China Yamweka Kizuizini Mwanasheria wa Haki za Binadamu Pu Zhiqiang

China imemweka kizuizini mwanasheria maarufu mtetezi wa haki za binadamu Pu Zhiqiang ikimtuhumu ‘kusababisha usumbufu,’ kwa kile kinachoonekana kuwa jaribio la kuhamisha mawazo ya wanaharakati ili wasilipe uzito tukio la maandamano ya 25 ya kudai demokrasia ilivyominywa kwa muda mrefu kwenye Viwanja vya Tiananmen.

Kwa mujibu wa gazeti la South China Morning Post, Pu amekamatwa kama mhalifu na plisi wa Beijing baada ya kuwa amehudhuria mkutano wa kuadhimisha kuminywa kwa demokrasia pamoja na “kurudusu maana na matokeo yake na kutoa wito wa uchunguzi wa kina kuhusu ukweli wa yaliyotokea siku ya Juni 4.’’

Watu wasiopungua 15 -wakiwemo wanazuoni, wanaharakati na jamaa wa wahanga waliouawa kwenye ghasia za Tiananmen – walihudhuria mkutano huo kwenye nyumba ya mtu binafsi jijini Beijing mnamo Mei 3, 2014. Watu wengine wasiopungua watano wamechukuliwa kwa mahojiano baada ya mkutano huo.

Photos of Xu protesting (photo from twitter)

Picha ya Pu katika maandamano ya 1989 katika viwanja vya Tiananmen. Picha hiyo inasambazwa kwenye  mtandao wa twita.

Pu ni mtu maarufu anayejulikana kwenye harakati za Weiquan, akiwa amewahi kuwatetea waandishi na wanahabari katika kesi kadhaa maarufu, ikiwa ni pamoja na msanii Ai Weiwei. Aliandikwa sana kwenye magazeti kwa kuongoza kampeni dhidi ya makambi ya kufanyishwa kazi. 

Kufuatia tabia yake ya kukosoa sera rasmi za serikali, Pu amejikuta mara kadhaa akifuatiliwa sana na vyombo vya usalama, na amekamatwa na kuhojiwa mara nyingi.  Pu  alipigwa marufuku kufanya chochote kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii nchini China mwaka 2013 baada ya kuwa ameyatumia majukwaa hayo kumkosoa hadharani kiongozi mkuu wa Chama cha Kikomunisti Zhou Yongkang.

Pu vile vile alishiriki kwenye harakati za kudai demokrasi mwaka 1989 wakati huo akiwa mwanafunzi.

Habari zozote zinazohusiana na harakati za Tiananmen bado zinazuiwa nchini China. Kutafuta chochote kinachohusiana na neno “Tiananmen” kwenye mtandao maarufu wa kijamii nchini China Sina Weibo  kutakutana na ujumbe unaomfahamisha mtafutaji kuwa majibu hayawezi kupatikana kwa mujibu wa sheria na kanuni zinazohusika.
Wanasheria wengi wameonyesha kuguswa na yaliyomtokea Pu na wametoa mwito wa kuachiwa mara moja kwa Pu kupitia mtandao wa Weibo. Hata hivyo, jumbe nyingi zinazoonyesha kumwuunga mkono Pu zimekuwa zikifutwa. 

Ujumbe wa mwanasheria wa Bejing Deng Shulin  ulifutwa haraka sana baada tu ya kuonekana:

邓树林律师: 必须释放浦志强!抓律师是今后司法改革的方向吗?

Pu Zhiqiang lazima aachiliwe. Hivi kweli kukama wanasheria ndio mwelekezo mpya wa kuboresha mahakama?

Msanii mwigizaji maarufu wa China Zhang Ziyi aliwaomba wafuatiliaji wa habari zake kwenye mtandao wa Weibo kutazama filani inayohusu namna wanasheria wanavyosaidia kutafutwa kwa haki:

《辩护人》一个追求民主、法制、公正为真理而斗争的律师让人肃然起敬。故事改编于韩国前总统卢武铉的真实事迹。在这儿无需再说电影拍得如何了,去看看人家拍的内容吧!

“Counsel”, mwanasheria anayeheshimiwa kwa kupambana akitetea demokrasia, utawala wa sheria na haki. Filamu hiyo imetumia masimulizi ya kweli ya rais wa zamani wa Korea Roh Moo-Hyun. Hakuna haja ya kurudia hapa namna filamu hiyo inavyoonekana, nenda ukaitazame!

Maya Wang wa shirika la Human Rights Watch alikuwa na maoni haya kwenye mtandao wa twita:

Kukamatwa kwa Pu na wengine ni tangazo muhimu zaidi kwenye maadhimisho ya miaka 25 na kwa kweli litavutia macho ya watu kuliko serikali inavyodhani.

Mwandishi Sui-Lee Wee alinukuu nsha iliyoandikwa na Pu kwenye mtandao wa twita:

Nilifurahi kusoma nsha ya Pu Zhiqiang ya Juni 4. “Kama kila mmoja atasahau, je hatutakuwa tunafungua mlango wa mauaji ya kimbari kwa siku zijazo?

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.