· Oktoba, 2013

Habari kuhusu Asia Mashariki kutoka Oktoba, 2013

Vyuo Vikuu Vingi Mno Nchini Singapore?

  11 Oktoba 2013

Limpeh anabaini ongezeko kubwa la taasisi za eleimu ya juu nchini Singapore. Je, hizo ni habari njema au mbaya kwa nchi ya Singapore? …kupanuka huku [kwa elimu ya juu] kumekuwa na matokeo mabaya kwa soko? Kwa hiyo wakati kupanuka huku kunaweza kuwa kumeongeza ajira kwa baadhi ya baadhi ya watu...

Wali Unaonata Haufai kwa Watoto, Akina Mama Waambiwa

  7 Oktoba 2013

@LaotianMama anawakumbusha akina mama wa Lao kutokuwalisha watoto wenye njaa wali unaonata ambao ni chakula cha asili kwao. Wali unaonata kwa watoto wachanga ni sawa na punje za wali katika utamaduni wa ki-Magharibi. Wazo ni lile lile kuwa kuwapa watoto wachanga chakula kigumu kutawashibisha. Kwa hiyo, kuwaanzishia watoto wachanga chakula...

Masuala Matano ambayo Raia wa Brunei Wanahitaji Kuyajadili

  7 Oktoba 2013

Teah Abdullah anaorodhesha masuala matano ambayo raia wa Brunei citizens wanahitaji kuyajadili: Kuimarisha lugha halisi, ngono baina ya ndugu wa damu, maisha ya anasa, ulaji unaozidi kiwango wa “baga” [aina ya mandazi yenye nyama], utegemezi uliopitiliza kwa serikali. Anafafanua kwenye suala la mwisho: …serikali ni sehemu muhimu katika maisha yetu...

Korea Kusini: Mwandishi Msafiri, Utamaduni Tofauti, na Jamii ya Wageni

  4 Oktoba 2013

John Bocskay, mwanablogu asiyeandika mara nyingi sana alifanya mahojiano na mwandishi wa utalii Rolf Potts aliyetumia miaka kadhaa kwenye jiji la pili kwa ukubwa nchini Korea Kusini, Pusan, anasema: Kila mtu niliyeonana naye katika vilabu vya wageni alidai kuwa mwandishi au msanii, lakini hungeweza kuona maandishi mengi au sanaa. Ilikuwa...

China: Miitikio ya Raia wa Mtandaoni Kufuatia Muswada wa Sheria ya Kurithi Kodi

  4 Oktoba 2013

Watumiaji wa mtandao nchini China walionyesha kutokuridhishwa kwao na muswada wa sheria unaopendekeza uwezekano wa kurithiwa kodi zinazoanzia yuan RMB 800,000 [yuan ni sarafu ya nchi hiyo]. Badala ya kuziba pengo la kipato miongoni mwa wananchi, watumiaji wa mtandao wanaamini kuwa sheria mpya inakusudia kuiba fedha kutoka kada ya wafanyakzi....