Habari kuhusu Asia Mashariki kutoka Disemba, 2009
Je, China Iliharibu Makubaliano ya Copenhagen?
Uln alijaribu kuchambua ni nini kilichotokea Copenhagen na kuhoji kwa nini nchi zinazoendelea hazikusaini baina yao wenyewe makubaliano ya kupunguza utokaji wa gesi ya ukaa. Inside-Out China ametafsiri taarifa inayosimulia...
Malaysia: Mtetezi wa Uhuru wa Vyombo vya Habari Amshtaki Mwanablogu
Mwanahabari-mwanablogu mkongwe anashtakiwa katika kesi ya madai na mwanasiasa anayejulikana kwa kutetea uhuru wa habari nchini Malaysia. Angalia maoni ya wanablogu wa Malaysia.
China na Iran: #CN4Iran
Jana, maelfu ya Wa-Irani waliingia mitaani ili kupinga dhidi ya utawala wa kiimla. Maandamano hayo yaliwakumbusha watu wa China juu ya vuguvugu la demokrasi la Tiananmen la 1989 na watumiaji...
Singapore: Kampeni ya “Kataa Ubakaji”
Nchini Singapore, mara nyingi kumbaka mke wako hakuchukuliwi kama tendo la kubaka. Waandaji wa kampeni ya “Kataa Ubakaji” wanataka kukomesha sheria inayokinga ubakaji ndani ya ndoa kwa kuzindua kampeni ya kukusanya saini ambazo zitawasilishwa kwa watunga sera. Wengi wa raia wa mtandaoni wanaiunga mkono kampeni hii.
China: Kujitoa Uhai kwa Msomi Mwingine tena – Kisa cha Yang Yuanyuan
YANG Yuanyuan, binti msomi mwenye miaka 30 aliyekuwa na shahada ya uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Shanghai Maritime, alijinyonga kwenye bafu la nyumbani kwake mnamo Novemba 25 mwaka huu. Siku...
China: Uvunjaji Nyumba kwa Kutumia Mabavu
Visa viwili vya uvunjaji nyumba kwa mabavu vimeibua hisia za kutaka kulindwa zaidi kwa haki za raia na utatuzi wa migogoro nchini Uchina. Watumiaji wa mtandao wa Kichina wanatoa maoni.
Indonesia: Sarafu za Kudai Haki
Raia wa mtandaoni (Netizens) wamezindua kampeni ya kukusanya fedha zilizo katika muundo wa sarafu ili kumuunga mkono Prita Mulyasari, mama wa nyumbani raia wa Indonesia aliyeandika malalamiko yake mtandaoni dhidi ya hospitali iliyotoa huduma mbaya, na ambaye alipatikana na hatia na mahakama moja ya kosa la "kuchafua jina" la hospitali hiyo binafsi.
Thailand: Waziri Mkuu wa Zamani Afariki Dunia
Samak Sundaravej — Gavana wa Zamani wa Bangkok, mwendeshaji wa kipindi cha mapishi, na Waziri Mkuu wa 25 wa Thailand amefariki dunia tarehe 24 Novemba. Soma maoni ya wanablogu na wanatwita wa Bangkok
China: Barafu Iliyotengezwa Uchina
Jumapili hii iliyopita tarehe 1 Novemba, Beijing ilishuhudia kuanguka kwa mapema zaidi kwa theluji katika miaka 22 iliyopita. Badiliko hilo la ghafla la hali ya hewa, lililofunika kabisa mji mzima...