Vikosi vya kijeshi vya Israeli vimeanza kuingia Gaza, baada ya siku 10 za mapigano zilizochukua maisha ya Wapalestina 200. M-Israeli mmoja aliuawa kwa shambulio la roketi kwenye eneo la Palestina. Hatua hiyo inakuja baada ya Hamas, kikundi kinachoitawala Gaza, kukataa pendekezo la kumaliza mapigano lililotolewa na Misri.
Tovah Lazaroff, mwandishi wa Boston aliye katikati ya mgogoro wa Israel na Palestina, anatwiti:
It's official from Israel's PMO office, the IDF has begun to enter Gaza.
— Tovah Lazaroff (@tovahlazaroff) July 17, 2014
Ni rasmi sasa kutoka kwenye ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel, vikosi vya jeshi vimeanza kuingia Gaza
Anaongeza:
PMO: The cabinet approved the ground operation after Israel accepted an Egypt brokered cease fire & Hamas rejected it.
— Tovah Lazaroff (@tovahlazaroff) July 17, 2014
Ofisi ya Waziri Mkuu: Baraza la Mawaziri limeidhinisha operesheni ya ardhini baada ua Israeli kukubaliana na pendekezo la Misri la kusitisha mapigano. Hamas ilikataa mapendekezo hayo
Ardhini huko Gaza, iFalasteen anasema:
Bombs everywhere in Gaza no electricity and very thing is bright from all the fires and bombs…
#GazaUnderAttack
— فلسطين i (@iFalasteen) July 17, 2014
Mabomu kila mahali hapa Gaza, hakuna umeme na kuna mwanga mkali wa milipuko na mabomu…
Nonstop bombing where no where to run… Only Allah will protect you Gaza…
#GazaUnderAttack
#PrayForGaza
— فلسطين i (@iFalasteen) July 17, 2014
Mabomu yanapigwa mfululizo na hakuna pa kukimbilia…Mungu tu atailinda Gaza