PICHA: Maisha Nchini Myanmar

Myanmar college graduates leaving a beauty salon

Wanafunzi wa Chuo wakitoka saluni. Meiktila, 2013

Mpiga picha aliyewahi kushinda tuzo Geoffrey Hiller kwa mara ya kwanza alitembelea nchi ya Myanmar mwaka 1987; na alishangazwa na kile alichokiona katika nchi hiyo:

Baada ya safari ya kuchosha, sikushangazwa na watawa, ila nyuso ya wananchi wa Burma, zilizochorwa kwa rangi nyeupe, mara nyingi zenye tabasamu. Nilitaka kufahamu zaidi hawa walikuwa akina nani, walioteswa na serikali ya kifisadi na vikwazo vya kimataifa.

Alikuwa amerudi Myanmar mara kadhaa na kushuhudia mabadiliko ambayo yametokea katika nchi hiyo katika miaka ya karibuni:

Nilirudi tena mwaka 2013. Kamera yangu ilitaka kuyanasa maisha ya kila siku, kuanzia mitaa iliyojaa watu ya mji wa kikoloni wa Yangon, hadi kwenye masoko yenye vumbi ya Mandalay, hadi Waislamu wa Meikhtila, na hata maisha ya mtoni huko and Pathein.

Sura ya mji wa Yangon ilishabadilika, majengo mengi mapya yakijengwa pamoja na magari mengi yanayoingizwa nchini humu.

Lengo lake lilikuwa kuchapisha kitabu kupitia Kickstarter mradi ambao ungehusisha picha zake kuweka kumbukumbu za maisha ndani ya nchi hiyo kuanzia mwaka 1987 mpaka kufikia mabadiliko ya kihiistoria ya hivi karibuni. Kitabu, Burma katika wakati wa Mpito, kitaonyesha picha za Meiktila mahali ambapo Hiller alitembelea kabla ghasia kuibuka mjini humo:

Baada ya kuwepo kwangu katika mji huu wa amani, taarifa za habari kuhusu mapigano na mauaji na kuchomwa moto nyumba za watu haziingii akili mwangu. Nilikuwa nimezungumza na wakaazi wengi wa mji wa Meiktila, wale wa dini ya Buddha na Waislamu, na sikuwahi kuhisi mapigano ya namna hiyo yangeweza kutokea

Maombi ya kitabu hicho yanaweza kufanytwa kupitia Kickstarter mpaka Oktoba 9.

Dalah, 2011

Dalah, 2011

burmese

Mwanamke akivuta sigara iitwayo cheroot, Mandalay, 1987

A building in Yangon, 2012

Jengo mjini Yangon, 2012

A young man holding a photograph of Opposition leader Aung San Suu Kyi and her father, General Aung San. Yangon Ferry, 2012

Kijana akiwa amebeba picha ya kiongozi wa Upinzani Aung San Suu Kyi na baba yake, Jenerali Aung San. Yangon Ferry, 2012

Women workers in Meiktila, 2012

Wanawake wakifanya kazi mjini Meiktila, 2013

*Picha zote na Geoffrey Hiller

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.