Habari kuhusu Uhuru wa Kujieleza kutoka Mei, 2009
Sri Lanka: Wanablogu Watathmini Kifo cha Kiongozi wa LTTE
Serikali ya Sri Lanka imetangaza kwa kupitia vyombo vya habari vya taifa pamoja na ujumbe wa simu za mkononi mchana leo (Jumatatu, 18 Mei, 2009) kwamba kiongozi wa Kundi linalotaka kujitenga la Wa-Tamil, the Liberation Tigers of Tamil Eelam (LTTE), Vellupillai Prabhakaran, amefariki. Salamu za rambirambi zinaashiria kwamba alikuwa shujaa kwa baadhi ya watu kadhalika wengine walimchukulia kama muuaji katili. Wanablogu wa Ki-Sri Lanka wanatathmini urithi wa kiongozi huyu wa vita na maana ya kifo chake kwa mustakabali wa Watamil na watu wa Sri Lanka.