Habari kuhusu Amerika Kusini kutoka Januari, 2010
Colombia: Ugumu wa Kutofautisha Wazuri na Wabaya
Kwa kupitia upigaji video wa kiraia, asasi tofauti nchini Colombia zinatoa mitazamo yao kuhusu uhalifu, unyama na migogoro inayohusisha matumizi ya silaha, ambayo ni vigumu kuwatofautisha watu wazuri kutoka kwa wabaya.
Haiti: Madhira ya Tetemeko la Ardhi
Mpaka sasa taarifa za majeruhi wanaotokana na tetemeko la ardhi lililoikumba Haiti zimejikita kwenye takwimu za kutisha, lakini ni majina machache tu ndiyo yameambatanishwa kwenye namba hizo. Katika makala hii tunapata simulizi za wale walionusurika kutoka kwenye janga hili la asili kama wanavyozirusha kwenye mtandao.
Bolivia: Mshindi wa Zamani wa Mashindano ya Urembo Atangazwa Kugombea Ugavana wa Jimbo la Beni
Bolivia Jessica Jordan kuwa mgombea wa kiti cha ugavana kwa tiketi ya Chama Cha Ujamaa (MAS) huko kwenye jimbo la Beni, ambalo kwa kawaida hudhibitiwa na upinzani.
Picha ya Dunia Katika Siku ya Kupinga Rushwa Duniani
Katika matayarisho ya uzinduzi wa mtandao wa teknolojia na Uwazi, hii ni makala ya kwanza kabisa katika mfululizo wa makala ambazo zitavinjari mada zinazohusiana kwa kupitia macho ya wanablogu wa dunia.