makala mpya zaidi zilizoandikwa na Mghosya kutoka Julai, 2014
Namna ya Kuwa Baba Mwema
Raia wa Panama Joel Silva Díaz anafafanua kile ambacho kinawashangaza watu wengi, hususani wanaume: namna ya kuwa baba mwema. Kwenye blogu yake anaeleza changamoto alizokutana nazo na baba yake mwenyewe na kuhusianisha na malengo yake kama baba: …Recuerdo que veía como un juego el buscar un tema de conversación, debido...
Dunia Yasimama na Palestina: Maandamano Yafanyika Kila Bara
maandamano yamelipuka katika miji mbalimbali duniani kote kuwaunga mkono wa-Palestina na kutoa wito wa kumalizwa kwa mapigano. Hapa ni picha chache za maandamano hayo.
Dondoo 13 za Kulinda Taarifa zako Kwenye Kompyuta Zinazotumiwa na Watu Wengi
Kama uko mbioni kwenda kwenye mapumziko na unafikiri kuchukua kompyuta yako na kuiunganisha na mtandao wa intaneti wa Siwaya (Wi-Fi) au kutumia kompyuta ambazo zinapatikana kwenye hoteli au kwenye eneo lolote la umma, unahitaji kusoma makala hii yenye dondoo 13 za kulinda taarifa zako, kama ilivyochapishwa na Andrea kwenye blogu...
Trinidad & Tobago: Je, Kuishi kwenye Enzi za Kidijitali Kunahatarisha Haki yako ya Faragha??
Blogu ya ICT Pulse inapitia taarifa iliyochapishwa hivi karibuni iliyoandaliwa na Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu juu ya haki ya faragha katika enzi hizi za dijitali.
Wanablogu wa Zone 9 Washitakiwa kwa Ugaidi Nchini Ethiopia
Wanablogu tisa na waandishi, wanne wao wakiwa wanachama wa Global Voices, wamekana mashitaka yao na wanajiandaa kwa utetezi kesi itakaposikilizw atena Agosti 8.
Televisheni ya Taifa Urusi Yahariri Wikipedia Kuibebesha Ukraine Lawama kwa Kuanguka MH17
Mtu mmoja wa televisheni ya Taifa Urus, VGTRK, amehariri makala ya kamusi elezo ya Wikipedia kuhusu kuanguka kwa ndege ya Malaysia MH17 ili kuibebesha Kyiv lawama.
Mvua ya Moto Inanyesha Gaza: Israeli Yaanza Shambulio la Ardhini
Wa-Palestina wanasema mvua ya moto inanyesha Gaza, baada ya Israeli kuanza operesheni ya ardhini kwenye ukanda wa Gaza usiku huu
Israel Yaanza Operesheni ya Ardhini Gaza
Vikosi vya kijeshi vya Israeli vimeanza kuingia Gaza, baada ya siku kumi za mapigano yaliyogharimu maisha ya wa-Palestina 200. Hatua hiyo inafuatia Hamas kukataa pendekezo la kusitisha mapigano lililotolewa na Misri.
Je, Ujumbe wa Shirika la Ndege la Singapore Baada ya Ndege MH17 Kuanguka Haukuwa wa Kiugwana??
Baada ya habari kufahamika kwamba ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia MH17 imeanguka mashariki mwa Ukraine, Shirika la Ndege la Singapore liliweka ujumbe huu kwenye mtandao wa Facebook na Twita: Customers may wish to note that Singapore Airlines flights are not using Ukraine airspace. — Singapore Airlines (@SingaporeAir) July...
Matamshi Matano ya Kushangaza Kufuatia Kuanguka kwa Ndege MH17 Nchini Ukraine
Wakati kukiwa na hisia zinazozidi kuongezeka kufuatia kuanguka kwa ndege nchi Ukraine, matamshi kadhaa yaliyotolewa na watu maarufu Moscow na Donetsk yamevuta hisia za watu