· Julai, 2010

Habari kuhusu Asia Mashariki kutoka Julai, 2010

Thailand: Vurugu Zinazotokana na Ujumbe Mfupi wa Maneno wa Waziri Mkuu

  27 Julai 2010

Wakati Waziri mkuu wa Thailand Abhisit Vejjajiva alipotwaa madaraka mwaka 2008, alituma ujumbe mfupi wa maneno kwa mamilioni ya wateja wa simu za viganjani wa Thailand akiwataka wawe na umoja. Hivi sasa anakabiliwa na makosa ya ufisadi kwa kupokea "zawadi" kutoka mashirika ya mawasiliano. Kadhalika anashutumiwa kwa kuvunja mipaka ya ya faragha za wateja wa simu za viganjani.

Asia ya Kusini Mashariki : Ngono na Udhibiti wa Mtandao

  26 Julai 2010

Uratibu wa maudhui katika intaneti unaonekana kana kwamba ni kinyume na demokrasia lakini serikali za Kusini Mashariki mwa Asia zinaweza kuhalalisha kitendo hicho kwa kuzusha haja ya kuwaokoa vijana kutoka kwenye janga la tabia za ngono holela.

Kambodia: Je, Viwango vya Maadili Miongoni Mwa Watawa Vinaporomoka?

  12 Julai 2010

Mtawa nchini Kambodia alikamatwa kwa akichukua picha za video za wanawake waliokuwa uchi katika jumba la watawa. picha hizo za video zilisambazwa sana kwa kutumia simu za viganjani na intaneti. Pia kuna taarifa nyingine za watawa kulewa na kuangalia filamu za ngono. Wanamtandao wa Kambodia wanatoa maoni

China: Nchi Imara, Watu Maskini

  9 Julai 2010

Shirika la utangazaji la taifa CCTV liliweka wazi mnamo tarehe 28 Juni kuwa China inatarajia kupata yuani trilioni 8 (sawa na dola trilioni 1.18) katika mapato ya fedha kufikia mwisho...