China: Nchi Imara, Watu Maskini

Shirika la utangazaji la taifa CCTV liliweka wazi mnamo tarehe 28 Juni kuwa China inatarajia kupata yuani trilioni 8 (sawa na dola trilioni 1.18) katika mapato ya fedha kufikia mwisho wa 2010. Mapato hayo kitaifanya China kuwa nchi ya pili kwa ukubwa wa mapato ya fedha baada ya Marekani. Inaoneka kuwa China imefanikisha ndoto yake ya kuwa taifa imara, hata hivyo, raia wa kwenye mtandao wamekuwa na mashaka kuhusu taarifa hiyo kwa sababu ya mgawanyo wa utajiri usio sawa.

“Hatua Kuu Mbele” katika mapato ya fedha

Mtaalamu wa mambo katika wavuti, Hou Jinliang, anasema kuwa “Hatua Kuu Mbele” ya namna hiyo haistahimiliki.

财政收入飞增,就像一个人吃了激素一样猛 长,外表很好很强大,很光鲜,可实质上是孱弱的。中国基尼系数超过国际警戒线,贫富差距日益拉大,劳动者之间分配不公…
…财政“坐火箭”, 一飞冲天,拿下了老二的位子,而民众的收入还在“骑蜗牛”。国际货币基金组织在2010年4月21日发布的数据显示,中国2009年的人均收入世界排名第 109位。可见,财政“大跃进”并不是一件值得吹嘘的事情,反而值得好好反思!

Hatua Kuu Mbele ya mapato ya fedha ni sawa na mtu anyetumia madawa ya kuongeza nguvu za kiume ya andrijeni, muonekana wake ni imara mno, lakini, katika ukweli, ni dhaifu mno kwa undani. Vipimo vya takwimu vinavyopima ukosefu wa usawa katika mgawanyo wa mapato na utajiri vya Gini vinaakisi ongezeko la tofauti katika vipato na ukosefu wa haki za kijamii…

…na sasa vile mapato yetu ya taifa yamepakia katika kombora na kuwa ya pili duniani. Kwa upande mwingine, vipato vya watu vinaendelea kupakiwa ndani ya konokono. Takwimu za IMF za tarehe 21, Aprili, 2010 zilionyesha kwamba kipato cha wastani cha Mchina mwaka 2009 kilishika nafasi ya 109 duniano. Hii inaashiria kuwa hatutakiwi kujisifu kuusu “Hatua Kuu Mbele” ya mapato ya fedha. Na kinyume chake, inatupasa tutafakari juu ya hali ilivyo sasa.

Mwanablogu, 1741596507, anafafanua zaidi juu ya hisia za dhiki kati ya watu wa kawaida:

我国政府财政巨大的收入与老百姓的低工资收入、低福利待遇、低社会保障、低医疗卫生条件、低教育投入,以及老百姓超高生活消费、天高的房价消费、极高的税收负担等等形成了巨大的反差。

Kuna tofauti kubwa kati ya mapato ya taifa na maisha ya watu: vipato vya chini, ukosefu wa kinga za kijamii na mafao, ukosefu wa huduma za afya na kupungua kwa ruzuku ya elimu. Katika upande mwingine wa sarafu, bei za nyumba na bidhaa za walaji zinazidi kuongezeka na watu wanatakiwa kulipa viwango vikubwa vya ushuru.

Nchi imara, watu masikini

Bai Yen anahitimisha kuwa China ni nchi imara, lakini watu wake wanaendelea kuwa masikini:

整个国家,富的越来越富,穷的越来越穷。官员们越来越富,老百姓越来越穷。

Katika nchi hii, nmatajiri wanakuwa matajiri zaidi wakati masikini wanakuwa masikini zaidi. Wafanyakazi wa serikali ndio matajiri zaidi wakati watu wa kawaida ni masikini zaidi.

国家财政收入增加了,又可以多办几届超豪华的奥运会世博会,又可以长长我国政府的脸面了。

Na hivi sasa wakati mabapo mapato ya fedha ya taifa yameongezeka, tunaweza kuwa na mashindano makubwa zaidi ya Olimpiki pamoja na maonyesho ya dunia ili kuiangaza sura ya serikali.

如果我国国民收入分配不公的格局不改变,那么国家财政收入增加再多,对咱们普通老百姓来说也毫无意义。

Ikiwa muundo wa mgawanyo wa mapato haubadiliki, hata nchi iwe tajiri namna gani, haina maana yoyote kwa watu wa kawaida.

Serikali za miji zina madeni

swlonging anaonyesha kuwa serikali za miji nazo pia ni masikini:

地方政府基本上也归属于我们这些穷民一类了,欠下一屁股债,日子实在 不好过。要知道,1994年分税制度的改革,虽然客观上加强了中央政府的财力,但是却削弱了地方政府的财力… 另一方面,地方政府还要承担大量的公共事务支出,没有多余的财力实现城市发展和基础设施建设,政府要实现这一部分功能,贷款是非常重要的一部分。在2008年底经济刺激政策下,地方融资平台设立和贷款受到鼓励,政府甚至发文要求下级县按要求设立融资平台。各地政府做出了一致的选择——贷款开展项目建设。

Serikali za miji zinafanana na watu masikini na nyingi zina madeni. Marekebisho ya ushuru ya mwaka 1994 yameongeza mapato ya fedha ya serikali kuu lakini yamedhoofisha nguvu za kifedha za serikali za miji… kwa upande mwingine, serikali za miji zinabeba wafanyakazi wa serikali na hazina mapato ya ziada ya kujenga miundo mbinu. Na matokeo yake, ianzibidi zikope fedha. Sera ya uchumi mwishoni mwa 2008 ilizihamasisha serikali za miji kutengeneza jukwaa la kifedha ili kupata mikopo. Hata serikali za mitaa zilijiunga na mipango hiyo ya fedha ili kupata mikopo ya miradi ya maendeleo.

6月23日,审计署公 布的报告显示,地方债务总体规模较大,存在风险,一些债务风险较为集中的地区债务余额超过本级财政可用财力的100%…

Tarehe 23 Juni, Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Taifa ilitangaza kuwa deni la ndani limeongeza hatari katika jamii. Katika maeneo kadhaa, deni la ndani ni 100% zaidi ya uwezo wa serikali…

Yeh Kai ana maoni kadhaa mazuri ya kuboresha hali:

1、  适度降低政府财政收入在GDP中的比重,还富于民。…
2、  建立更透明的财政收支监督管理体系。加大财政信息公开的力度,大力提高财政收支透明度。…
3、  优化财政支出、压缩行政办公费用、加大民生投入。民间对财政收支疑问颇多,其实关键还在财政收入的使用去向。如果财政收入的大头都切实的投向民生,民众是 欢迎的。但是,我们的财政收入中的相当部分却作为各级政府的行政办公费用,具体多少无从查考,但从庞大的公务员和事业编制、豪华的行政办公楼、以及各级官 员乘坐的车子来看,民众的疑问是有道理的。从另一方面,在社会保障、医疗、教育等方面的投入仍然不足,突出的表现是看病难、上学难、退休养老难。…中央政府有必要出台统 一性措施,硬性规定社会保障、医疗、教育在政府财政收入中的占比,并逐年提高,只有暂时采用强制性措施,才能切实加大民生投入,压缩行政办公费用,增进社 会的和谐稳定与健康发展。

1. Punguza uwiano wa mapato ya fedha kwa pato la taifa (GDP), na weka utajiri katika watu…
2. Jenga mfumo wazi wa ufuatiliaji wa fedha za taifa. Taarifa kuhusu bajeti ya taifa na matumizi ziwe wazi na ziweze kuwafikia wananchi…
3. Punguza gharama za utawala na tumia zaidi kwenye kuboresha maisha ya watu. Watu wana mashaka na mapato na matumizi ya taifa. Lakini watu watakubali matumizi ambayo yanaboresha maisha yao, lakini hivi sasa, sehemu kubwa ya mapato inatumika kwenye gharama za utawala za serikali za miji. Tunaweza kuliona hilo katika upanuzi wa muundo wa wafanyakazi wa serikali, majumba ya kifahari ya serikali na magari. Kwa upande mwingine, uwekezaji wa serikali kwenye kinga za kijamii, afya na elimu hauridhishi. Watu hawana pesa za kwenda hospitali, shule na kufaidi maisha baada ya kuritaya… Serikali kuu inapaswa kuanzisha sera ambayo itarekebisha fungu la matumizi ya umma ndani ya pato la taifa na kuongeza fungu hilo kidogo kidogo ili kujenga jamii shwari na yenye afya.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.