· Machi, 2014

Habari kutoka Muhtasari wa Habari kutoka Machi, 2014

Iran: Mwanafunzi Ahukumiwa Miaka 7 Jela

Blogu ya PersianBanoo iliripoti kuwa “mwanafunzi mwanaharakati wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Qazvin aliyefukuzwa, Maryam Shafipour amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela. Awali iliripotiwa na familia yake kuwa alikuwa amepigwa na maofisa wa kiume waliokuwa wanamhoji wakati wa kuhojiwa kukiendelea”.

Matukio ya Ghasia Zinazofanywa na Majeshi ya Urusi nchini Ukraine

  4 Machi 2014

Blogu maarufu ya “Tafsiri za Maida ilichapisha bandiko la mtandao wa Facebook la Dmitry Tymchuk, Mkuu wa Kituo cha Ukraine cha Stadi za Siasa za Kijeshi, linaloeleza matukio ya ghasia za kimataifa zinazodaiwa kufanyika na “matendo yasiyo ya kawaida” tangu Februari 2014. Tymchuk anaanza uchambuzi huu kwa kusema: Kwa mfano,...

“Si rahisi kuwa Mhindi” nchini Marekani

  3 Machi 2014

Ricey Wild, Mmarekani wa asili anayeblogu kwenye blogu ya Indian Country Today, anandika kuhusu kuuawa kwa mbwa mwitu kwenye jimbo la Minnesota, Marekani. […]Rafiki yangu mpenzi Melissa alikuja kunichukua mwezi uliopita kwenda kwenye mkutano wa kupinga uwindaji wa mbwa mwitu kwenye jimbo la Mennesota na kwingineko. Tulipanda kaskazini na kuungana...

Trinidad na Tobago: Kati ya Serikali Mbili

  3 Machi 2014

Katika mukhtadha wa idadi na ukubwa wa miradi inayotekelezwa kwa kupitia mipango ya serikali ya nchi hiyo, Afra Raymond anaeleza kwa nini ushirika wa kiwango cha juu unaoonyeshwa hivi sasa na Trinidad na Tobago kwa China ni “suala nyeti linalostahili tafakuri ya kina.”

Majira ya Baridi Tajik, “Jiji Baya Zaidi Barani Asia”

  2 Machi 2014

Mwanablogu msafiri anaandika kuhusu namna alivyotumia muda wake wa msimu wa baridi jijini Dushanbe, mji mkuu wa Tajikistan.  Nilitumia sehemu kubwa ya sehemu ya majira ya baridi nikiwa nimejikunyata kwenye kifaa cha kupashia nyumba kiitwacho (pechka), huku nikiwa na kikombe cha chai mkononi. Baadhi ya nyakati za asubuhi kila kitu...

Kuhusu habari zetu za Muhtasari wa Habari

Hizi ni habari mpya zilizoandikwa kwa muhtasari.