Japan: Mkeo anapougua

Pale utamaduni wa “mifugo ya mashirika” au kwa maneno mengine “utamaduni wa ujumla wa wafanyakazi” (社蓄 shachiku) na maadili ya ndoa vinapogongana – zaidi ya watu 300 walitoa majibu kuhusiana na swali lililoulizwa kwenye jukwaa kubwa la mijadala lijulikanalo kama Hatsugen Komachi: Je, mwanaume aombe ruhusa kazini pale mkewe anapougua?

Hali ilivyokuwa

Rina amekuwa akiishi kwenye ndoa kwa miaka 8 sasa na binti yake anasoma darasa la tatu. Anataka kutalikiana na anarejea tukio moja katika ndoa yake ambalo limebaki katika akili yake tangu wakati huo.

Wakati binti yao alipokuwa akingali mchanga, Rina alinyong'onyea sana kwa sababu ya kukosa usingizi kutokana na kulia sana kwa binti yao nyakati za usiku. Alipatwa na homa kali kiasi cha kushindwa kumhudumia binti yao mchanga, lakini mumewe alikataa katakata kuchukua likizo yenye malipo na alikataa pia kurejea nyumbani mapema kuliko ilivyo kawaida. Rina alihuzunika sana kwamba hata simu mumewe alikuwa hapigi. Ilimchukua takribani miezi miwili kwa hali yake kutengemaa tena na anashindwa kabisa kusahau jinsi mumewe alivyoshindwa kumsaidia katika kipindi hicho.

Swali

ここういう状態の場合、会社を休めないまでもせめて定時で帰ってきてほしいというのはわがままでしょうか。
みなさんのご家庭はどうですか?妻が病気の時、夫は会社を休んで子供の世話をしてくれますか?また、会社で「妻が病気だから」と言って休んでいる人をどう思いますか?

Katika hali ya namna hii, je, nitakuwa mbinafsi kwa kutaka mume wangu walau arejee nyumbani mapema pasipo kufanya kazi saa za ziada, kama si kuomba ruhusa siku nzima?
Je, hali ikoje katika familia zenu? Je, mume wako huomba ruhusa kazini siku nzima ili kuwatunza watoto pale mke anapougua? Je, kuna watu kwenye kampuni yenu ambao huomba ruhusa kutokuwepo kazini kwa sababu mke wake anaumwa?

Majibu

Mara moja, wanawake wengi wazazi wa muda mrefu walituma simulizi zao kuhusu nyakati kadhaa ambapo walikuwa wagonjwa lakini walijikokota kutoka kitandani ili kujitunza na kuwatunza watoto wao pasipo msaada wa waume zao – si kwa sababu walitarajia au walitaka msaada kutoka kwao.

‘Aliyeolewa na mwenye watoto wawili’ alisema:

インフルエンザで寝込んでいるときも、40度の熱が三日間下がらない時も、一週間38度から熱が下がらずいた時も夫に休ん で欲しいと思ったことはありませんでした。夫の職種が営業だったので客先と約束があれば休めないのも仕方がないし、客先と急に約束が入ったら帰れないのも 仕方がないので。会社に勤めてお給料を頂いている以上会社に損害を与えるような休暇をとれないのは当たり前。
トピ主様のご主人の業種がわかりませんが当人の体調不良と家族の体調不良はまた別でしょう。夫の風邪を理由に仕事を休む妻というのもありえないと思いますがどう思いますか?

Hata wakati nilipokuwa hoi kitandani kwa sababu ya mafua, au nilipokuwa na homa kali ya nyuzi joto 40 kwa siku tatu mfululizo, au nyuzi joto 38 kwa wiki nzima, haikuwahi kupita akilini mwangu kuhitaji mume wangu akae nyumbani. Yeye ni bwana mauzo kwa hiyo hana budi kukutana na wateja wake na nyakati za usiku hakuwezi kuwepo na msaada kama kuna dharura.
Ni wazi kwangu kwamba kama mtu anapokea mshahara, hawezi kupumzika baadhi ya siku, kwani jambo hilo litakuwa na athari mbaya kwa kampuni. Sina hakika mumeo anafanya kazi gani, lakini kuugua kwake na kuugua kwa mwanafamilia mwingine ni vitu viwili tofauti. Nashindwa kuamini kwamba kuna mwanamke anayetaka mumewe akae nyumbani siku yeye (mke) akiugua. Unawaza nini hapo?

Miri anasema, huna budi kuzingatia sifa ya mumeo.

旦那さんのお仕事の形態にもよると思いますが、急なお休みは周りにとても迷惑をかける事となります。それに自分(妻)の管理が出来ていない事で夫の会社に迷惑をかけるなぞ夫の評価を下げる事と思って居ます。
妻が病気(入院する様な病気以外)夫が会社休むは普通とは思えません。ヘルパーさん頼むとか考えます。

Kwanza inategemea kazi aliyonayo mumeo, lakini kuomba ruhusa za ghafla kazini kwa kawaida husababisha usumbufu mkubwa kwa wafanyakazi wenzake na kwa wateja. Kukosa kwako nidhamu ya kuchunga afya yako kunampunguzia sifa mumeo kazini kwa kusababisha usumbufu kwenye kampuni. Sidhani kama ni jambo la kawaida kwa mume kutofika kazini kwa sababu mkewe anaumwa, labda kama inampasa kulazwa hospitalini. Mimi ningewaza kumwajiri nesi au mhudumu.

Teardrop naye anakumbuka jambo kama hilo. Mumewe alikwenda zake kunywa na marafiki zake akimwacha yeye anaumwa, jambo lililosababisha ugomvi mkubwa.

でももっとびっくりしたのはこの話をした時の女性達の反応!「そんなことで・・・。」という反応なんですよね。ウチなんてもっとひどいわよ~って。
妻たちはみんなこういう仕打ちに慣れてしまって、感覚がマヒしてしまっているんだなぁって、悲しく思ったことを覚えています。
でもあれから数年・・・完全に私もマヒしてます。

Kilichonishangaza zaidi (kuliko ukweli kwamba alikwenda zake kunywa) ilikuwa ni vitendo vya mashoga zangu! Waliniambia, “Je, umekasirika kwa sababu hiyo tu? Mimi nina tatizo kubwa zaidi!” Nakumbuka kuwaza jinsi gani ilivyo huzuni kwamba wake wanalazimika kuzoea unyanyasiaji huu kiasi cha kuwafanya wasiwe na hisia tena. Ni miaka michache imepita…. Na hisia zangu zimekufa kabisa.

Kanon anasema kwamba mumewe huonyesha mapenzi yake kwa njia nyingine.

夫の会社の激務や夫の社内での立場を思えば「体調悪いから帰ってきて!」とは言えません。私の体調の悪い時に夕飯を外で済ませてきてくれる。駅の自販機でポカリを買ってきてくれる。私にはそれだけで十分に優しい夫です。

Ile kuwaza tu kuhusu kazi nyingi zinazomkabili mume wangu na jinsi wanavyomchukulia ofisini kwake, kwa kweli siwezi tu kusema “Tafadhali rudi nyumbani mapema kwa sababu sijisikii vizuri!”. Ninapoumwa, yeye hula chakula chake cha usiku mgahawani. Ananinunulia vinywaji baridi kwenye mashine ya vinywaji mtaani. Kwangu mimi huyu ni mume anayenijali kwa kufanya vitendo hivi.

‘Kengyo-shufu’ (mama wa nyumbani anayefanya kazi) anasema:

ちゃんと仕事をしたことないから言える言葉だと思います。
ご主人だって休みたいんだと思います。でも休めないんですよ。自分が体調悪くて休むのは周りに風邪をうつしてはいけないとかそういったことではないですか?
簡単に休めないという現在の多くの日本の企業が問題だと思いますが休めないのが現実です。

Haya ni maneno ya mtu ambaye hajawahi kufanya kazi kamwe. Nafikiri mumeo anataka kukaa nyumbani, lakini anashindwa.
Ukweli kwamba wafanyakazi wana wakati mgumu kupumzika siku moja moja ni tatizo linaloyakabili makampuni mengi makubwa ya Kijapani, lakini ukweli ni kwamba hawezi kujichukulia mapumziko tu.

Wapo wengine wanaomwonea huruma, kama nabe.

リナさんの言うことは正しいです。全然わがままではありません。
 私はもちろん休んでいます。 […] 妻が病気になっても働く時代は終わってます。
二人で力を合わせて生活守って時代です

Rina, unachokisema ni sahihi. Hiyo wala si ubinafsi! Huwa ninaomba ruhusa ya kumpumzika pale mke wangu anapougua. […] Zama ambapo wanaume huwaacha nyumbani wake zao walio wagonjwa na wao kwenda kazini zimepita. Sasa, hatuna budi kuungana na kulinda uhai wetu.

Pochi anashangazwa na jinsi kila mmoja alivyo mkali, na kwa kukebehi anauliza kama wanafanya kazi kwa saa 15 – 16 kila siku katika mwaka mzima.

家族がせっぱつまった状態のときに、仕事のほうがどうにか都合がつきそうだったら、少々遅刻して病院につれていくとか、コ ンビニで食料を調達するとか、残業はせずに急いで帰ってくるとかするのは社会人失格?頭から「休めるわけない!!」と決めつけるのは、ストイックな姿を会 社の人に見せたいから?自分の楽しみのために有給をとることもあるでしょう。(有給をとって友人とゴルフにいく上司をなんども見てます)

Ikiwa ninampeleka hospitali mwanafamilia yangu na kuchelewa kufika kazini, au ninakwenda dukani kununua vyakula, au ninaharakisha kurejea nyumbani bila kufanya kazi katika saa za ziada pale hali inaporuhusu, je, hii ina maana kwamba mimi si mwanajumuiya kamili? Je, mnatangaza rasmi mapema kuwa “Siwezi kwamwe kupumzika hata siku moja!” kwa sababu tu unataka kujionyesha jinsi ulivyo na bidii kwa wenzako? Watu huchukua likizo zenye malipo kwa ajili ya kujiburudisha, au siyo? (Nimeona mara nyingi mabosi wakichukua likizo zenye malipo ili kwenda kucheza mchezo wa gofu na rafiki zao.)

Tokumei anasema inategemea unaumwa kiasi gani na anaongeza kusema:

結婚生活を快適に過ごすこつは、お互いに相手に期待しないことではないかともうすぐ銀婚式の私は思っています。期待すると裏切られたと思うし、期待しなければ些細な優しさもありがたく感じられます。再婚の際の参考までに

Hivi karibuni nitasherehekea miaka 25 ya ndoa yangu, na ninaweza kukuambia kwamba siri ya kuwa na maisha yasiyo na mivutano mingi katika ndoa ni kutokuwa na matarajio makubwa sana kwa mwenzako. Kama hutarajii, basi akikufanyia hata jambo dogo jema basi litakufurahisha. Huu ni ushauri tu kama utatokea kuolewa tena.

Huu ni ushauri wa Echika:

うちの会社の場合、男性が家庭の事情で会社を休むと、上司はあまりよく言いません。なので、私も自分の体調不良と偽って休暇をとり、妻の看病をしました。

Bosi wangu huwa hawawafikirii vyema wanaume wanaoomba ruhusa kwa sababu ya matatizo ya kifamilia. Ninachofanya ni kuwaambia ofisini kwamba mimi ndiye ninayeumwa, kwa hiyo hukaa nyumbani na kumtunza mke wangu.

‘Usuaji’ anasema kwamba jambo hilo kwamwe haliwezekani katika kampuni anayofanyia kazi.

でも、文句を言い続けて一生夫婦であり続けることよりも、離婚と言う手段を選んだトピ主さんの勇気は素晴らしいと思います。

Pamoja na yote, nakupongeza kwa kuchagua kutalikiana na mumeo, kuliko kuishi naye maisha yote huku ukinung'unika.

Nya anasema kwamba inaweza kuwa ni jambo la kusumbua, lakini wanaume hawawezi kubahatisha kujua wanachokitaka wanawake, mpaka kielezwe bayana.

妻が病気の時、「食事を作るのは難しいだろうから、外食して帰るよ」という夫さん、よくいますよ。高熱で起きられない妻の 食事は??思いつきません。面倒だけど「作れないのでコレコレを買ってきて(何か買ってとまかせると、こってりしたコンビニ弁当とか買ってきてしまう)」

Kuna wanaume wengi ambao husema “Nitakula kabisa chakula cha usiku kabla ya kufika nyumbani kwa sababu najua itakuwa vigumu kwako kupika”. Yaani haiwaingii akilini kwamba mke mwenye homa kali naye anahitaji kula. Japokuwa ina usumbufu lakini huna budi kusema “Siwezi kupika leo, kwa hiyo tafadhali ninunulie hiki na kile”. Kama ukiwaachia, watakwenda kwenye duka ambapo watanunua kifurushi cha chakula chenye mafuta mengi kutoka kwenye duka la walaji au chochote kile.

Hatuna budi kutambua kwamba Hatsugen Komachi ana mwelekeo wa kike ua hata ule wa mwanamke mama wa nyumbani. Nyongeza ya kuvutia katika simulizi hili ni majibu kutoka kwa Hatena,ambaye ana mtazamo wa kiume zaidi, ambaye alitofautiana kabisa (Hakuna kazi duniani iliyo muhimu zaidi ya afya yangu au ya familia yangu. 自分、もしくは家族の健康にも優先する仕事なんてこの世に一つもない。) kama ilivyokuwa kwenye mjadala kuhusu utaalamu katika SNS LinkedIn (ruhusa inatakiwa:Wafanyabiashara wa Kijapani wanatoa kafara familia zao), lakini hiyo ni simulizi kwa ajili ya siku nyingine.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.