Habari kuhusu Uhuru wa Kujieleza kutoka Disemba, 2009
Global Voices Yaingia Ubia na Google Katika Tuzo ya Uhuru wa Kujieleza
Mapendekezo kwa ajili ya Tuzo ya Kuvunja Mipaka yatafunguliwa leo (Disemba 29, 2009), hii ni tuzo mpya aliyoundwa na Google pamoja na Global Voices ili kuienzi miradi ya kwenye mtandao wa intaneti iliyoanzishwa na watu au vikundi ambavyo vinaonyesha ujasiri, ari na uwezo katika kutumia intaneti ili kukuza uhuru wa kujieleza.
Malaysia: Mtetezi wa Uhuru wa Vyombo vya Habari Amshtaki Mwanablogu
Mwanahabari-mwanablogu mkongwe anashtakiwa katika kesi ya madai na mwanasiasa anayejulikana kwa kutetea uhuru wa habari nchini Malaysia. Angalia maoni ya wanablogu wa Malaysia.
Morocco: Mwanablogu Mwingine Atupwa Gerezani
Mnamo tarehe 14 Desemba, siku ya Jumatatu, mwanablogu Bashir Hazzam na mmiliki wa mgahawa wa Intaneti Abdullah Boukhou walihukumiwa kifungo cha miezi minne jela kwa huyo wa kwanza na mwaka mmoja kwa huyo wa pili pamoja na kulipa faini ya MAD 500 (sawa na dola za Marekani 63) kila mmoja katika mahakama ya Goulmim.
Misri: Makao Makuu ya Kuzimu Duniani
Wanablogu na wanaharakati wengi wa Kimisri wamekuwa wakikamatwa na Usalama wa Taifa katika nyakati tafauti kwa sababu mbalimbali –za kweli au za bandia –Wa7da Masreya aliwahoji wanablogu mbalimbali na kuweka makala ya kina kuhusu mbinu za utesaji na hila za kisaikolojia ambazo wanablogu wale wamekuwa wakikumbana nazo kwenye makao makuu ya Usalama wa Taifa katika wilaya ya Jiji la Nasr.
Tunisia: Mwanafunzi Atupwa Gerezani kwa Kuhojiwa na Chombo cha Habari
Wanaharakati nchini Tunisia wamezindua ukurasa wa Facebook na blogu ili kumuunga mkono Mohamed Soudani, 24, aliyetoweka mnamo tarehe 22 Oktoba 2009 nchini humo mara baada ya kufanya mahojiano na Redio Monte Carlo International na vilevile Redio France International. Tangia hapo marafiki walipata fununu kwamba alikamatwa na kutupwa korokoroni na kuteswa vibaya.
Iran: Maandano ya Siku ya Mwanafunzi kwenye YouTube
Maelfu ya waandamanaji hawakuujali utawala wa Kiislamu leo kwa kuandamana wakati wa siku ya mwanafunzi, wakiimba kaulimbiu dhidi ya Ali Khamenei, kiongozi wa Jamuhuri ya Kiislamu, na wakipinga sera ya mambo ya nje ya serikali.
Brazil: Wito wa Kugomea Gazeti Linaloongoza Nchini
Wanablogu wa Brazili wamekuwa wakihamasisha mgomo dhidi ya kile walichokiita Coupist Press Party, yaani Sherehe ya Chombo cha Habari ya Kutaka Kupindua Serikali, kwa hiyo wamekuwa wakiwataka watu kuacha kununua, kusoma au kutoa maoni na badala yake kufuta usajili wao kutoka kwenye gazeti la Folha de São Paulo na tovuti yake.
Twita Kutoka Beirut: Siku ya Pili ya Warsha ya Wanablogu wa Uarabuni
Siku ya pili ya Warsha ya Wanablogu wa Kiarabu ilianza na mada inayohusu Mtandao wa Herdict, tovuti inayotumia vyanzo vya watumiaji kukusanya taarifa za uchujaji wa habari kwenye intaneti kutoka...
Warsha ya Wanablogu wa Uarabuni: Tafakuri ya Twita kwa Siku ya Kwanza
Wakati siku ya kwanza ya Warsha ya Pili ya Mwaka ya Wanablogu wa Uarabuni ikifungwa, tutaangalia tafakuri za washiriki kwa siku nzima, kujua wamejifunza nini na namna wanavyojisikia. Siku ilianza...
Indonesia: Sarafu za Kudai Haki
Raia wa mtandaoni (Netizens) wamezindua kampeni ya kukusanya fedha zilizo katika muundo wa sarafu ili kumuunga mkono Prita Mulyasari, mama wa nyumbani raia wa Indonesia aliyeandika malalamiko yake mtandaoni dhidi ya hospitali iliyotoa huduma mbaya, na ambaye alipatikana na hatia na mahakama moja ya kosa la "kuchafua jina" la hospitali hiyo binafsi.