· Novemba, 2010

Habari kuhusu Amerika Kusini kutoka Novemba, 2010

Peru: Kampeni ya Kuzuia Kufungwa kwa Maktaba ya Amazon

  11 Novemba 2010

Juan Arellano wa Globalizado [es] anaripoti juu ya kampeni ya kuzuia kufungwa kwa maktaba huko Iquitos, Peru , maktaba ambayo inatilia mkazo vitabu na masuala yanayohusu Amazon. Maktaba hiyo ni ya pili kwa umuhimu katika masuala ya Amazon huko Marekani ya Latini.

Watu wa Uruguay Waomboleza Kifo cha Mwanamuziki José Carbajal, ‘El Sabalero’

  11 Novemba 2010

Mwimbaji na mtunzi José Carbajal, anayejulikana kwa jina la utani kama “el Sabalero,” amefariki kutokana na shambulio la moyo mnamo Oktoba 21 akiwa na umri wa miaka 66. Carbajal anachukuliwa kuwa gwiji na utambulisho wa utamaduni wa Uruguay. Mwaka huu alikuwa akifanya kazi na wasanii wengine katika mradi wa Kompyuta Moja ya Mapajani kwa Kila Mtoto nchini Uruguay Uruguay, Mpango wa Ceibal, ili kutumbuiza kwenye maonyesho kwa ajili ya watoto wa shule nchini kote.