Habari kutoka 28 Disemba 2012
Assad atumia Ndege ya Kivita Kuwaua Raia Wake
Serikali ya Syria imefanya shambulizi kubwa la angani dhidi ya raia wa nchi hiyo -waliokuwa wamesimama kwenye foleni waisubiri mikate kwenye kiwanda cha kuokea miakte huko Halfaya, Hama. Inakadiriwa kwamba watu waliouawa katika shambulio hilo mjini humo ni kati ya 90 na 300, waasi wakisema kuwa watu hao walikuwa wamejitenga na vikosi vya Assad. Mtandaoni, wanaharakati wanashangazwa inakuwaje dunia inaendelea kutazama tu maisha ya watu wasio na hatia wakiuawa kwa mamia.