Misri: Wafanyakazi wa Asasi Zisizo za Kiserikali Nchini Misri Wafungwa Jela

Kuhukumiwa kwa wafanyakazi 43 wa Misri na kigeni katika mashirika yasiyo ya kiserikali [NGOs] na kifungo jela cha hadi miaka mitano, kumeibua hasira kwenye mitandao ya kijamii – na sehemu nyinginezo. Hatua hiyo inaonekana kama onyo kwa mashirika yanayotetea haki za binadamu, na yale yanayokuza demokrasia.

Mwanablogu wa Misri Zeinobia anaelezea:

Inasikitisha mno kwa sababu mashirika haya yamekuwa na nafasi muhimu sana nchini Misri linakuja suala la maendeleo na misaada ya wafadhili ilichangia sana katika hili. Cha kusikitisha zaidi ni jinsi wafanyakazi wa mashirika haya wanavyoadhibiwa namna hii.
Wanawake na wanaume hao wa ki-Misri, hawataweza kupata kazi kirahisi nchini Misri wanapokuwa na hatia katika kesi ya kisiasa kama hii.
Bila shaka ulimwengu hauna ujinga, unaelewa nini kilichotokea na kinachoendelea.
Lazima tufahamu kwamba hii ilikuwa ni hila ya utawala wa zamani wa Mubarak, kuyaacha mashirika hayo yafanye kazi zake bila leseni ili kuweza kuyafunga wakati wowote yanapovuka mstari. Imeshawahi kutokea awali kwa vituo vya televisheni kama Orbit, Dream TV na Al Jazeera Mubshar Misr.
Kwa kweli ni sahihi kusema chama cha Muslim Brotherhood kinafuata nyayo za serikali ya Mubarak na SCAF.
Hiki ni kikwazo kingine kwa haki za binadamu nchini Misri na kwa kweli hakitahamasisha watu kuja nchini au kuwekeza. Naamini uamuzi huu utakuwa kikwazo katika uhusiano kati ya Marekani na chama cha Muslim Brotherhood na pia kati ya Umoja wa Ulaya na Muslim Brotherhood.

Kwenye mtandao wa Twita, raia wa mtandaoni walipokea habari hizi kwa mshtuko.

Sally Sami alitwiti:

@Salamander: Kwa mshtuko mkubwa juu ya uamuzi #kesiyaNGO!! Hakuna mtu anastahili kufungwa kwa kufanya kazi na NGO …

Lina El Wardani alitoa maoni:

@linawardani: Nimestushwa una kuogopeshwa sana na uamuzi wa #kesiyaNGO watu 11 kuhukumiwa mwaka 1, wengine watano miaka miwili, 27 miaka 5, na kama vile haitoshi mashirika manne yakifungwa

Bel Trew alitoa maelezo:

@Beltrew: #Kesi za mashirika haya zilioongozwa na waziri wa enzi za utawala wa Mubarak chini ya utawala #SCAF, ni watu walikuwa wanashitakiwa na sio mashirika kwa kile kinachoitwa kutosajiliwa

And Mona Eltahawy anaongezea:

@monaeltahawy: “Haki” nchini #Misri: kifungo jela kwa washitakiwa katika mashitaka ya mashirika yasiyo ya kiserikali yaliyosukumwa na mambo ya siasa, wakati vigogo wa utawala huo pamoja na polisi wakionekana hawana hatia kwa kuwaua waandamanaji

Ghada Shahbender analalamika[ar]:

المآساة الحقيقية انه ٩٩٪ من المصريين حيتقبلوا الحكم بالسجن على موظفين المنظمات الغير حكومية و يفرحوا بتحجيم ‘التدخل الاجنبى’ اللى بيروج

@ghadasha: Janga halisi ni kwamba asilimia 99 ya Wamisri watakubali uamuzi [wa mahakama] kuwafunga jela wafanyakazi  wa mashirika hayo na kuwa na furaha kwa kuzuia nchi hiyo “kuingiliwa na mataifa ya nje”, jambo ambalo ndilo linachukuliwa kuwa sababu kwa sasa.

نظام مبارك و المجلس العسكرى و الاخوان – اللى بيتلقوا معونة دولية و بيشحذوا من المجتمع الدولى – روجوا لفكرة ‘التدخل الاجنبى’ و استغلوها للقمع

@ghadasha:… utawala wa Mubarak, Baraza Kuu la kijeshi [SCAF] na Muslim Brotherhood – ambao wote hupata misaada ya wafadhili na huomba omba kwa jumuiya ya kimataifa. Wao ndio wanatangaza dhana ya “kuingiliwa na wageni” na kuitumia vibaya kukandamizaji [mashirika haya]

Mmoja wa watuhumiwa, Robert Becker, ambaye alihukumiwa miaka miwili na alikuwa mshatika wa pekee wa kigeni kubaki nchini Misri wakati wa kesi, alisema alilazimishwa kwenda “uhamishoni” baada ya uamuzi kutangazwa. Alitwiti:

@rbecker51: Niko salama nje ya #Misri. Kwa ushauri wa wanasheria wangu, nimelazimika kuikimbia nchi bila kutaka na kwa kweli nikiwa na hasira mpaka rufaa itakapotatuliwa.

Katika twiti mbili za awali, anaelezea:

@rbecker51: Asanteni nyote kwa maneno mazuri. Naipitia kuona uwezekano wa kisheria/rufaa kwa msaada wa wanasheria wangu

@rbecker51: Ninasisitiza sina hatia kwenye mashitaka haya ya kuanzisha NGO [asasi isiyo ya kiserikali] miaka sita kabla ya mimi kuwasili nchini Misri na kwa sasa ninasubiri mipango ya rufaa yangu

Sally Sami anahitimisha [ar]:

فعلا داخلين على أيام سوداء لما ناس يتحكم عليها بالسجن لمجرد أنهم اشتغلوا في منظمات غير حكومية …

@Salamander: Kweli tunaingia kwenye siku za giza.. wakati ambao watu wanafungwa jela kwa ajili tu ya kufanya kazi katika mashirika yasiyo ya kiserikali

Kwa miitikio zaidi, angalia alama habari #ngocrackdown na #ngotrial.

Kwa mujibu wa taarifa za habari na akaunti zao wenyewe za mtandao wa Twita, washitakiwa  watakata rufaa kupinga hukumu hiyo.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.