Habari kuhusu Asia Mashariki kutoka Agosti, 2010
Malaysia: Je, Uhuru wa Habari Unaelekea Wapi Sasa?
Picha uliyonayo ni kwamba Malaysia inaweza kuwa ni moja ya nchi zinazokua haraka kiuchumi katika bara la Asia, lakini je unafahamu kuwa ilikuwa katika nchi tatu za mwisho (nchi ya 131) kwenye masuala ya uhuru wa vyombo vya habari? Je wananchi na vyama vya upinzani vinavyopigana dhidi ya uchujwaji wa habari wanapata ahueni? Tutajua ukweli kwa kuangalia hali ya sasa ya uhuru wa vyombo vya habari nchini Malaysia.
China: Pato la Taifa Linaongezeka, Matumizi Katika Huduma za Jamii je?
Tunaendelea kusikia kuwa uchumi wa China unaendelea kukua; je matumizi ya huduma za jamii yameongezeka? Akiba binafsi zinabaki kwenye benki, anaandika mwanablogu mmoja: kutokea hospitali mpaka shuleni mpaka malipo ya uzeeni, China haiwezi kujilinganisha.
Ufilipino: Maoni ya Wanablog Juu ya Elimu ya Ya afya ya Uzazi
Mwaka huu wa masomo serikali ya Philippines inatekeleza mpango wa elimu ya uzazi kwenye shule za umma unaofadhiliwa na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya watoto na vijana. Na wanablogu wametoa maoni juu ya suala hilo.
Korea Kusini: Maombolezo ya Kitaifa ya Mwanamwali wa Kivietnam
Mwanamwali mdogo wa Kivietnam aliuwawa na mumewe wa Kikorea nchini Korea. Wanablogu wa Korea wanatoa rambirambi zao kwa kifo kibaya cha mke huyo mwenye umri mdogo huku wakiitaka serikali kutokomeza eneo hili lisiloonekana kwa urahisi la haki za binaadamu, linalohusiana na wachumba kutoka nchi za kigeni.
Udhibiti Nchini Singapore
Singapore imesababisha kelele kubwa baada ya kupiga marufuku filamu ya aliyewahi kuwa mfungwa wa kisiasa na kumkamata mtunzi Mwingereza wa kitabu kilichoandiaka kuhusu adhabu ya kifo nchini humo. Wanablogu wanajadili.