Habari kuhusu Uhuru wa Kujieleza kutoka Juni, 2013
Israeli: Waandamanaji Wakumbana na Ukatili wa Polisi Jijini Yerusalemu
Maandamano yaliyoandaliwa na vikundi vitatu vinavyohusiana na Vuguvugu la Israel la haki ya kijamii (#j14) yalifanyika jijini Yerusalemu mnamo Jumamosi usiku (Juni 8). Waandamanaji walidai kubatilishwa kwa uamuzi wa kuuza zaidi kiasi kikubwa cha hifadhi ya gesi wakati ni asilimia 12.5 tu ya mapato hayo yatakwenda serikalini kama kodi.
Misri: Wafanyakazi wa Asasi Zisizo za Kiserikali Nchini Misri Wafungwa Jela
Kuhukumiwa kwa wafanyakazi wa ki-Misri na kigeni wanaofanya kazi katika asasi zisizo za kiserikali (NGO) kifungo cha hadi miaka mitano jela, kumesababisha hasira katika mitandao ya kijamii na katika maeneo mengine. Hatua hiyo imeonekana kama onyo kwa mashirika ya kutetea haki za binadamu na yale yanayokuza demokrasia.
Kukamatwa kwa Mwandishi wa Habari wa Kimasedonia Kwachochea Maandamano
Waandishi wa habari wa Kimasedonia walikusanyika [tazama video na soma nakala] mbele ya Mahakama ya Makosa ya Jinai hivi leo katika mji mkuu Skopje kupinga kukamatwa kwa mwenzao, Tomislav Kezarovski, kwa mujibu wa...
Ukatili wa Polisi Nchini Macedonia: Miaka Miwili Baadae
Siku ya Alhamisi, Juni 6, katika kituo cha Skopje, Vuguvugu la Kupinga Ukatili wa Polisi litatimiza miaka miwili baada ya mauaji ya Martin Neshkovski, ambayo yalisababisha maandamano makubwa katika ngazi za...
Uganda: Hatimaye Magazeti Yaliyofungiwa na Polisi Yafunguliwa
Uganda imeruhusu magazeti mawili kufunguliwa tena baada ya msuguano uliodumu kwa siku 11 kati ya serikali na vyombo vya habari juu ya barua yenye waliyoipata ambayo iliyoonyesha njama ya kumtayarisha mtoto wa kwanza wa Rais Yoweri Museveni kumrithi kiongozi huyo aliyedumu kwa miaka 27.
Tunisia: Mwanaharakati wa FEMEN Akabiliwa na Mashtaka Mapya
Wakati mwanaharakati wa FEMEN raia wa Tunisia Amina Tyler akitarajiwa kupanda kizimbani kusomewa mashitaka mapya mnamo Juni 5, chama cha Upinzani kimekosolewa kwa kukaa kimya na kushindwa kumwunga mkono binti huyo