Israeli: Waandamanaji Wakumbana na Ukatili wa Polisi Jijini Yerusalemu

Maandamano yaliyoandaliwa na vikundi vitatu vinavyohusiana na Vuguvugu la Israel la haki ya kijamii (#j14) yalifanyika jijini Yerusalemu mnamo Jumamosi usiku (Juni 8). Waandamanaji walidai kubatilishwa kwa uamuzi wa kuuza zaidi kiasi kikubwa cha hifadhi ya gesi wakati ni asilimia 12.5 tu ya mapato hayo yatakwenda serikalini kama kodi. Waandamanaji pia walionyesha upinzani wao dhidi ya bajeti ya serikali mpya, ambayo inatarajiwa kwa kiasi kikubwa kuongeza kodi kwa wa-Israeli wa tabaka la chini na la kati, na wakati huo huo ikikata huduma za serikali ambazo matabaka hayo hutegemea. Maandamano hayo, licha ya kuwa na amani na kuwa na madogo (yakiwa na mamia kadhaa tu ya waandamanaji) yalikumbana na kiwango cha juu kabisa cha ukatili wa polisi usio wa kawaida.

Mwanaharakati wa mrengo wa kushoto Ben Marmara alitwiti mfululizo wakati wote wa maandamano:

שוטרים מכים נשים בירושלים, יש לכלוא את השוטרים
שוטרים היכו מפגינה וכעת עצרו אותה. #J14
שוטרים ממשיכים לעצור בני אדם ולהעמיס אותם על טנדרים. #J14 יש כבר כמה וכמה עצורות ועצורים בירושלים.
כמו בהפגנה ברמת גן גם היום המשטרה עברה על החוק ומנעה בכוח קיום של הפגנה. אח”כ עצרו מפגינים ומפגינות

Polisi wanawapiga wanawake, wanapaswa kufungwa jela.Kuna idadi ya wafungwa wa kike na wa kiume mjini Yerusalemu. Polisi wanaendelea kuwakamata watu na kuwajaza katika magari yao yapolisi.
Kama yalivyokuwa maandamano ya Ramat Gan [kupinga hatua ya kuuza gesi ya asili], kwa mara nyingine tena, polisi walivunja sheria na kutumia nguvu kuzuia maandamano. Kisha wakawatia mbaroni waandamanaji.

Mwanaharakati wa #j14 anayeishi Yerusalemu, Yishai Oltchik, alibandika andiko hili kwenye mtandao wa Facebook:

:

אז היום אני יכול לציין את הפעם הראשונה שבה שוטר דפק לי בעיטה. תקף אותי, זאת אומרת.

למה? פשוט כי עמדתי עם שלט הפגנה שקורא לקיום דיון בכנסת בנושא ייצוא הגז. לא דיברתי עם השוטר, לא עמדתי קרוב אל השוטר, אפילו לא הראתי סימנים שאני לא מתכוון לשתף פעולה אם הוא יבקש ממני לזוז. אפילו לא הסתכלתי אליו באופן ישיר. אפילו לא צילמתי, שזה דבר שמותר לעשות אבל בדרך כלל מסתיים בתקיפה.
פשוט עמדתי במקום, ואז הוא הגיע, דחף בעוצמה את הבחורה שהחזיקה איתי את השלט (והעיף אותה על גבה), ועל הדרך בעט בי.

איך הגבתי? קראתי אליו בהפתעה “למה?” ואחרי שניה הרמתי ידיים באוויר (שלא יגיד שאני תוקף אותו) וצעקתי שהשוטר תוקף אותי. הוא כנראה החליט שזה מספיק ועזב אותי לנפשי.
הלכתי לקצין המשטרה הקרוב ואמרתי לו ששוטר בעט בי ללא סיבה; הוא חייך והמשיך ללכת.

ומכל מה שהיה שם, הכאב של הבעיטה, הזעם והעלבון על כך שהותקפתי ללא סיבה (ומי שמכיר אותי יודע שאני לא אדם אלים), מה שהכי מכעיס אותי זו הידיעה שזה לא משהו מיוחד. זה לא יוצא דופן.
פשוט הגיע תורי הפעם, ועוד יש לי מזל שהשוטר הסתפק רק בבעיטה אחת — כי בדרך כלל זה לא נפסק אחרי מכה אחת בודדת.
ראיתי עוד לפחות עוד עשרה אנשים נדחפים בעוצמה ו/או חוטפים מכות ‘בקטנה’ משוטרים, ועוד מעצר אלים אחד או שניים שיצא לי לראות.

Kwa hiyo leo naweza kuweka kumbukumbuku kwa mara ya kwanza kwa askari kunipiga mateke. Alinishambulia, Namaanisha. Kwa nini? Kwa sababu tu mimi nilisimama na bango la kutoa wito kwa Knesset [Israel Bunge] kusikiliza zaidi maoni ya watu kuhusu kuuzwa kwa gesi asilia nje ya nchi… Mimi sikuzungumza na askari … na sikumwangalia  moja kwa moja. Sikuweza hata kumpiga picha ya video, kitu ambacho hata hivyo si kosa kisheria lakini kwa kawaida huishia kwa kushambuliwa [na polisi]. Mimi nilisimama tu pale na kisha yeye akaja, akamsukuma kwa nguvu  msichana aliyeshika bango na mimi (akamsukuma aangukie mgongo), na akifanya hayo, alinipiga mateke na mimi …. Nilikwenda kwa afisa wa polisi aliyekuwa karibu na kumwambia kwamba askari amenipiga teke bila sababu; polisi akatabasamu tu akiendelea kutembea.

Kitu ambacho kinanifanya kuwa na hasira ni kujua kwamba hili silo jambo lisilo la kawaida. Ni kwamba tu ilikuwa nafasi yangu wakati huu, na mimi nilikuwa na bahati kwamba polisi walidhani kwamba teke moja lilitosha – kwa sababu kwa kawaida hayaishi baada ya pigo moja. Nilioona si chini ya watu wengine 10 wakisukumwa na kupigwa mateke na polisi, na mmoja au wawili wakikamatwa vurugu.

Mwanaharakati  wa Tel Aviv wa #j14 Orly Bar-Law alibandika picha hii kwenye mtandao wa Facebook na akaandika:

Right to left: "Bibi [nickname for Netanyahu] - stop the economic terrorism!  Orly with a sign in the center: "Export of gas = suicide for the state" and "No to the cut in child stipends" [one of the proposed austerity measures that will greatly harm the lower class]

Kulia hadi kushoto: “Bibi [Jina la utani la Netanyahu] – Zuia ugaidi wa kiuchumi!
Orly katikati: “Uuzaji wa gesi nje = kujiua kwa serikali” na “Tunapinga kukatwa kwa mafao ya mtoto” [moja ya hatua za kubana matumizi zinazopendekezwa zitakazowadhuru sana watu wa tabaka la chini]

מאות אזרחים נורמטיביים, שוחרי שלום, לא אלימים ומודאגים שבאו למחות על הגזירות הכלכליות, המצב הכלכלי וכנגד ייצוא הגז, נתקלו היום בירושלים בהתנהלות משטרית אלימה וקשה, חסרת כל פרופורציה.
פרשים??? להכות נשים??? מפגין שנדרס על ידי שוטר על אופנוע???
מה נסגר אתכם?
מי נתן את ההוראה לעצור את ההפגנה באלימות ולדכא את זכות המחאה? מי נתן את ההוראה למנוע מצעדת מחאה דמוקרטית להגיע לביתו של ראש הממשלה?
מי אחראי לטירוף הזה?

Mamia ya raia wanaouguswa na hatua za kubana matumizi zinazopangwa kuchukuliwa na serikali wenye kutii sheria bila vurugu, walioamua kupinga mpango huo pamoja na hali mbaya ya kiuchumi na hatua za kuuza gesi nje walikumbana na hatua mbaya za vurugu zisizolingana zilizofanywa na polisi. Polisi kupanda farasi?? Wakiwapiga wanawake?? Mwandamanaji ambaye alikanyagwa na kupitiwa juu yake na askari anayeendesha pikipiki?? Mna shida gani nyie watu?
Ni nani aliyewapa amri ya kuzuia haya maandamano kwa ukatili na kukandamiza haki ya kuandamana? Ni nani mbaye alitoa amri ili kuzuia mkutano wa hadhara wa kidemokrasia kutofikia nyumba ya Waziri Mkuu? Ni nani aanayehusika na ukichaa huu?

Andrea Radu alipandika tena andiko la Orly na kuongeza:

בדמוקרטיה היחידה במזרח התיכון מכים דורסים ועוצרים מפגינים שלוים כי ניסו לממש את זכותם הדמוקרטית להפגין #J14 #1984

Katika nchi pekee ya kidemokrasia katika eneo la Mashariki ya Kati, waandamanaji wa amani wanakanyagwa, wanapigwa na kukamatwa kwa sababu walijaribu kutumia haki yao ya kidemokrasia ya kuandamana.

Policemen riding horses surround #j14 protesters near the Prime Minister's residence in Jerusalem Photo: #j14 activist Gali Fialkow

Polisi wanaoendesha farasi wakiwazingira waandamanaji wa #j14 karibu na makaazi ya Waziri Mkuu jijini Yerusalemu
Picha: Mwanaharakati wa #j14 Gali Fialkow

Maandamano na ukatili wa polisi hayakugonga vichwa vya habari za vyombo vya habari vya Israel na wanaharakati walilalamikia habari kutangazwa kiupendeleo. Naminag ambaye alikuwa katika maandamano alitwiti:

בטמקא אומרים שאתמול השוטרים השתמשו ‘בכוח סביר’. וואללה, כי אני ראיתי מפגינה שהוטחה על גרם מדרגות והתגלגלה בהן למטה, שוטר שדרס מפגין עם האופנוע שלו ושוטר שנגח במפגין עם קסדה. וכל זה עוד לפני שצעדנו 100 מ’. #j14

Ynet [tovuti kubwa ya habari nchini Israel, inayomilikiwa na Yedhioth Aharonot, mwenye uhusiano wa karibu na Waziri wa Fedha, Yair Lapid] anasema kwamba polisi wa walimumia “nguvu sawia”. Kweli? Sababu niliona mwandamanaji akisukumwa chini ya ngazi kadhaa na kubingirita chini, polisi aliyemkanyaga mwandamanaji kwa pikipiki yake na polisi ambaye alikuwa amevaa kofia aliyempiga kichwa mwandamanaji. Na yote haya yalifanyika kabla hata ya kutembea mita 100.

Kwenye mtandao wa Facebook, mtumiaji anayejulikana mara nyingi kama ”mwanasheria wa #j14″, Baraka Cohen, anaweka video hii kuonyesha polisi akimburuta mwandamanaji atoke kwenye maandamano:

Anaweka video nyingine kwenye  mtandao wa YouTube kuonyesha polisi akimkamata kwa  kusimama tu kwenye upande wa kutembelea:

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.