Habari kuhusu Amerika Kusini kutoka Disemba, 2009
Ecuador: Serikali Yaifungia Idhaa ya Televisheni ya Teleamazonas
Serikali ya Ecuador iliiondoa idhaa ya televisheni ya teleamazonas kwa masaa 72 kwa kusambaza habari za uongo. Wakosoaji wanaona kuwa hatua hii ni tishio kwa uhuru wa kujieleza.
Brazil: Wito wa Kugomea Gazeti Linaloongoza Nchini
Wanablogu wa Brazili wamekuwa wakihamasisha mgomo dhidi ya kile walichokiita Coupist Press Party, yaani Sherehe ya Chombo cha Habari ya Kutaka Kupindua Serikali, kwa hiyo wamekuwa wakiwataka watu kuacha kununua, kusoma au kutoa maoni na badala yake kufuta usajili wao kutoka kwenye gazeti la Folha de São Paulo na tovuti yake.
Guatemala: Kuvunja Milango ya Madanguro
Blogu inayojulikana kama Noticias para Dios inatoa habari za ndani, kama vile mambo yenyewe yanavyotokea pasipo kuficha kitu, kuhusu maisha ya kila siku ya mwanasheria wa Ki-Guatemala anayejaribu kuwaokoa watoto kutoka kwenye madanguro ambako wamekuwa wakiishi baada ya kuchukuliwa kutoka makwao.