Muda mfupi baada ya waandamanaji kuvamia bunge la Taiwani wakipinga makubaliano yenye utata kati ya nchi hiyo na China, mji mkuu wa visiwa hivyo Taipei vilifurika waandamanaji kuanzia Aprili 26 mpaka 30, mara hii wakipinga kiwanda cha nne cha uzalishaji wa nguvu za nyuklia kinachoendelea kujengwa ingawa inahofiwa kuwa kinaweza kusababisha madhara.
Polisi waliwalazimisha waandamanaji kutawanyika na waliweka miiba na uzio kuwazuia kuzudi. Maandishi yenye maneno chevaux de frise yaliwekwa kuzunguka ikulu ya nchi hiyo, Bunge la Yuani na Majengo ya Serikali ya Yuan pamoja na majengo mengine ya kiserikali.
Wakijibu hatua hiyo, waandamanaji hao walitumia ubunifu. Walipamba uzio uliowekwa na polisi kwa utepe wenye maneno ya kupinga nguvu za nyuklia, wakaweka mabango ya kisiasa, maua na vitu vingine na hivyo kugeuza miiba iliyokuwa imewekwa na polisi kuwa kama maonyesho ya kazi ya sanaa. Watumiaji wengi wa mtandao nchini humo walitumiana picha zenye mapambo hayo, na hapa chini ni baadhi ya picha hizo: