· Novemba, 2009

Habari kutoka Muhtasari wa Habari kutoka Novemba, 2009

Cuba: Ukweli wa Sanchez Kutiwa Mbaroni Waibuka

  8 Novemba 2009

Kukamatwa, kupigwa na kuachiwa huru kulikofuata kwa wanablogu Yoaní Sánchez, Claudia Cadelo na Orlando Luis Pardo kulikofanywa na majeshi ya usalama ya Cuba tarehe 6 Novemba, kunapata matangazo mengi katika vyombo vikubwa vya habari na katika ulimwwengu wa blogu pamoja na ule wa Twita. Yoani ameandika (es) kuhusu tukio hilo...

Yoani Sanchez Pamoja na Wanablogu Wengine wa Cuba Wakamatwa na Kupigwa

  8 Novemba 2009

Jioni ya tarehe 6 Novemba, blogu ya Babalú iliweka kiungo kuelekea makala iliyoandikwa na Penultimos Dias (es) ilitoa taarifa kuwa baadhi ya wanablogu mashuhuri wa Cuba, wakiwemo Yoaní Sánchez na mchangiaji wa Global Voices Claudia Cadelo, walitiwa mbaroni na majeshi ya usalama. Habari mpya kutoka kwa Penultimos Días zinataarifu kuwa...

Ghana: Vionjo Sehemu ya Kwanza

Sehemu ya kwanza ya vionjo vya Ghana iliyotayarishwa na Gayle: Nchini Ghana, kila kanda ina kitu cha kutoa. Utamaduni, historia, pwani, wanyama na mimea, unaweza ukavivinjari nchini kote, kutokea kwenye mitisitu ya kitropiki kule kusini mpaka mbuga za savana za kaskazini. kama ni mpenzi wa pwani au historia, utaburudika na...

Afrika: Chungu cha Kuiyeyusha Afrika

Marvin anaandika kuhusu Afripot, tovuti ya habari inayotilia makini habari za Afrika: “Hivi sasa anatambulisha chungu cha kuyeyushia Afrika – Afripot. Tayari nimo ndani ninayeyuka na ninatumaini kukuona pale na wewe pia kwani mazungumzo kuhusu Afrika na Waafrika yanachukua kasi na kupamba moto. Ni nani ajuaye, inaweza kutengeneza joto la...

Kuhusu habari zetu za Muhtasari wa Habari

Hizi ni habari mpya zilizoandikwa kwa muhtasari.