Habari kuhusu Asia Mashariki kutoka Novemba, 2009
Afya Duniani: Siku ya Vyoo Duniani Yatoa Harufu
Ingawa inaweza kusikika kama masihara, Siku ya Vyoo Duniani inatilia maanani kwenye suala ambalo si la mzaha linalowakwaza karibu nusu ya watu wote duniani – ukosefu wa vyoo na mfumo wa usafi.
China: Obama ni Mshabiki Mkubwa wa Kutokuchuja Habari
Adam Minter amesikitishwa na maoni ya Obama kwenye Mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa Jiji la Shanghai, hasa, maelezo yake kuwa “Mimi ni muunga mkono mkubwa wa kutokuchuja habari“.
Philippines: Mti wa Dita Waokoa Maisha ya Watu 36 Wakati wa Mafuriko
Mti wa aina ya Dita huko Manila mjini uligeuka kuwa "Mti wa Uzima" wakati ulipotumika kama kimbilio na wakazi ambao walitegwa kwenye nyumba zao wakati wa janga la kimbunga na mafuriko ya hivi karibuni. Somo: Usikate miti.
Tamasha la Blogu Indonesia
Tulitembelea tamasha la blogu la Indonesia au PestaBlogger 2009. Hii nim ara ya tatu kwa tukio hili la mwaka kufanyika. Tukio hili lilishuhudia wanablogu kutoka kila sehemu ya Kisiwa hiki ambacho pia ni Taifa wakimiminika mjini Jakarta ili kusherehekea, kujadili na kujumuika.
Misri: Mwanablogu wa Kiume Aagizia Bikra ya Bandia
Mengi yalisemwa na kuandikwa juu ya zana ya kutengeneza bikra ya bandia - mpaka mwanablogu Mmisri wa kiume Mohamed Al Rahhal akanunua moja. Marwa Rakha anatuletea habari hiyo.
Vietnam: Matangazo Mengi Katika Uwanja wa Ndege
Charvey amebaini matangazo mengi kuliko kawaida katika uwanja wa ndege wa Vietnam.
Ujauzito na Magereza: Afya na Haki za Wanawake Magerezani
Mapambano bado yanaendelea kuhakikisha haki za binadamu kwa wanawake wajawazito duniani pote, ni inaelekea kwamba katika mchakato huo, wanawake waliopo magerezani wanasahauliwa. Je ni hatua zipi zilizochukuliwa kuhakikisha kuwa nao wanaangaliwa kwa utu, kwa kuzingatia uhai wanaoubeba.
Japan: Mkeo anapougua
Pale utamaduni wa “mifugo ya mashirika” au kwa maneno mengine “utamaduni wa ujumla wa wafanyakazi” (社蓄 shachiku) na maadili ya ndoa vinapogongana – zaidi ya watu 300 walitoa majibu kuhusiana...