Brazil: Je, Milango ya Benki Hubaini vyuma au Rangi za Watu?

Usiku wa mkesha wa Siku ya Kujivunia Weusi nchini Brazil – inayosherehekewa tarehe 20 Novemba, wakati nchi inapofufua vita vinavyoendelea dhidi ya ubaguzi – Circo Voador Audiovisual Collective ilifanya jaribio. Waliwarekodi wanachama wao wawili katika filamu, ambao wana rika moja na waliovalia mavazi yanayofanana, wakijaribu kuingia benki katika benki moja katika nyakati tofauti, huku wakiwa wamebeba mikoba iliyojaa vyuma – funguo, sarafu, simu za mkononi. Mmoja wao alichukua sekunde chache kuingia bila ya matatizo yoyote; mwingine hakuweza kuingia, alizuiwa na mlango unaozunguka, ambao ni kitu cha kawaida katika mabenki mengi nchini Brazil. Kijana wa kwanza alikuwa mzungu, wa pili, mtu mweuzi. Angalia matokeo:

Kwa mujibu wa waliotengeneza filamu, jaribio hili limeonyesha kuwa milango yenye vifaa vinavyobaini vyuma huwa inawashwa na walinda usalama kwenye mabenki. Kwa maneno mengine, taratibu za ulinzi ambazo benki inazitumia hivi sasa zinategemea maamuzi ya watumishi, maamuzi ambayo mara nyingi hugubikwa na dhana zilizokuwepo kabla ya tukio, imani potofu na ubaguzi dhidi ya watu wa aina fulani. Kwenye blogu yao, Circo Voador [Sarakasi inayopaa, pt] anawakaribisha wasomaji kujiunga, kwa kutuma video zao za watu weusi tofauti tofauti wengi inavyowezekana. Wnafafanua jaribio hilo:

Na primeira cena aparecem várias pessoas ao redor da bolsa. Todas elas fizeram o teste com a mesma bolsa, algumas foram barradas outras não. Em nenhum momento alguém alterou o conteúdo dos pertences na bolsa. A escolha da imagem do MC Shackal não se deveu ao fato dele ser negro e sim, por termos nos utilizado de câmeras escondidas e o momento em que o registramos, não sofreu interferências externas, como carros ou pessoas paradas na frente da câmera.

Katika sehemu ya kwanza ya filamu kuna watu wengi waliokuwepo karibu na mkoba. Wote walifanya jaribio kwa kuubeba mkoba ule ule mmoja, wengine walizuiwa na wengine hawakuzuiwa. Hakuna aliyebadilisha vitu vilivyokuwemo ndani ya mkoba. Tumeamua kuijumusha sehemu ya filamu tuliyoipiga na MC Shackal siyo kwa kuwa yeye ni mtu mweusi lakini ni kwa sababu tulitumia kamera iliyofichwa na wakati tuliponpiga picha, hapakuwa na vitu vilivyoingilia, kama vile magari au watu waliosimama mbele ya kamera.

Watu wengi walitoa maoni kwenye kisanduku cha maoni cha blogu ya Circo Voador. Baadhi ya wasomaji walishawahi kukutwa na mikasa inayofanana na huu kama Dona Biologia [pt], ambaye ni mwalimu:

Coloquei chaves, celular, bolsinha de moedas no local indicado e a porta apitava e travava. Por fim, o rapaz chamou um pseudo gerente que atravessou a porta e, dentro do caixa eletrônico da agência, me fez abrir a bolsa de provas e quando não viu nada que justificasse, teve a audácia de dizer que fora a minha bolsinha de lápis. Me arrependo até hoje de não ter processado o banco pelo constrangimento.

Niliweka funguo, simu ya mkononi, pochi ya sarafu katika sehemu iliyoelekezwa na bado mlango uliwasha king’ora na kujifunga. Hatimaye, yule kijana alimuita meneja uchwara ambaye alipita mlangoni na, katika mashine ya kutolea pesa, akanitaka nifungue mkoba wangu [wa mwanafunzi] wa makaratasi ya insha na aliposhindwa kukuta chochote kilichoweza kuhalalisha [tabia yake] alikuwa na ujasiri wa kuniambia kuwa sababu ilikuwa ni kasha langu la penseli. Bado ninasikitika kwa kutoishitaki benki kwa kunizuia.

Christiano J. Jabur [pt], ambaye aliwahi kuzuiwa katika mlango wenye vifaa vya kung’amua vyuma mjini Sao Paulo kwa sababu ya kubeba kamera ya kidijitali, anadai kuwa ubaguzi dhidi ya watu kwenye milango ile ile ya kuzunguka hutokea kwenye mabenki bila kujali rangi ya ngozi:

Tive que colocá-la numa caixinha para conseguir entrar no banco. Mas uma senhora de idade, também branca, que tentou entrar na agência da Nossa Caixa, na mesma cidade, foi barrada e não conseguiu entrar de jeito nenhum, mesmo chamando a polícia. O gerente do banco ininuou que ela poderia ser criminosa, pois existem muitas pessoas hoje, acima dos 50 e 60 anos de idade, cometendo crimes (o que não deixa de ser verdade). Não vou dizer que não exista preconceito contra negros e pardos nos bancos, por parte de vigilantes e atendentes. Mas dizer que são só os negros que são barrados nas portas giratórias é uma bela de uma mentira.

Ilinibidi niiweke [kamera] katika kasha ili niweze kuingia ndani ya benki. Lakini mwanamke mzee, mzungu, alijaribu kuingia katika tawi la Nossa Caixa kwenye mji ule ule alizuiwa na hakuweza kuingia kabisa, hata baada ya kuwapigia simu polisi. Benki iliashiria kuwa angeweza kuwa jambazi, kwa sababu kuna watu wengi wenye zaidi ya miaka 50 mpaka 60 ambao hufanya makosa siku hizi (jambo ambalo ni kweli). Siwezi kusema kuwa walinzi wa usalama na wahudumu kwenye mabenki hawana ubaguzi dhidi ya watu weusi na wale wenye rangi ya kahawia. Lakini kusema kwamba watu ni weusi pekee ambao huzuiliwa katika milango inayozunguka ni uongo.

Katika upande mwingine, mlinzi wa usalama aitwaye Leandro [pt] anafafanua katika kisanduku hicho hicho cha maoni jinsi mfumo unavyofanya kazi, na anakosoa namna ambayo video ile ilivyotafsiriwa na baadhi (ya watu):

Sou Vigilante (segurança), e posso afirmar, este sistema é falho, mas este vídeo esta sendo usado para sujar a imagem de profissionais que estão apenas cumprindo ordens… os ‘controles’ podem sim travar e destravar as portas giratórias, mas isso não é valido para todas as agencias, são sistemas diferenciados pra cada agencia ou cada porta giratória… e não temos controle sobre o “Nível de travamento“ de cada porta (isso é de responsabilidade do gerente), que costuma variar de 4 a 7 níveis, por isso vc pode entrar em uma agencia e ficar travado e em outra passar sem problema algum…
Sei que intenção de vc's não é esta, li o que estão propondo e apoio totalmente, mas não esta sendo divulgado desta forma, outros sites e meios de comunicação estão colocando informações “picadas”, pela metade… eu mesmo recebi um Email como Titulo: “Vigilantes racistas?”

Mimi ni mlinzi wa usalama na ninaweza kukwambia kuwa mfumo huu una makosa, lakini video hii inatumika kuichafua sifa ya wafanyakazi ambao wanafuata amri tu… kuna ‘vidhibiti’ ambavyo kwa hakika huweza kufunga au kufungua milango inayozunguka, lakini hii si kweli katika matawi yote, mfumo ni tofauti kwa kila tawi au kila mlango unaozunguka… hatuna uwezo wa kudhibiti ‘ngazi ya ufungaji’ wa kila mlango ambayo huwa kati ya ngazi ya 4 mpaka 7 (huu ni wajibu wa meneja), na hii ndiyo sababu inayokufanya ukamatwe kwenye mlango wa tawi moja lakini ukaweza kuingia ndani ya tawi jingine bila ya matatizo…
Ninajua kuwa haikuwa nia yako, nimesoma kile unachokusudia kukisema na nikiunga mkono kabisa, lakini (kile ulichokusudia) hakisambazwi hivyo, tovuti nyingine na vyombo vya habari vimechapisha vipande vya taarifa nusu… mimi binafsi nimepokea barua pepe yenye kichwa cha habari: “Walinzi wa usalama wabaguzi?”

Kadhalika video hiyo imeenea haraka kwenye ulimwengu wa blogu. Rafael Cesar [pt] anasema kwamba milango kujifunga kwa watu weupe au weusi si kiini cha suala hili:

A questão é que sabemos que aquele detector de metais é muito mais uma desculpa para os seguranças fazerem o controle da forma como julgam apropriada do que qualquer outra coisa. O que trava, mesmo, é aquele controlezinho que eles carregam. Comigo é rotineiro, sem qualquer exagero, passar por aquela porra sem metal nenhum na mochila (já deixei até estojo naquela caixinha ao lado por causa de lapiseira) e me travarem. Ou seja: o que volta e meia detectam em mim é um meliante em potencial, porque por várias vezes não havia qualquer metal a ser detectado. Se eu não tinha metal, por que ‘a porta’ travou? E, se eu tenho metal, por que logo em seguida ‘a porta’ destrava?E nessa de o crivo da segurança passar pelos olhos dos seguranças, é claro que o indivíduo negro leva a pior. Assim como leva a pior com a polícia, com emprego etc.

Kiini cha suala ni kuwa tunafahamu kwamba vifaa vya kung’amua vyuma, zaidi ya yote, ni kisingizio cha walinzi wa usalama walio kwenye zamu kutumia uamuzi wao katika njia wanayoona sawa. Milango hufungwa, kwa kutumia kifaa kidogo wanachokibeba cha kuwashia na kuzima. Kwangu ni tabia, bila ya kutaka kujikuza, kupita katika upumbavu ule bila ya chuma chochote kwenye mkoba wangu wa mgongoni (nimewahi hata kuacha kasha pembeni kwa sababu ya kichongeo cha penseli cha chuma) hata hivyo nilizuiwa. Kwa maneno mengine: kitu wanachokiona kwangu kila wakati ni kuwa nina uwezo wa kuwa mwizi, kwani mara kadhaa sikuwa na chuma ambacho kingeweza kubainiwa. Ikiwa sikubeba chuma chochote, kwa nini mlango ulijifunga? Na kama nimebeba chuma, kwa nini basi mara tu milango hujifungua? Kwa kuwa hatua za usalama huchujwa kwa kutumia macho ya walinzi wa usalama, bila ya shaka mtu mweusi ana wakati mgumu zaidi. Kwa namna sawa sawa na mbavyo ana wakati mgumu zaidi na polisi, kwenye kuomba kazi n.k…

Helio Ventura [pt] anachukua fursa kuchapisha maandishi yaliyochapwa kwanza mwezi Machi 2007 na kuuliza kama milango hubaini vyuma au melanin (chembe hai zinazosababisha kuwa na ngozi nyeusi) baada ya mteja mweusi kuuwawa ndani ya benki jijini Rio de Janeiro:

Rio de Janeiro, sexta-feira, 22 de dezembro de 2006, 13 horas e 20 minutos. O micro-empresário negro Jonas Eduardo Santos de Souza, 34 anos, estava na fila da agência do banco Itaú da Av. Rio Branco, da qual era cliente há 10 anos, para operações de rotina. Mas ele foi vítima do racismo que persiste em existir em nosso país, apesar de muitas vozes da elite e da intelectualidade negarem. Ele foi morto com um tiro no peito por Natalício de Souza Marins, 29 anos, vigilante da agência.
Ao tentar entrar na agência bancária, Jonas foi parado pela conhecida e constrangedora porta giratória. Ele foi abordado por Natalício e obrigado a pôr na bandeja todos os objetos que possuía. Como a porta continuava travando, Jonas foi obrigado a tirar inclusive o cinto. O gerente foi acionado por Natalício, e só autorizou o acesso do jovem micro-empresário à agência após exigir que Jonas provasse ser cliente da agência, mostrando um cartão do banco. Após o constrangimento, já dentro da agência, Jonas e Natalício continuaram a discutir, até que o vigilante, demonstrando total despreparo para o exercício da função, sacou seu revólver e matou Jonas, que não teve chance de defesa. […]
Assim como também poderíamos estar do outro lado, o de Natalício, também negro, um pai de família que teve suprimidas as oportunidades de acessar uma profissão que pudesse dar melhores condições à sua filha de 5 anos, que se viu obrigado a pleitear apenas funções que exigem menor qualificação, como a de vigilante. Ele também foi atingido pelo racismo estrutural que assola este país. Isso em nada muda o fato dele ter agido equivocadamente: é um homicida e deve receber as sanções legalmente previstas. E ser também negro não atenua o crime. Mas nos faz perguntar: que sistema é este que coloca dois semelhantes em lados opostos, fazendo com que um tire a vida do outro? Até quando fatos como este acontecerão? Percebemos o quão perverso é este “racismo à brasileira”, uma política de extermínio silenciosa, disfarçada de risco social e fatalidade.

Rio de Janeiro, Ijumaa, Disemba 22, 2006, saa 7:20 mchana. Mjasiriamali mweusi Jonas Eduardo Santos de Souza, umri mika 34, alikuwa amepanga foleni ili kupata huduma ya kawaida katika tawi la benki ya Itau katika Rio Branco, ambako alikuwa mteja kwa muda wa miaka 10. Lakini alikuwa muathirika wa ubaguzi ambao unaendelea kuwepo katika nchi yetu, pamoja na kukataa kuwa ubaguzi haupo, kukataa ambako kunatoka kwa makundi mengi ya wataalamu na wasomi. Aliuwawa kwa kupigwa risasi kifuani na mlinzi wa usalama kwenye tawi hilo, Natalício Marins de Souza, 29.
Wakati akijaribu kuingia kwenye tawi hilo, Jonas alizuiwa na milango inayozunguka inayojulikana vyema kwa kuwatia watu aibu. Alijongelewa na Natalicio na kulazimishwa kuweka vitu vyake vyote kwenye sinia. Mlango ulikuwa bado umefungwa, Jonas alilazimishwa hata kuvua mkanda wake. Natalicio akamuita meneja, ambaye alimruhusu huyu mjasiriamali kijana baada ya kumtaka Jonas kuthibitisha kuwa alikuwa ni mteja wa wa tawi lile, kwa kuonyesha kadi yake. Baada ya aibu ile, ndani ya benki, Jonas na mlinzi wa usalama waliendelea kubishana mpaka mlinzi yule wa usalama, alipodhihirisha kuwa hakuwa na uwezo wa kuifanya kazi yake, alitoa bunduki na na kumuua Jonas, ambaye hakuwa na uwezo wa kujikinga. […]
Tunaweza kuwa upande wa Natalicio, ambaye pia ni mweusi, baba wa familia ambaye hakuwa na fursa ya kupata taaluma ambayo ingemwezesha kumpa mazingira bora binti yake wa miaka 5, hivyo kulazimika kuomba kazi ambazo zinahitaji vigezo vya chini zaidi, kama vile kazi ya ulinzi wa usalama. Na yeye naye alikumbwa na ubaguzi wa kimfumo unaoisibu nchi hii. Hii haibadili ukweli kuwa alifanya makosa; ni muuaji na anapaswa kupokea adhabu zinazotolewa na sheria. Kadhalika kuwa mweusi hakupunguzi kosa. Lakini inatufanya tujiulize: huu ni mfumo wa namna gain unaowaweka watu wawili walio sawa kwenye pande tofauti, na kumsababisha mmoja kuchukua maisha ya mwingine? Mpaka lini matukio kama haya yataendelea kutokea? Tunaona gani ‘ubaguzi’ ulivyo mbaya katika Brazil, sera ya kimya kimya inayomaliza watu, iliyojificha kama hatari ya kijamii na ajali isiyozulika.

Andréia Freitas [pt], ambaye aliwahi kufanikiwa kuingia ndani ya benki bila bugudha na kisu cha jikoni ambacho alikuwa amekinunua kabla, anasema kuwa hitimisho la kusikitisha ni kuwa watu huona sura ya nje tu ya watu wengine:

Por que será que cresceram os assaltos a banco realizados por homens de terno e gravata? Por que será que hoje existe o roubo de carros em estacionamentos e os assaltantes chegam no local pra assaltar de carro importado? Golpes de estelionatários em hotéis de luxo, em lojas de grife, em restaurantes cinco estrelas…

A resposta é óbvia: O mundo é movido por “aparências”! Sim… se você é considerada uma pessoa “bem apessoada” a vida fica mais fácil pra você em todos os aspectos. Agora… se você não está tão “bem vestido”, ou seu cabelo “acordou” num dia ruim, ou seu sapato tá meio surrado, pode apostar que a vida não será bolinho pra você.

O ser humano vê as aparências! Se as portas dos bancos fossem realmente controladas por uma máquina, por um dispositivo eletrônico de segurança, os dois caras do vídeo do YouTube tinham sido barrados! E nada mais justo do que barrar OS DOIS, que portavam objetos de metal.

Ni kwa nini ujambazi katika mabenki unafanywa na watu waliovalia suti na tai? Kwa nini siku hizi magari huibwa kwenye sehemu za maegesho na majambazi huwasili katika magari yaliyoagizwa kutoka nje ya nchi? Utapeli kwenye mahoteli ya kifahari, maduka ya wabunifu, migahawa ya nyota tano…

Jibu liko wazi: dunia inaendeshwa na “wajihi au jinsi unavyoonekana”! Naam… kama unaonekana ni kijana mwenye sura nzuri, maisha ni rahisi kwako kwa kila hali. Sasa… kama wewe si “mtanashati”, au kama uan siku ya nywele mbaya, au kama viatu vyako vimechakaa kidogo, unaweza kutabiri kuwa maisha hayatukuwa mepesi kwako.

Binaadamu huona jinsi watu wanavyoonekana! Kama milango ya benki ingekuwa inaendeshwa na mashine kati maana halisi, mashine ya umeme, vijana wawili walioonyeshwa kwenye video ya YouTube wangezuiwa! Na hakuna jingine lililo sawa zaidi ya kuwazuia WOTE WAWILI, kwani wote walikuwa wamebeba vifaa vya chuma.

Kuna kampeni ya kwenye mtandao [pt] iliyoanzishwa na jaribio linalozitaka benki za Brazil kuacha kutumia milango inayozunguka na kuwekeza kwenye mfumo wa mionzi (X-ray) au vifaa vya usalama ambavyo vinaonyesha vitu alivyonavyo mteja, kampeni hiyo imesainiwa na zaidi ya watu 2,000 mpaka sasa. Wito wa kampeni hiyo ni kuwa kila mtu anapaswa kuhudumiwa kwa heshima na kila benki.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.