Thailand: Waziri Mkuu wa Zamani Afariki Dunia


Samak Sundaravej — Gavana wa Zamani wa Bangkok, mwendeshaji wa kipindi cha mapishi, na Waziri Mkuu wa 25 wa Thailand amefariki dunia tarehe 24 Novemba.

Samak alikuwa mwanasiasa aliyewachanganya wengi ambaye aliondolewa madarakani kisheria kutoka nafasi ya juu kabisa wakati Mahakama ilipoamua kuwa alivunja sheria ya kuendesha kipindi cha runinga cha mapishi wakati akiwa anashikilia nafasi ya umma.

Bangkok Pundit
anapitia wasifu wake uliochapishwa na magazeti makubwa. Thaizer anamwelezea Samak kama mpishi makini aliyekifanya chakula cha wa-Thai kuwa maarufu:

mpishi makini, shauku ya Samak kwa chakula cha kiThai ilimfanya awe maarufu kwenye masoko ya kuuza vyakula vya vibichi mjini Bangkok na ukali wake, na namna yake ya kuchukulia mambo isiyo na porojo ilimfanya awe mwongoza kipindi maarufu wa kipindi cha mapishi katika luninga za Thailand. Katika namna ya kinyume, kilikuwa ni kipindi ambacho hatimaye kilimng’oa kwenye nafasi yake ya Uwaziri mkuu.

Samak anakumbukwa sana kama mhamasishaji wa mapishi wa kweli

Baada ya ushindi wake kwenye uchaguzi jambo la kwanza alilolifanya lilikuwa ni kuwaalika waandishi wa habari nyumbani kwake kuonja tambi alizozitengeneza nyumbani. Samak ni mhamasishaji wa kweli wa vyakula, na tunadhani atakuwa mchangiaji mkubwa kwa dunia nzima kwa uzoefu wake na kupenda kwake chakula cha Ki-Thai.

Sehemu ndogo ya video ya youtube inaonyesha mazishi ya Samak yaliyohudhuriwa na idadi kubwa ya watu:

Wanatwita wa Bangakok wana maoni kadhaa juu ya habari za kifo cha Samak:

zaz_zy: Pumzika kwa amani Khun Samak ulimwengu wa mapishi utakukosa. Ukweli na usemwe…hiyo ni kweli tupu.
TAN_Network: waunga mkono wa mashati mekundu kuandamana kupinga kuwepo kwa Mbunge wa chama cha Democrat kwenye mazishi ya Samak
Tongteng: @suthichai Ingawa siko kama Khun Samak, ningesema kwamba ninashangazwa kuona maoni hasi mengi mtandaoni leo. Pumzika kwa amani.
praditpi: Samak Sundaravej, waziri mkuu wa 25 wa Thailand, amefariki leo. Pamoja na wema wake, namtakia mapumziko mema ya amani
anirutpichedpan: Kifo cha K Samak kimethibitisha kuwa watu wengi husahau dhana njema ya kusameheana katika ukamilifu wake! Chuki tu hubaki! Sahau kuhusu upatanishi, nasema

wisekwai
: Upumzike pema peponi Samak. Siasa za Thailand zimepoteza sehemu ya rangi yake
ChadapornLin: ni huzuni kwa kifo cha Samak kwamba najaribu kufikiri mambo mema ya kumkumbuka nayo kwa hisani lakini siwezi

Wakati wa mazishi hayo yaliyodhaminiwa na familia ya Kifalme, wapinzani wa serikali wa Mashati ya Mekundu (wengi walikuwa wafuasi wa Samak) nje ya hekalu waliwazomea maafisa wa serikali waliohudhuria desturi hiyo.

Samak alikuwa na wakosoaji wengi. Baada ya kifo chake, baadhi ya wanablogu wamechagua kutoa mabaya yake aliyoyaacha. Harrison George anaitaja historia ya Samak katika kuipinga demokrasia

Samak alianzisha haki ya watawala wote wa kisiasa wa Thailand kutumia nafasi zao za kikazi kuhalalisha mauaji, kuwatia nguvuni wapinzani wao, kuvifungia vyombo vya habari na kumchafua yeyote mwenye ujasiri wa kuwahoji, na bado akaelezewa, kama mrithi wake Mbunge Somchai aliyemwelezea kama “aliyeyatoa maisha yake kwa demokrasia”

Bangkok Dazed anamwelezea Samak kama “mwansiasa anayezusha hisia za msisimko unaoupata wadudu wakikutambaa

Anaweza kuwa alikuwa na rangi lakini alikuwa mhusika anayechefua aliyevaa sifa mbaya za siasa za Thailand. Ninatamani angewachukua wanasiasa wa sasa wengine mamia kadhaa ateremke nao kaburini.

Political Prisoners in Thailand anaandika kwamba Samak ni kiumbe aliyetoweka kwenye siasa:

Samak alikuwa mmoja wa walinzi wa kale wa Thailand ambaye aliweza kukaa jukwaani na kubaki na heshima yake kisiasa kwa sababu sura nyingi za msingi za siasa za Thailand zimebaki zilivyokuwa. Kwa maneno mengine, kwa sababu mazingira ya kisiasa yalibadilika kwa taratibu, kiumbe wa kisiasa wa kale ameweza kuendana nayo na hata kufanikiwa.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.