Unaona lugha zote hapo juu? Tunatafsiri habari za Global Voices kufanya habari za kidunia zimfikie kila mmoja.

· Februari, 2014

Habari kutoka Muhtasari wa Habari kutoka Februari, 2014

Maandamano ya Venezuela: ‘Vyombo vya Habari vya Kimataifa: Ingilieni Kati!’

Mpendwa Mhariri wa Kimataifa:

Sikiliza na uelewe. Hali ya mambo imebadilika nchini Venezuela usiku wa kuamkia leo. Kile kilichokuwa kinaonekana kuwa hali ya kutokuelewana iliyokuwepo kwa miaka sasa imebadilika ghafla.

Kile tulichokishuhudia asubuhi hii si habari ya Venezuela uliyodhani unaielewa.

Kwenye blogu ya Caracas Chronicles Francisco Toro anashutumu kutokuwepo kwa vyombo vya habari vya kimatafa kutangaza ghasia na matukio yanayoendelea kukua tangu Februari 19.

Francisco anaonyesha picha za kurasa za habari za mashirika makubwa ya habari kama BBC, The New York Times, CNN, The Guardian, Al Jazeera idhaa ya Kiingereza, na Fox News asubuhi ya Februari 20 —yote hayana habari zozote kuhusu matukio ya ghasia tangu siku iliyopita.

Anahitimisha:

Kiwango cha kupuuzia hali ya mambo inayoendelea Venezuela kinashangaza sana.

Kufungiwa kwa vyombo vya habari vya ndani kunasindikizwa na “kususiwa” na vile vya kimataifa, ambavyo wala hakuna anayewafuatilia isipokuwa tu kupuuza na kuona kama yanayoendelea hayawahusu. Ni vigumu kueleza hisia za kutokusaidiwa unapotazama kurasa hizi na kutokuona chochote. Venezuela inawaka moto; hakuna anayejali.

Hebu niliweke hili wazi. Nyote mnahitaji kuingilia kati. Muda wa kutupilia mbali kile mlichodhani mnakielewa kuhusu Venezuela ndio huu.

Unaweza kuangalia ukurasa wa habari zetu maalumu kuhusu maandamano yanayoendelea Venezuela hapa.

VIDEO: Kuelekea Mfumo wa Haki na Jumuishi Nchini Chile

Katika video hiyo hapo juu iliyowekwa na Mfuko wa Jamii Wazi , Giorgio Jackson, kiongozi wa zamani wa wanafunzi na mbunge mpya kabisa nchini Chile, anajadili mfumo wa elimu nchini mwake na maanaa hasa ya kuwa “jamii wazi”.

Trine Petersen anaandika:

Mfumo wa haki na jumuishi unaoifanya elimu ipatikane kwa watu wote ni nguzo imara kwa jamii iliyo wazi na inayoheshimu haki, Inawezesha ushirikiano na kuaminiana. Wachile wanataka mfumo wa elimu unaohimiza elimu kuwa bidhaa huru kwa watu wote na inawawezesha raia wote kushiriki kwenye tafakuri tunuizi na kujieleza kwa uhuru zaidi.

Kiongozi wa Upinzani Nchini Venezuela Leopoldo López Ajisalimisha Serikalini

Kiongozi wa Upinzani nchini Venezuela Leopoldo López amejisalimisha mwenyewe kwa Vikosi vya Polisi, kama alivyokuwa ametangaza angefanya kwenye video [es] hiyo hapo juu.

López, kiongozi wa chama cha Voluntad Popular, alitakiwa  kujisalimisha kwa agizo la mahakama jijini Caracas kwa kutuhumiwa kuhusika na makosa ya jinai yanayohusiana na maandamano  yanayoendelea nchini Venezuela.    

Maandamano makubwa ambayo López alijisalimisha siku ya Februari 18 yalikuwa yalikuwa ya amani, na wafuasi wake walipiga kelele [es]  kumwuunga mkono. Twiti ifuatayo ina mkusanyiko wa picha za maandamano na pia za tukio la López kujisalimisha kwenye mamlaka za serikali jijini Caracas: 

Venezuela- Maandamano ya Februari 18

Video hii [es] ilipigwa wakati López akijisalimisha: 

Na kwenye video hii [es] unaweza kumsikia López akihutubia umati wa waandamanaji akiwa kwenye gari ya polisi lililokuwa likilindwa kwa silaha na ambalo lingempeleka kwenye Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali nchini Venezuela.

Mpaka toleo la lugha ya Kihispania la posti hii linaandikwa, watu walikuwa bado wako mitaani wakiandamana[es].

Wiki ya Mitandao ya Kiraia Jijini Lagos 2014

Wiki ya Mitandao ya Kiraia jijini Lagos 2014 (Februari 17-21) inaendelea jijini Lagos, Niajeria:

Wiki ya Mitandao ya Kiraia Lagos ndio kwanza mwaka wake pili kufanyika na tayari imepata umaarufu kama mkutano mkubwa zaidi wa kiteknolojia, mitandao ya kijamii na kibiashara barani Afrika. Tukio hilo limevutia wanazuoni maarufu, bidhaa maarufu, watu wajifunzao na wabunifu maarufu. Likiwa na idadi ya watu wapatao milioni 20, Lagos ndilo jiji kubwa la watu weusi duniani na inasemekana ni kitovu cha bara la Afrika na makazi ya makampuni makubwa ya kibiashara na kiteknolojia katika bara la Afrika. Kw akutambua umuhimu wa bara hili kuunganishwa, na kuhamasisha ushirikiano, dhima kuu ya mkutano wetu wa mwaka 2014 ni: AFRIKA ILIYOUNGANISHWA NDIYO MUSTAKABALI.

Tukio la pekee na la aina yake, Wiki ya Mitandao ya Kiraia Lagos ni mkutano wa kidunia unaohudhuriwa na watu wenye bongo zinazochemka kwa kiwango cha kidunia ambao hauna kiingilio na uko wazi kwa yeyote. WMK Lagos ni wa pekee kwa sababu asilimia 70 ya majopo, dhifa na warsha zimeandaliwa na umma