· Novemba, 2009

Habari kutoka Muhtasari wa Habari kutoka Novemba, 2009

Azerbaijan: Bikra

  4 Novemba 2009

Mwanablogu wa Emotions on Air, Mind Mute anatafakari marajio ya jamii kwamba wanawake watabakia mabikira mpaka watakapofunga ndoa. Japokuwa ipo nchini Azerbaijan, blogu hiyo inabaini mfumo unaofanana wa maadili katika eneo lote la Caucasus na inaongelea kuhusu dhana na taratibu za namna hiyo za mfumo dume.

Pakistani: Katika Vita

  4 Novemba 2009

Mohammad Malick anatoa maoni juu ya shambulizi la kigaidi la hivi karibuni kwenye soko la watu wa tabaka chini na la kati huko Peshawar: “limeonyesha kuwa hii ni vita ambyo magaidi wanasimama upande mmoja wa mstari wa damu, na sisi wananchi upande mwingine.”

Kuhusu habari zetu za Muhtasari wa Habari

Hizi ni habari mpya zilizoandikwa kwa muhtasari.