Brazil: Mtazamo wa Wakazi wa Vitongoji Maskini

Wiki iliyopita, picha za vita kati ya wasafirishaji na wafanyabiashara ya madawa ya kulevya mjini Rio de Janeiro zilitapakaa duniani. Tarehe 17 Oktoba, mapambano kati ya magenge yanayotokea vilima vya Morro Sao Joao na Morro dos Macacos yaliwatisha watu. Mamia ya askari wa jimbo walipelekwa katika juhudi za kudhibiti magenge hayo yanayoshindana lakini haikusaidia: ugomvi kati ya wafanyabiashara wa madawa ya kulevya na polisi yalipelekea kutunguliwa kwa helikopta ya polisi na vifo vya polisi watatu, na kuchukua maisha ya zaidi ya watu 30 wengine, miongoni mwao wakiwemo watu wanaotuhumiwa kuwa wanachama wa magenge na wapiti njia.

Wakati helikopta inalipuka. Picha na Taiane Oliveira kwenye Twitpic.

Wakati helikopta inalipuka. Picha na Taiane Oliveira kwenye Twitpic.

Blogu ya Censurado inaukosoa mtizamo wa gavana katika mgogoro huu, baada ya kusikia habari zinazoashiria kuwa polisi hawakujua chochote juu a uvamizi:

Vocês viram as cenas na televisão este fim de semana? Helicóptero caindo, policial morrendo queimado, inocente metralhado nas ruas e traficante invadindo a favela do outro em plena luz do dia, uma verdadeira cena de filme de guerra. Dizem no Rio que até o serviço secreto israelense sabia que um morro atacaria o outro, mas mesmo assim o governador Sérgio Cabral diz que a policia carioca não sabia de nada? Acho que ele anda passando muito tempo com o Lula. Só isso explica essa ‘ignorância’ sobre o tema.

Je uliiona habari katika televisheni mwishoni mwa juma hili? Helikopta akianguka, polisi wanaungua moto, watu wasio na hatia wanapigwa kwa risasi mitaani na wauza madawa ya kulevya wakivamia vitongoji vya wauzaji wengine mchana kweupe; kama picha kutoka kwenye sinema ya vita. Mjini Rio, watu wanasema kuwa hata shirika la kijasusi la Israel lilikuwa linafahamu kuwa wauza madawa ya kulevya wangeeenda kuwashambulia wauzaji wengine, lakini bado gavana Sergio Cabral alisema kuwa polisi wa carioca walikuwa hawafahamu lolote? Nadhani anatumia muda mwingi na [rais wa Brazil] Lula. Hiyo ndiyo sababu pekee ya “kutokufahamu kwake” juu ya suala hili.

Mwanablogu Ana Maria [pt] anasema kuwa kuitungua helikopta siyo kazi rahisi na kuonyesha kuwa huu unaweza ukawa ni mwanzo tu. Anasema[pt]:

Mas os senhores do tráfico, donos dos morros cariocas possuem não apenas as armas capazes disso, possuem indivíduos capazes de manuseá-las e causar um desastre como o do sábado.
Isso vai ficar marcado para sempre na memória da PM e do cidadão de bem, morador do estado do Rio de Janeiro.
Se eles podem fazer isso com um helicóptero da polícia tripulado por homens treinados, que dão a vida pela segurança pública, o que podem fazer com o cidadão comum?
Não vou “tapar o sol com peneira”.
As coisas podem piorar.

Sio tu vigogo wa madawa ya kulevya, bali pia wamiliki wa makazi ya masikini katika carioca, wanazo bunduki zenye uwezo wa kufanya jambo kama hilo mikononi mwao, na pia wanao watu waliofundishwa kuzitumia na kusababisha janga kama la Jumamosi iliyopita.
Tukio hili litaacha lama katika kumbukumbu za Polisi na raia wa kawaida, wakazi wa jimbo la Rio de Janeiro.
Kama wanaweza kufaifanyia hivi helikopta inayoendeshwa na watu waliofuzu, ambao wametoa maisha yao ili kutoa usalama kwa umma, je wanaweza kufanya nini kwa raia wa kawaida?
Siwezi “kulificha jua kwa chujio”.
Mambo yanaweza kuwa mabaya zaidi.


Maelezo ya wakazi juu ya vita vya madawa ya kulevya

Mwanamke aliyembeba mtoto anatembea bila kujali mbele ya maofisa wa polisi wanaofanya doria katika Morro dos Macacos

Mwanamke aliyembeba mtoto anatembea bila kujali mbele ya maofisa wa polisi wanaofanya doria katika Morro dos Macacos

Mradi wa habari wa jamii Viva Favela [pt] unatoa maelezo ya wakazi walioshuhudia kwa macho ugomvi huu. Waandishi wao wa kiraia – ambao wote wanaishi katika mstari wa mbele wa mapambano – wamekusanya maoni kutoka kwa wakazi wa kwenye maeneo hayo na picha za siku ambayo vita vya madawa ya kulevya vilianza jijini Rio de Janeiro.

Mtu wa kwanza kusikilizwa na Viva Favela alikuwa Hugo Mattos, ambaye anaishi kwenye mtaa ambao ndio njia ya kuelekea kwenye eneo ambalo matukio yalijiri (Morro dos Macacos). Alisema kuwa wauza madawa ya kulevya walitumia bunduki zenye nguvu ya juu na akaongeza kuwa kuna aina fulani ya hofu ya jumla kwamba ikiwa polisi watalichukua tena eneo linalokaliwa na wauza madawa ya kulevya, patazuka machafuko mabaya kama jibu kutoka kundi linalotawala Morro dos Macasos:

O tiroteio começou por volta das duas da manhã e só terminou às oito horas, quando a policia chegou. Muita gente teve que dormir fora de casa nesse dia.

As pessoas dizem que ninguém deve sair de casa depois das 10 horas, porque algo pode acontecer.

Kutupiana risasi kulianza kwenye majira ya saa 8 za usiku na kumalizika saa 2 asubuhi wakati polisi walipowasili. Iliwabidi watu wengi walale nje ya nyumba zao usiku ule. Watu wanasema kuwa hakuna anayepaswa kutoka nyumbani kwake baada ya saa 4 za usiku, kwa kuwa lolote linaweza kutokea.

Kwa mujibu wa Viva Favela, taarifa kama hizi huletwa wakati wote kutoka kwa wakazi wa maeneo hayo, ambao hawana uwezo wa kufanya lolote. Jioni ya Jumanne tarehe 20 Oktoba, wakazi wa Morro Sao Joao waliandamana kutokana na hofu ya kuvamiwa kama majibu (ya wauza madawa walioshambuliwa awali), hofu ambayo ilitajwa kuwa haikuwa na msingi wowote na Mkuu wa jeshi la Polisi, Kanali Mario Sergio Duarte. Hata hivyo, watu walikwishaingiliwa na hofu. Mkazi mwingine wa Morro dos Macacos, Karen Carolina Nascimento anasema kuwa kutupiana risasi kati ya wauza madawa ya kulevya na polisi kumekuwa kukiendelea kwa miezi miwili. Anahofu mgogoro mpya:

Já era praticamente uma rotina, mas no último sábado foi diferente. O confronto aconteceu por causa de uma tentativa de invasão e não foi a primeira vez que os traficantes do Morro São João tentam. O comentário que se escuta no morro é que a facção rival deu uma ordem para tomar o Morro dos Macacos até dezembro e que esses bandidos tiveram ajuda de policiais para tentar invadir.

O policiamento não está reforçado e os moradores estão muito apreensivos com medo de uma outra invasão. Eu trabalho no pé do Morro São João e vou para a minha casa andando. Ontem só havia um único carro com dois policiais dentro parado em uma esquina. Em cima do morro não existe policiamento nenhum. Uma vez ou outra um carro blindado sobe e faz uma ronda. Estamos com muito medo porque com certeza a facção rival vai tentar tomar novamente.

[Vita vya Magenge] vimekuwa ni kama kama kawaida, lakini jumamosi hii ilikuwa tofauti. Mgogoro ulianza kwa sababu ya jaribio la kuivamia Morro dos Macacos lililofanywa na wauza madawa ya kulevya kutoka Morro Sao Joao, na hili halikuwa jaribio la kwanza. Neno lililokuwa kwenye kwenye makazi ni kuwa kundi shindani limetoa amri ya kuiteka Morro dos Macacos ifikapo mwezi Desemba na kwamba maofisa wa polisi walikuwa wanawaunga mkono wauzaji hao.
Doria ya polisi haitekelezwi na wakazi wana wasiwasi mkubwa, wanahofia uvamizi mpya. Ninafanya kazi chini ya bonde la Morro Sao Joao na hutembea ninaporudi nyumbani. Jana, kulikuwa na gari moja tu lililokuwa na maofisa wawili wa polisi ndani yake lililoegeshwa kwenye kona. Hakuna doria ya polisi juu kwenye makazi. Mara moja moja kwa nadra gari iliyokingwa (mithili ya gari ya jeshi) huja huku juu na kufanya doria. Tumo kwenye hofu kubwa kwani tuna hakika kuwa kundi shindani litajaribu kulikomboa eneo.

Viva Favela [pt] pia inatoa maoni ya Wagner da Silva de Barros, mwenye umri wa miaka 29 ambaye ni mkazi wa Vila Penheiro kutoka Complexo da Mare, anayesema kuwa athari za mgogoro katika Morro dos Macacos umefika mbali kiasi hiki kwa sababu ya helikopta iliyotunguliwa na anaongeza kuwa vita hii itaenea pia kwenye jamii nyingine nyingi:

A queda do helicóptero e a morte dos três policiais chocou parte da população, mas na Maré, durante cinco meses, nós vivemos um confronto entre facções que matou muita gente, inclusive moradores que nada tinham a ver com o tráfico, e não teve nem metade da divulgação que esse tiroteio dos Macacos está tendo.

Esses tiroteios reforçam de que na favela só existe bandido e violência, mas o que muitas pessoas ignoram é que trabalhadores morrem durante os conflitos e são logo identificados como traficantes pela polícia.

Kuanguka kwa helikopta na vifo vya maofisa watatu wa polisi kulishtua sehemu ya wakazi wa kwenye vitongoji, lakini Mare [vitongoji hivyo vya hali ya chini], kwa miezi mitano, tumeishi katika ugomvi baina ya makundi ambao umeua watu wengi zaidi, pamoja na wakazi ambao hawakuwa na uhusiano wowote na biashara ya madawa ya madawa ya kulevya, na hawa hawakupata hata nusu ya habari zilizotangazwa na vyombo vya habari juu ya mapambano ya risasi katika Morro dos Macacos.
Mapambano haya ya risasi yanasisitiza ukweli kuwa katika maeneo ya maskini (favelas) kuna majambazi na machafuko, ila jambo ambalo watu wengi hawafahamu ni kuwa wafanyakazi hufariki wakati wa machafuko na haraka polisi huwatangaza kama wauza madawa ya kulevya.

Kwa mujibu wa Viva Favela [pt], katika kesi ya Morro dos Macacos, vijana watatu wa kiume wasio na hatia ambao waliuwawa kwa risasi walijumuishwa kwenye orodha ya majambazi waliouwawa. Katibu wa Usalama Jose Mariano Beltrame alijirudi na kuomba msamaha kwa familia za Marcelo Costa Gomes, 26, Leonardo Fernandes Paulino, 27, na Francisco Haílton Vieira Silva, 24. Walikuwa wanarudi nyumbani kutokea kwenye hafla wakati uvamizi ulipotokea. Kijana wa nne, mhudumu wa hoteli Francisco Alaílton Vieira da Silva, 22, aliokolewa na wakazi na hivi sasa yuko hospitali katika kitengo cha huduma maalum. Mpenzi wake wa kike ni mjamzito wa miezi 3.

Walter Mesquista wa Viva Favela pia anatoa picha za mgogoro huo zilizopigwa na mpiga picha Guillermo Planel siku ambayo watu wanaiita “Vita vya Mihadarati”.

Kuna mauaji takriban 6,000 kwa mwaka katika jimbo zima la Rio, ambalo lina wakazi milioni 14. Operesheni “Eneza Amani” yenye doria ya kudumu imekuwa ikitekelezwa kwa mwaka mzima katika vitongoji vitano. Ongezeko la uwepo wa polisi vitongojini kunayalazimisha magenge kupigania maeneo mengine.

Viva Favela ni mradi wa uanahabari wa kijamii ambao unafanya kazi na wanablogu malum pamoja na wapiga picha ambao wanaishi katika maeneo maskini ya Rio de Janeiro. Mradi huo uko chini ya uongozi wa Mhariri Rodrigo Nogueira. Unaweza kupata taarifa zaidi katika akaunti yao rasmi ya Twita [pt] na katika jamii ya Orkut [pt].

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.