-
Waziri wa Utamaduni na Ulinzi wa Uislamu wa Iran, Ali Jannati, alisema “Iran haiwezi kuufungia Mtandao wa Facebook milele.” Maofisa kadhaa wa Iran kama Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Kigeni, hutumia mitandao ya Twita na Facebook hata wakati tovuti hizo zimefungiwa nchini Iran.