Habari kuhusu Uhuru wa Kujieleza kutoka Julai, 2010
Lebanoni: Utawala wa Dinosauri
Punde baada ya matukio ya unyanyasaji ya hivi karibuni nchini Lebanon, Msemo wa “Utawala wa Dinosauri” ulianza kutumika na wanaharakati wa mtandaoni kwenye kampeni dhidi ya uvamizi wa namna hii katika mitandao yao. Mwanablogu wa Lebanon Tony anaeleza maana ya msemo huo.
Asia ya Kusini Mashariki : Ngono na Udhibiti wa Mtandao
Uratibu wa maudhui katika intaneti unaonekana kana kwamba ni kinyume na demokrasia lakini serikali za Kusini Mashariki mwa Asia zinaweza kuhalalisha kitendo hicho kwa kuzusha haja ya kuwaokoa vijana kutoka kwenye janga la tabia za ngono holela.
Ivory Coast: Mwanablogu na Mwandishi wa Habari Théophile Kouamouo Akamatwa Pamoja na Timu Yake Tangu Julai 13
Waandishi wa habari watatu wa Le Nouveau Courrier d'Abidjan walitiwa mbaroni na polisi baada ya kukataa kueleza vyanzo vya habari vya uandishi wao wa kipelelezi kuhusu biashara ya usafirishaji kahawa na kakao kwenda nje ya nchi. Yafuatayo ni maoni kutoka kwa raia na vyombo vya habari nchini Ivory Coast huku wenzao watatu wakiendelea kupigania kuachiwa kwa wanahabari hao.
China: Kashfa ya Wizi wa Kitaaluma Uliofanywa na Wang Hui, Mtazamo wa Kimataifa
Kuna kashfa ya wizi wa kitaaluma iliyoibuka mwezi Machi katika duru za kitaaluma za Kichina pale Profesa wa Fasihi wa Chuo Kikuu cha Nanjing, Wang Binbin, alipotuhumu kwamba kazi ya...