Habari kuhusu Amerika Kusini kutoka Novemba, 2009
Brazil: Je, Milango ya Benki Hubaini vyuma au Rangi za Watu?
Benki nyingi nchini Brazil zinatumia milango inayozunguka yenye vifaa vya kubaini vyuma. Je, milango hiyo inatumika kama kisingizio cha kubagua watu? Video ya uandishi wa kiraia inaonyesha moja ya matukio hayo.
Brazil: Mtazamo wa Wakazi wa Vitongoji Maskini
Katika makala hii, tunasikia mitazamo ya wanahabari raia kutoka mradi wa Viva Favela kuhusiana ya vurugu inayotokana na mihadarati huko Rio de Janeiro na jinsi inavyofagia makazi ya walalahoi, kama wanavyoiona mbele ya milango ya nyumba zao.
Paraguay: Wenyeji Wanyunyiziwa Dawa za Kuua Wadudu kwa Ndege
Huko Mashariki mwa Paraguay, jumla ya watu 217 wa jumuiya ya wenyeji ya Ava Guaraní walianza kusumbuliwa wakionyesha dalili mbalimbali za kiafya zinazoaminika zilisababishwa na unyunyiziaji wa makusudi wa dawa za kuua wadudu hasa baada ya wao kuwa wamegoma kuhama kutoka katika ardhi waliyoirithi kutoka kwa mababu zao.
Venezuela: Kukutana na kazi za msanii Jesus Soto
Kazi za msanii wa Kivenezuela Marehemu Jesus Soto zinapaswa kuguswa na kujizamisha ndani yake ili kuzielewa. Wachache waliwahi kutembelea kazi zake kwenye makumbusho wameandika uzoefu wao.
Video: Dunia Yaadhimisha Kuanguka kwa Ukuta wa Berlini
Leo ni Kumbukumbu ya 20 ya kuanguka kwa Ukuta wa Berlini, kizingiti madhubuti cha kiusalama ambacho kiliwahi kuligawa jiji la Berlini katika pande mbili za Mashariki na Magharibi huko Ujerumani. Leo tunaonyesha baadhi ya picha za video zinazotoka pande mbalimbali za dunia zinazopandishwa ili kusherehekea siku hii na nini ukuta huo ulimaanisha siyo Ujerumani tu bali duniani kote.
Cuba: Ukweli wa Sanchez Kutiwa Mbaroni Waibuka
Kukamatwa, kupigwa na kuachiwa huru kulikofuata kwa wanablogu Yoaní Sánchez, Claudia Cadelo na Orlando Luis Pardo kulikofanywa na majeshi ya usalama ya Cuba tarehe 6 Novemba, kunapata matangazo mengi katika...
Yoani Sanchez Pamoja na Wanablogu Wengine wa Cuba Wakamatwa na Kupigwa
Jioni ya tarehe 6 Novemba, blogu ya Babalú iliweka kiungo kuelekea makala iliyoandikwa na Penultimos Dias (es) ilitoa taarifa kuwa baadhi ya wanablogu mashuhuri wa Cuba, wakiwemo Yoaní Sánchez na...
Bolivia: Uhaba wa Maji Kwa Sababu ya Theluji Inayoyeyuka
Safu ya milima ya Chacaltaya ina baadhi ya vilele ambavyo ni alama zenye maana katika safu ya milima Andes iliyopo Bolivia. Kwa kuwa ilikuwa ni sehemu moja pekee ambapo mchezo...
Amerika ya Kati: Kasi Kubwa ya Ueneaji wa Jangwa
Ueneaji wa jangwa unasambaa kimyakimya lakini kwa kasi kubwa mahali pengi duniani na Amerika ya Kati haijaweza kukwepa hali hii iliyo na athari mbaya za kutisha. Wakati ambapo majangwa ni maumbo ya asili, ueneaji wa jangwa ni mchakato wa kuharibika kwa nyanda za ardhi kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na uharibifu unaofanywa na binadamu.
Ujauzito na Magereza: Afya na Haki za Wanawake Magerezani
Mapambano bado yanaendelea kuhakikisha haki za binadamu kwa wanawake wajawazito duniani pote, ni inaelekea kwamba katika mchakato huo, wanawake waliopo magerezani wanasahauliwa. Je ni hatua zipi zilizochukuliwa kuhakikisha kuwa nao wanaangaliwa kwa utu, kwa kuzingatia uhai wanaoubeba.