezea kutoamini kwake katika nguvu ya kuunganisha ya mpira wa miguu kwa Wamisri:

Ujumbe wa twita wa Mmisri NohaAtef, kwa upande mwingine, ulionyesha vitu vinavyoweza kuinua mioyo katika mpira wa miguu:

Katika mifano mingi, mpira wa miguu ulichimbua ushindani wa kitaifa. Waaljeria na Wamisri walikwenda kichwa kwa kichwa kwenye twita wakati pambano likiendelea. Mmisri Sandmonkey aling’aka:

Mualjeria-Mmarekani themoornextdoor alijibu mapigo akitania:

Mwishowe, Mualjeria reemba alitukumbusha kuwa mambo bado hayajaisha mpaka yaishe:

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.