Matukio ya Ghasia Zinazofanywa na Majeshi ya Urusi nchini Ukraine

Blogu maarufu ya “Tafsiri za Maida ilichapisha bandiko la mtandao wa Facebook la Dmitry Tymchuk, Mkuu wa Kituo cha Ukraine cha Stadi za Siasa za Kijeshi, linaloeleza matukio ya ghasia za kimataifa zinazodaiwa kufanyika na “matendo yasiyo ya kawaida” tangu Februari 2014. Tymchuk anaanza uchambuzi huu kwa kusema:

Kwa mfano, Februari 28, saa 2.45 asubuhi urukaji wa ndege 10 za kijeshi ulifuatiliwa na kituo cha uangalizi kilichopo katika eneo la Takil kutokea Shirikisho la Urusi kuelekea Ukraine.

Helkopita tatu (mbili KA-27 na moja Mi-8) ilitua kwenye uwanja wa ndege wa Kacha na kuvuka mpaka na utaratibu uliopo wa kudhibiti forodha kwa mujibu wa maombo yaliyoweka mwanzoni. Helikopta zilizobaki zilikuja karibu na uwanja wa ndege; hapo, hapakuwa na jibu lililopokelewa kuhusu ombi lililotolewa na mkuu wa mpaka kuhusu ulazima wa helikopta kupitia kwenye taratibu rasmi, zilizowasili bila maombi ya awali yaliyofanywa kwa kuvunja makubaliano yanayotakikana.
Mkuu wa mpaka wa kituo cha Huduma za Ulinzi wa Mpaka wa Ukraine alitoa tamko la kuvunjwa kwa taratibu za mpaka wa Ukraine uliofanywa na helikopta hizo.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.