Habari kuhusu Asia Mashariki kutoka Mei, 2014
Mwimbaji Mwingine Akamatwa China kwa Kuusifu Utamaduni wa Kitibeti
Kufuatia kukamatwa kwa mwimbaji wa Kitibeti Gepe nchini China,hapa ni mtiririko wa matukio ya jinsi hiyo sambamba na video za nyimbo husika kwenye mtandao wa YouTube.
Macau: Watu 3,000 Wazunguka Baraza la Wawakilishi Kukwamisha “Muswada wa Walafi”
Taarifa zaidi zinapatikana kwenyetaarifa yetu ya awali ya GV.
PICHA: Watu 20,000 Waandaman huko Macau China Kupinga “Muswada wa Ulafi”
Muswada utampa mkuu wa serikali jimboni Macau, nchini China, kinga ya kushitakiwa kwa makosa ya kijinai wakati akiwa madarakani na ataaendelea kupata mshahara wake hata baada ya kuondoka madarakani.
Baada ya Miezi Sita, Waathirika wa Kimbunga Haiyan Waendelea Kudai Msaada na Haki
Miezi sita baada ya kimbunga kikubwa kuharibu mamiliaoni ya makazi katika eneo la katikati ya Ufilipino, wahanga wanaendelea kuomba misaada na kutendelewa haki. Kuna madai ya kukosekana kwa mpango wa kurejesha hali kuwa ya kawaida.
Udikteta Umekwisha Lakini Uhuru wa Habari Bado ni Tishio Nchini Myanmar
Irrawaddy alisisitiza kuendelea kwa matatizo yanayowakabili waandishi wa habari nchini Myanmar licha ya mageuzi kutekelezwa na serikali …Licha ya mabadiliko yanayoonekana katika jinsi serikali inavyotumikia vyombo vya habari, mawazo ya...
‘Hali Mbaya’ ya Haki za Binadamu Nchini Vietnam
Mtandao wa haki za Binadamu illitoa ripoti yake ya 2013 kuhusu ‘hali mbaya’ ya haki za binadamu nchini Vietnam: …. Hali ya haki za binadamu nchini Vietnam iligeuka na kuwa...
Wakati Mgogoro wa Kisiasa Ukikolea: Thailand Kufanya Uchaguzi Mwingine Mwezi Julai
Kwa sababu ya kushindwa kwa uchaguzi wa mwezi Februari kutatua mgogoro wa kisiasa nchini Thailand, uchaguzi mwingine umepangwa kufanyika Julai 20. Lakini je, upinzani utasusia kwa mara nyingine?
China Yamweka Kizuizini Mwanasheria wa Haki za Binadamu Pu Zhiqiang
Hii si mara ya kwanza kwa Pu Zhiqiang kuwekwa kizuizini. Akiwa mkosoaji maarufu wa sera za serikali ya China, amekuwa akifuatiliwa kwa karibu na vyombo vya usalama wa nchi hiyo.
PICHA: Waandamanaji Nchini Taiwani Wageuza Uzio wa Polisi kuwa Mapambo
Polisi waliweka uzio wa kuwapa tahadhari waandamanaji kuzunguka majengo ya serikali katika jitihada za kuwazuia waandamanaji kukusanyika. Wataiwani wakawajibu kwa kile kinachoonekana kuyageuza mabango hayo ya tahadhari kuwa mapambo.