China: Barafu Iliyotengezwa Uchina

Jumapili hii iliyopita tarehe 1 Novemba, Beijing ilishuhudia kuanguka kwa mapema zaidi kwa theluji katika miaka 22 iliyopita. Badiliko hilo la ghafla la hali ya hewa, lililofunika kabisa mji mzima kwa barafu, liliwashangaza wakazi wengi. Lakini vyombo vya habari viliripoti baadaye kwamba uangukaji huo wa barafu ulisababishwa na ofisi ya kurekebisha hali ya hewa mjini hapo.

Maelezo nyuma ya mvua hiyo bandia ilikuwa ni kwa sababu Beijing imekuwa ikikabiliana na ukame. Usiku kabla ya barafu, serikali ililipua angani kemikali ya fedha ya ayodaidi. Athari zilizojitokeza ni kuongezeka kwa theluji kwa tani milioni 16.

“Hatutapoteza fursa yoyote ya kutengeneza mvua bandia kwa kuwa Beijing inakabiliwa na ukame unaotishia, ” alisema Zhang Qiang, kiongozi wa ofisi ya kurekebisha hali ya hewa, kwa vyombo vya habari vya taifa.

China ina historia ya kutengeneza mvua kwa kulazimisha, hasa wakati wa kujaribu kusitisha ukame. Katika nyakati nyingine, ofisi ya kurekebisha hali ya hewa imepunguza mvua kuhakikisha anga linakuwa tupu, mfano wakati wa gwaride la Siku ya Uhuru au wakai wa michezo ya Olimpiki.

Wanamtandao wamegawanyika katika mitazamo yao kuhusu barafu hii iliyotengenezwa mwishoni mwa juma lililopita. Wengine waliandika kwa ushabiki kuhusu uzuri wake, kama mwanablogu,鱼干儿.

北京的天气,总是这么让人匪夷所思。毫无预兆的就下了场雪,而且还一发不可收拾。听说是人工催下来的,管他呢,我们就爱这样的天气。

Hali ya Hewa ya Beijing ni nzuri kupindukia. Bila tahadhari, barafu ilianza kudondoka. Na ilikuwa aina ya barafu ambayo isingeweza kusafishwa kiurahisi na kudhibitiwa. Nilisikia kwamba barafu hiyo ilikuwa ya kutengenezwa. Lakini sijali. Tunapenda hali ya hewa ya aina hii.

Wengine, hata hivyo, wamekerwa. Anaandika 小米

回来才听说这是场人工降雪,是谁这么主观的断定这是下雪的好时机呢??到处都是措手不及的冷,电力、交通、供暖等都遇到很棘手的问题。

Niliposikia kuwa barafu hiyo ni ya kutengenezwa, ilibidi nishangae ni mtu gani aliyewaza kuwa huu ulikuwa ni wakati sahihi wa barafu kuanguka? Kila mahali watu walikutwa bila ya kujiandaa na baridi na matatizo mengine mabaya yanayohusiana na umeme, msongamano na mfumo wa kupasha nyumba joto.

Katika jukwaa la mtandaoni, mtumiaji mmoja alilalamika kwamba seriali ilipaswa kuwatahadharisha watu kabla ya wakati, na kuongeza kwamba safari nyingi za ndege kwenye viwanja vya ndege zilicheleweshwa.

要我说,这种人定胜天的精神是好的,虽然北 京人都“被冬天”了,如果真能解除北方旱情也算是功德一桩。就是没通知大家的气象局太不地道。

Kwa mtazamo wangu, aina hii ya moyo wa ‘mwanadamu kuyashinda maumbile ya asili’ ni mzuri, ingawa wakazi wa Beijing ‘walilazimishiwa’ kipindi cha baridi. Kama wanaweza kutatua kweli madhara yaliyotokana na ukame basi kufanya hivi kuna faida. Lakini namna kitengo cha hali ya hewa kilivyoshindwa kumjulisha yeyote kabla ya wakati si sahihi kabisa.

Makala chache zilizofika kwenye mtandao zimeonyesha wasi wasi kuhusu aina gani ya madhara barafu isiyo ya asili inaweza kuwa nayo kwenye mazingira. Mwanablogu mmoja天边的云, alishangazwa kama kuna mtu ana haki ya kubadili hali ya hewa.

但是,在我们还不能完全掌握天气变化的规律时,就盲目改变局部的天气,是否会对 整个环境造成更大的不利影响呢?比如,这次因为北京缺水,就让原本要下到山东(假设而已)的雪在北京下了,会不会造成山东更缺水呢?

Lakini pale tunapobadili hali ya hewa kijinga kabla ya kuweza kudhibiti kanuni zake, je, hii haitaathiri sana mazingira kwa ujumla? Kwa mfano, barafu iliyotokea wakati huu ilikuwa ni kwa sababu Beijing ilikuwa inakabiliwa na ukame. Itakuwaje kama barafu hii ilikusudiwa kuangukia Shandong (hebu na tujifikirie hivyo kwa muda), badala ya Beijing. Je, hii haitasababisha ukame mkubwa zaidi katika Shandong?

Alex Pasternack, mwanablogu na mwandishi mjini Beijing, aliandika makala kwenye Tree Hugger akifafanua madhara ya kutengeneza mvua bandia kunakofanywa na mwanadamu.

Ukame umeathiri heka 800,000 za mashamba kufikia mwishoni mwa Oktoba, vyanzo rasmi vilikadiria, na tufani ya barafu inasemekana kuwa ilihitajika sana kama msaada kwa wakulima wa sehemu hiyo.

Lakini si wakulima wote katika eneo hilo waliofaidika. Athari moja wapo inayowezekana ya kubadilishwa huku kwa hali ya hewa ni kwamba inabadili uelekeo wa unyevu unyevu kutoka kwenye maeneo mengine ambayo yanauhitaji vile vile, kwa minajili ya kutengeneza mvua kubwa katika eneno linalokusudiwa.

Wanamtandao wengine wameanza utani kuhusu barafu hiyo. Elizabeth Kain aliandika kwenye blogu yake:

Barafu ya jana ilikuwa ya mapema zaidi katika miaka kumi. Nina hakika mama yangu, aliyekaa kwenye uwanja wa ndege wa Beijing kwa masaa saba kwa sababu tu safari zote za ndege zilizovurugwa na kukatishwa kuingia na kutoka mjini, atafurahi kujua usumbufu wote huo ulisababishwa na serikali.

Maoni mengine juu ya barafu hiyo pia yalitoa uchunguzi wenye akili:

Martin M. Novemba 2, 2009 saa 3:30 pm

Kila kitu kinatengenezwa China, hata barafu

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.