Hali ya mambo nchini Venezuela yaendelea kuzorota, huku pakiwa na maandamano na mikusanyiko nchi nzima ayalisababisha vifo vya watu kumi na mamia kujeruhiwa mpaka sasa. Wavenezuela duniani kote wanaopinga serikali yao wameandaa mikusanyiko ya amani kupaza sauti zao na kuzifanya serikali za nchi wanazoishi kuelewa mwenendo wa mambo. Mexico haija nyuma.
Raia wa Venezuela wanaoishi Mexico wametumia mitando ya kijamii kuandaa maandamano Februari 16. Baada ya kukutana kwenye sanamu ya Simon Bolivar (Baba wa taifa la Venezuela) iliyoko kwenye eneo la Polanco, waandamanaji walitembea kupitia kwenye mtaa wa Reforma wakielekea mahali panapoitwa Malaika wa Uhuru. Hapo, wakiungwa mkono na baadhi ya wananchi wa Mexico, Wavenezuela hao walidai uhuru wa habari wakati huu ambapo vyombo vya habari vimezuiwa kutangaza habari na kuimba wimbo wa “uhuru”, “amani” na “hatutaki vifo zaidi”, kisha wakaimba wimbo wa taifa wa Venezuela kama inavyoonekana kwenye video ifuatayo [es]:
Baada ya maandamano haya, Wavenezuela waliandaa mkesha mbele ya jengo la makao makuu ya Umoja wa Mataifa ya Marekani (OAS) jijini Mexico tarehe 18 Februari.
Wakipepea vitambaa vyeupe na kukeba mishumaa, Wavenezuela hao walifanya maombi kwa ajili ya wanafunzi waliouawa tarehe 12 Februari. “Huu ni ujumbe wangu kwa Venezuela: Hamko peke yenu”, alisikika mwanamke mmoja kwenye mkesha huo.