China: Kashfa ya Wizi wa Kitaaluma Uliofanywa na Wang Hui, Mtazamo wa Kimataifa

Kuna kashfa ya wizi wa kitaaluma iliyoibuka mwezi Machi katika duru za kitaaluma za Kichina pale Profesa wa Fasihi wa Chuo Kikuu cha Nanjing, Wang Binbin, alipotuhumu kwamba kazi ya uzamizi ya Wang Hui kuhusu Lu Xun – Kugomea Kukata Tamaa – ina aya kadhaa ambavyo vimenukuliwa moja kwa moja kutoka katika vitabu vingine pasipo kukiri kunukuu huko. (Taarifa zaidi za historia ya jambo hilo zinapatikana Granite Studio na ChinaGeeks)

Wang Hui anaheshimika kama msemaji mkuu wa “Mrengo Mpya wa Kushoto” wa duru za wasomi wa Kichina na pamoja na kuwa na kashfa hiyo, mwezi Mei alipendekezwa na Chuo Kikuu cha Tsinghua na hatimaye alifaulu kupata tuzo ya udhamini kutoka kwenye mamlaka ya juu kabisa ya serikali, Baraza la Dola.

Wakati ambapo Wang Hui mwenyewe aliamua kubaki kimya akitarajia kwamba suala hilo “lingefafanuliwa na kumalizwa ndani ya jamii ya wanataaluma”, wasomi wengi walio vyuoni na wasomi wengine walio uraiani wametoa maoni yao kuhusu jambo hilo kupitia vyombo vya habari vya ndani. Wapo waliomtetea Wangu Hui; wapo waliosema kwamba kitendawili hicho kinatokana na kutokutaja vitabu vya rejea kwa kufuata utaratibu wa kawaida zaidi kuliko kufanya wizi wa kitaaluma kwa makusudi; wapo ambao wamependekeza ufanyike uchunguzi wa kina ukiongozwa na kamati huru ya wanataaluma. Mdahalo huo mzima umefanywa zaidi miongoni mwa wasomi wa ndani ya nchi na kwenye mtandao wa intaneti mpaka hivi karibuni kabisa (Julai 7) pale chombo cha habari kimoja cha nchini humo (ifeng.com) kilipochapisha barua iliyotiwa saini kwa pamoja na “jumuiya ya kimataifa ya wasomi, wafasiri, wahariri, wanahistoria na wakosoaji wa utamaduni” wakimwunga mkono kwa juhudi zote Wang Hui.

Uungwaji mkono kutoka katika jumuiya ya wanazuoni wa kimataifa

Barua hiyo ya wazi, iliyotiwa saini na wanazuoni wenye majina mkubwa wa kimagharibi kama vile Tani Barlow, Arif Dirlik, Gayatri C. Spivak na Frederic Jameson,imezichukulia shutuma hizo za wizi wa kitaaluma kama “mashambulizi kutoka katika vyombo vya habari vya Uchina vinavyojitafutia umaarufu” na inatetea umadhubuti wa kitaaluma wa Wang Hui:

Shutuma hizo zimepata pingamizi na hata kuonekana kuwa hazina maana kufuatia uchambuzi yakinifu uliofanywa na Zhong Biao, Shu Wei, Wei Xing na wengineo. Miongoni mwa waliotia sahihi zao kwenye barua hii ni pamoja na wafasiri, ambao bila shaka wapo karibu sana na kazi za Wang Hui. Kila mfasiri amekagua tena na tena rejea zote katika machapisho makubwa yote ya wasifu za watu miongoni mwa zile alizoandika Profesa Wang Hui katika miaka thelathini iliyopita. Hakuna mfasiri aliyeona hata dalili kidogo ya wizi wa kitaaluma hata kwa kujaribu kuchukua maana ya mbali kabisa ya neno hilo.

Jambo la pili, miongoni mwetu wapo wataalamu wa masuala ya Asia katika Masomo Juu ya Uchina na tunathibitisha kwamba umadhubuti wa kitaaluma wa Profesa Wang unasimama kidete na vivyo hivyo umuhimu wake katika masomo ya kimataifa kuhusu Asia.  

Jambo la kushangaza zaidi, ushuhuda wa Zhong Biao na Wei Xing, kama ulivyonukuliwa kwenye barua hiyo, uliandaliwa maalumu kwa ajili ya mdahalo huu lakini umenukuliwa kama kwamba watu hao wawili ni wasomi wanaofahamika vema sana na umma. Zaidi ya hilo, “uchunguzi wao huo yakinifu” bado haujamsafisha Wang Hui kuhusu makosa yake hayo ya kiufundi. Katika makala ya Zhong Biao, anaelezea historia ya kitabu cha Wangu Hui na anakosoa shutuma zisizo na maana alizotoa Wang Binbin:

《反抗绝望》的编辑出版正好处于1988-1991年这一段众所周知的特殊时期,当时具体的学术规范状况与今天有很大的不同。汪晖在该书重印时的对“主要参考书目”的“注”中说:“本书初版时,应出版社要求,删去了全部参考书目。现在这份书目是重新编定的。”

Uchapishaji wa “Resistance to Despair” ulifanyika kati ya 1988 – 1991. Sote tunajua jinsi kipindi hicho kilivyokuwa nyeti. Viwango vya kitaaluma wakati ule vilikuwa tofauti sana. Katika toleo jipya, Wang Hui katika moja ya rejea zake analeza kuhusu toleo lile la kwanza “Katika toleo la kwanza, mchapishaji alitaka rejea zote zilizokuwemo zifutwe. Hii ni orodha mpya iliyohaririwa ya rejea.”

脱注是作者的疏失,日后修订《反抗绝望》时可以补充完善。但从上下文的引证来看,作者并无掩盖与前述几本著作的关系的意思,因为在这些段落的前后,作者都 曾引及这些书。而且这里的引述主要都是历史背景性的或理论背景性的叙述,是参照性质的,并不涉及作者的中心观点。疏失和剽窃,是完全不同性质的问题。

Rejea za chini ya ukurasa zinazokosekana ni kosa la mwandishi na anaweza kurekebisha jambo hilo katika toleo linalofuatia. Hata hivyo, kwa kusoma katika matini na rejea za chini ya ukurasa, mwandishi hajaribu kuficha ukweli kwamba vifungu vya maneno vina uhusiano wa karibu na vitabu vichache alvyonukuu katika kurasa zilizotangulia. Zaidi ya hilo, kile ambacho kimenukuliwa ni zaidi cha kihistoria na kinadharia kuliko kuwa hoja kuu ya msingi ya mwandishi. Makosa yasiyofikiriwa na masuala ya wizi wa kitaaluma ni masuala mawili yenye tofauti za kiasili.

Mashambulizi kupitia vyombo vya habari?

Wei Xing ndiye wa kwanza kulieleza jambo hilo kama mashambulizi kupitia vyombo vya habari na mtazamo wake huo ni bayana kwamba umechukuliwa na jamii ya kimataifa ya wanazuoni katika barua yao ya pamoja:

从王文来看,汪晖所谓”抄袭”的地方其实”并不很多”,而且”较难定性”。这其实已经承认,3月25日《南方周末》破例刊登王文,其实是一种媒体预先设定”有罪”推论而进行的非法的”缺席”审判,因为其论证本身是完全站不住脚的。

Ni wazi kwamba katika makala ya Wang Binbin, kuna vifungu vya habari “vichache sana” “vilivyonukuliwa” na ni “vigumu kuzungumzia kuhusu vyanzo vyake”. Hata hivyo, gazeti la Southern Weekend liliamua kuchapisha makala kinyume na utaratibu wake wa kawaida mnamo Machi 25. Aina hiyo ya uandishi wa habari ni “hukumu bila kuwepo” isiyo halali hasa pasipo kuwa na ushahidi wa kutosha lakini umejengwa kwenye kukisiakisia kuwepo kwa “hatia ya kudhaniwa”.

Kwa kunukuu kutoka katika midahalo mbalimbali katika majukwaa ya mitandaonikama ule wa Douban Duping (讀品) na zhongguosixiang.com, Wei Xing anaamini kwamba migogoro ya vyombo vya habari na intaneti imeharibu uadilifu wa kitaaluma:

面对平面媒体与网络媒体合谋推动的猖狂暴力,学术其实已经斯文扫地。难道中国的学术界就只能这样陷入其中而不能自拔吗?学术界究竟如何来保卫自己的独立与自由?这已经是一个摆在学术界面前的严峻问题。

Njama kati ya vyombo vya habari vya magazeti na vile vya mtandaoni vimechochea vurugu zisizozuilika na kuishia kuharibu kabisa umadhubuti wa ulimwengu wa taaluma. Je, turuhusu ulimwengu wa taaluma wa Kichina kuzama katika vurugu za namna hiyo? Je, tunawezaje kulinda uhuru wetu wa kitaaluma? Hili si jambo la kupuuzwa.

Uchunguzi ulio wazi na unaoendana na uwajibikaji

Wanazuoni na wasomi wengi watachukulia nukuu hiyo hapo juu kama kichekesho – hasa kwa kuzingatia kwamba Ulimwengu wa Taaluma wa Kichina haukuwahi kufurahia uhuru wa kitaaluma tangu mwaka 1949 na upande wa siasa za kiliberali unaamini kwamba njia pekee ya kuona unapatikana uhuru wa kitaaluma ni kuhakikisha kunakuwa na uwajibikaji kwa umma. Kwa maana hii, barua hiyo iliyotiwa saini na na maprofesa wa vyuo vikuu na wasomi wa uraiani zaidi ya 60 ikiitisha uchunguzi wa haraka ukiongozwa na Chuo Kikuu cha Tsinghua na kile cha Akademi ya China kuhusu Elimu ya Jamii juu ya shutuma za wizi wa kitaaluma zinazomkabili Wang Hui pengine ndiyo njia yenye ufanisi zaidi ya kupigania uhuru wa kitaaluma:

事件發生距今已3個月,其間不斷有學者呼籲中國社會科學院和清華大學組織調查委員會,但是至今未見回應。汪暉對上述批評迄今也沒有任何回應,但他曾表態, 希望能由學術界內部來解決。為對汪暉教授負責,澄清這一爭議,結束莫衷一是的狀態,走向良性循環,我們支持熊、林二位的建議,聯名要求中國社科院和清華大 學迅速答複,履行職責。我們也同意易中天的主張,在組成調查委員會時,應邀請貴院、貴校之外的學者,乃至海外學者參加,公示委員會名單和調查結果。我們同 時要求,調查結論以及各委員投票意向最終能公布,以示公開、公正,接受公眾監督。

Mdahalo huo umekuwa ukiendelea kwa miezi mitatu sasa, wanazuoni wengi wameihimiza Akademi ya China ya Elimu ya Jamii na Chuo Kikuu cha Tsinghua kuunda kamati ya uchunguzi. Mpaka sasa hakuna jibu kutoka kwenye taasisi hizo mbili. Wang Hui ameendelea kubaki kimya kuhusu shutuma hizo lakini alipata kutamka kwamba angetamani jambo hilo limalizwe ndani ya jumuiya ya wasomi. Ili kufafanua mkanganyiko na utata, tunaunga mkono pendekezo lililotolewa na Xiong Bingji na Lin Yusheng katika barua hii fupi na tuna matarajio kwamba taasisi hizi mbili zitatoa jibu zuri katika kutekeleza wajibu huo. Tunakubaliana pia na Yi Chongtin kwamba kamati hiyo iundwe na wasomi wa kutoka ng'ambo na haina budi kuchapisha matokeo ya uchunguzi na hata kuhakikisha kwamba mchakato mzima, ikiwa ni pamoja na maoni na mitazamo ya wanakamati mmoja mmoja, inakuwa wazi kwa umma mzima.

Upande wa siasa za kiliberali wa nchini China dhidi ya mrengo mpya wa kushoto wa kimataifa

Barua hizo mbili sasa zinatazamwa kama kukabiliana kwa koo mbili za wasomi: upande wa siasa za kiliberali nchini China dhidi ya mrengo mpya wa kushoto wa kimataifa. Wakati kundi hilo la kwanza linataka ufanyike uchunguzi ulio wazi na uwajibikaji kwa umma, kundi hilo la pili linachukulia kwamba mdahalo huo ni mashambulizi ya vyombo vya habari na ukosoaji wa wazi kama vurugu zinazoelekezwa dhidi ya uhuru wa kitaaluma.

Wu Lian, ambaye ni mkosoaji wa fasihi, amekasirishwa sana na barua hiyo ya pamoja ya kimataifa:

你们居然说“媒体无端地攻击一个学者”,无端,那就是诽谤!你们应该在中国将媒体告到中国法庭!而不是通过写信,给一个面目模糊的大学当局施压!你们搞错了,大学校长不是法官!

Mnasema kwamba “Vyombo vya habari vimemshambulia mwanazuoni pasipo kuwa na sababu yoyote”, kama hivyo ndivyo, basi ni kumchafulia jina! Mlipaswa kuburuza vyombo hivyo vya habari katika mahakama za nchini China, wala hamkutakiwa kuandika barua hii ili kushinikiza mamlaka ya chuo kikuu. Mmekosea, mkuu wa chuo si jaji katika suala hili!

你们声称要“声援”汪晖教授?你们又搞错了吧!难道这是一次政治迫害?我们怎么从来没有看到你们在另一些远为严重的事件之后,对那些被迫害者的声援?你们是否觉得,你们的所谓学术声誉,居然比另一些价值更为重要,更需要加以急迫的保护?

Mlisema kwamba hamna budi “kumwunga mkono Profesa Wang”. Hapa tena mmekosea! Je, huu ni ukandamizaji wa kisiasa? Imekuwaje kwamba hatujawahi kamwe kusikia mkitoa uungaji mkono pale wapinzani wa kisiasa wanapokandamizwa katika matukio makubwa ya kisiasa? Je, mnafikiri kwamba sifa ya kisomi ni bora zaidi kuliko masuala mengine na kwa hiyo inastahili uungwaji wenu mkono kuliko vitu vingine?

你们任意裁剪光天白日之下的事实,关注此事的每一个汉语阅读者,都知道王彬彬教授指控汪晖教授《反抗绝望》一书涉嫌抄袭的那篇文章,首先发表在中国学术期刊《文艺研究》,此后才由《南方周末》刊登!你们显然故意忽略了这一事实,就如你们常说的那样,“历史是被建构出来的”,你们现在直接“建构”事实了!

在这一“建构”之下,学术刊物《文艺研究》从人间蒸发了,不见了,消失了,不存在了!

这是对一本重要的中国学术刊物的公然藐视!

Mlichofanya ni kama kurudufu na kubandika ukweli mchana kweupe. Kila Mchina anayefuatilia jambo hili anafahamu kwamba makala iliyoandikwa na Wang Binbin inayotuhumu Resistance to Despair ya Profesa Wang kwanza ilichapishwa katika “Literature and Arts Studies” yaani “Masomo ya Fasihi na Sanaa” na baadaye ikachapishwa tena na gazetila Southern Weekend. Mmefumbia macho ukweli huu na kama ambavyo daima mmesema, “historia hutengenezwa”, sasa mmeshiriki moja kwa moja kaika “kutengeneza” ukweli!

Katika “utengenezaji” huo, jarida la kitaaluma la hapa nchini, Literature and Arts Studies, limegeuka mvuke, limeyeyuka na kutoweka!

Hili ni tusi kubwa kwa jarida hili muhimu la kitaaluma la China!

你们给清华大学当局写这封言辞灼灼的公开信,到底所意何为?证明汪晖教授的清白?可是调查尚未开始!证明汪晖教授学术成果斐然享誉你们所建构的“世界”?可是王彬彬教授并没有谈论这个问题!证明“媒体”只是一场“狂乱”,希望学校当局不要加以理会?可是已有众多的学院学者介入了此事,媒体履行了它的职能,因为公众具有知情权!莫非你们认为学者只要在媒体发表文章或发表言论,他们就成了媒体的一部分?

Je, lengo hasa la barua hii ya wazi yenye hoja nyingi zinazojizungushazungusha iliyotumwa kwenye mamlaka ya Tsinghua? Je, ni kuthibitisha kwamba Profesa Wang Hui hana hatia? Lakini hakuna uchunguzi uliokwishafanyika mpaka sasa! Kuthibitisha kwamba Profesa Wang Hui anaheshimiwa katika “ulimwengu” wenu mlioutengeneza? Lakini makala ya Wang Binbin haikujishughulisha n a suala hilo! Je, ni kuthibitisha kwamba “chombo cha habari” ni “kichaa” na kwamba chuo kikuu hakina sababu ya kujibu jambo hilo? Hata hivyo, wanazuoni wengi wamejadilia kuhusu jambo hilo na ni wajibu wa vyombo vya habari kuripoti kuhusu jambo hilo. Umma una haki ya kupashwa habari ya jambo hilo! Au mnafikiri kwamba kila wanazuoni wanapozungumza au kuchapisha kupitia vyombo vya habari mbalimbali, basi majadiliano yao yatageuzwa kuwa habari zinazogaa kwenye vyombo vya habari?

Maoni ya papo kwa papo

Yaelekea mwingilio huu wa kimataifa kwenye kashfa hii kwa vyovyote kutaongeza mafuta kwenye maji ambayo tayari yanachemka nchini China. Hapa chini tayari kuna majibu kupitia kwenye Twita:

mozhixu
  

汪晖不是成天反全球资本主义的扩张吗, 怎么一到自己跟前,就抱上全球文化霸权的大腿了, 真恶心人啊

Je, hivi huyu Wang Hui, si anapinga utandawazi na ubepari wa kiulimwengu? Inakuwaje sasa anataka kukumbatia utegemeano wa kiutamaduni wa kidunia pale linapokuja suala la maslahi yake binafsi, jambo hili linatia kinyaa!

WuyouLan
  

汪暉在國內和西方都自居左派。在國內,和共產黨抱團,叫左派。在西方,反體制,叫左派。

Wang Hui ni wa mrengo wa kushoto nchini China na magharibi. Katika China upande wa bara, mrengo wa kushoto umekumbatia CCP; kule magharibi, mrengo wa kushoto huhoji mfumo uliopo.

lingcangzhou
  

80位学者支持剽窃的公开信观点和老头劈叉——扯蛋一样。公开信三点均属扯淡,第一点未解释举报者提出的抄袭段落;第二点证明剽客诚信谁信证明者?第三点攻击传媒,把汪晖替换为“大学”!此公开信无耻啊!

Maoni ya wanazuoni 80 kwenye barua ya pamoja wakiunga mkono wizi wa kitaaluma ni ya kishenzi. Kwanza, barua hiyo haikuzungumzia aya zilizozua mjadala kama alivyozitaja Wang Binbin na wengine; Pili, je, nani atakayewaamini wale ambabo wanajaribu kuthibitisha uadilifu wa mwizi wa kazi za kitaaluma? Tatu, kwa kuvishambulia vyombo vya habari, barua hiyo inahamisha fikra kutoka kwenye suala la “tatizo la wizi wa kitaaluma wa Wang Hui” kwenda kwenye “uhalali wa chuo kikuu”. Barua hii ya wazi haina hata chembe ya aibu!

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.