Wakati Mgogoro wa Kisiasa Ukikolea: Thailand Kufanya Uchaguzi Mwingine Mwezi Julai

Anti-government protesters gather at a rally showing their loyalty to King Bhumibol Adulyadej. Protesters are demanding the resignation of the Prime Minister. Photo by Sanji Dee, Copyright @Demotix (5/5/2014)

Waandamanaji wanaoipinga serikali wakiwa wamekusanyika katika mkutano wa hadhara kumwuunga mkono Mfalme Bhumibol Adulyadej. Waandamanaji hao wanadai kujiuzulu kwa Waziri Mkuu. Picha na Sanji Dee, Hati miliki @Demotix (5/5/2014)


Si muda mrefu baada ya maandamano ya harakati ya kupinga uchaguzi, yanayoratibiwa na chama cha People Democratic Reform Committee (PDRC) kilichopata ushindi wao kufuatia kuvurugwa kwa uchaguzi wa Februari nchini Thailand, tarehe mpya imepitishwa kura zitapigwa tarehe Julai 20. Waziri Mkuu aliye kwenye shinikizo Yingluck Shinawatra alionekana mwenye furaha kwamba yeye labda anaweza kubaki madarakani kwa muda mrefu kidogo, licha ya kukabiliwa na mashtaka mawili ya ufisadi.

Mahakama itatoa hukumu ya madai hayo kesho, Mei 7, 2014, na Yingluck anaweza kuong'olewa madarakani kama atapatikana na hatia.

Je, wanannchi wa Thailand wana hamasa yoyote ya kufanya uchaguzi kwa mara ya pili ndani ya muda wa chini ya miezi sita?

Uchaguzi baada ya uchaguzi imeonyesha kuwa wapiga kura nchini Thailand wana “wasiwasi” na “kuhofia” uchaguzi unaokuja. Wengi wanaamini kwamba uchaguzi huo hautaweza kutatua migogoro ya kisiasa iliyodumu kwa karibu muongo mzima ambayo imesababisha Thailand kutawaliwa na mawaziri wakuu 6, serikali 5, chaguzi 3 na mapinduzi ya kijeshi mara moja. Zaidi ya hayo, uchaguzi mpya unaweza kugharamu kiasi cha bilioni 3.8 baht ($127,000,000) ambazo ni mzigo mwingine kwa walipa kodi – ambao baadhi yao ni wafuasi wa chama cha PDRC kinachoweza kususia uchaguzi kabisa. Hii itakuwa kupoteza fedha, muda, rasilimali na kusumbua vichwa vya watu kama mambo yale yale yatatokea.

Wapinzani waligomea uchaguzi wa Februari wakidai kwamba mchakato wa uchaguzi haungekuwa huru na haki kama familia ya Waziri Mkuu itaruhusiwa kushiriki. Uchaguzi ulifanyika hata hivyo, ingawa ilibidi kukabiliana na maandamano makubwa mitaani yaliyoandaliwa na wapinzani kwa zaidi ya miezi mitatu.

Mazungumzo katika mitandao nchini Thailand yanaonekana kuonyesha kutokuwa na matumaini miongoni mwa wapiga kura nchini humo:

Chaichol MCFC aliandika kwenye mtandao Pantip:

Sidhani kama kutakuwa na uchaguzi. Si kwa sababu ya serikali, lakini kwa sababu ya Taug [Suthep] na washirika wake. Alisema atafanya mageuzi nchini ndani ya kipindi cha miezi 6, lakini hakufanya chochote zaidi ya kuomba [fedha] mitaani na kusababisha uharibifu.

1204962 anadhani labda mapinduzi mengine yanahitajika:

Tayari nyumba imevunjwa na madaraka yamerudishwa kwa watu wale wale. Nini kingine tunaweza kufanya [kutatua mgogoro]. Mapinduzi tu mengine ya kijeshi, tafadhali.

Wafuasi wa chama cha PDRC walikwenda mbali zaidi na kuwataka watu kufanya hujuma kwenye uchaguzi huo.

Kwa Suthep – kiongozi wa chama cha PDRC -ukurasa wa Facebook, maelfu ya maoni yalimiminika kwa lengo la kusaidia kampeni ya kupinga “Mageuzi kabla ya Uchaguzi”. Max Chakrit aliandika:

Utawala wa wengi haufanyi kazi nchini Thailand kwa sababu sauti ya wengi huja kutoka kwa watu wasio na elimu (lakini katika nchi nyingine, utawala wa wengi ni mzuri). Hii ndio sababu watu wa Thailand hutawaliwa kwa urahisi ….

Porn Pramualsap pia alitoa maoni:

Yeyote anayeendesha nchi, haijalishi, muhimu asiwadanganye wakulima.

Wiki chache zijazo ni za muhimu kama uchaguzi utafanyika kama ilivyopangwa. Vikwazo viwili vikubwa ni pamoja na ikiwa Yingluck atakwepa mashtaka mawili yanayomkabili; na kingine ni ikiwa siku ya usajili kwa mgombea, iliyowekwa Mei 25, itaenda vizuri. Namna usajili utakavyofanyika kwa mafanikio ndiyo itakuwa kiashiria cha uchaguzi kufanyika.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.