makala mpya zaidi zilizoandikwa na Mghosya kutoka Septemba, 2014
Vyombo vya Habari Vyaususia Wimbo wa Kupigania Uhuru Ulioimbwa na Msanii Maarufu Nchini Macedonia
Msanii maarufu wa Macedonia wa miondoko ya kufoka foka amejikuta akipoteza umaarufu baada ya kuachia ‘kibao’ kinachojadili masuala ya uhuru wa habari nchini Macedonia.
Serikali ya Marekani Yadai Takwimu za Shirika la Indymedia Athens
Mnamo Septemba 5, Wizara ya Sheria ya Marekani iliitaka shirika linaloshughulika na masuala ya kuhifadhi tovuti iitwayo May First kutoa taarifa za mmoja wa wateja wake, ambaye ni Kituo cha Ugiriki cha cha Uandishi Huru Athens, kinachofahamika kama Indymedia Athens. Likiwa limeanzishwa mwaka 2005, May First ni shirika lisilo la kibiashara linalojikita...
Filamu Yaonesha Namna Kabila Dogo Linavyojaribu Kuwazuia Wakata Misitu Kuharibu Mazingira
Sunset Over Selungo ni filamu ya dakika 30 inayoonesha namna kabila la wenyeji la Penan linavyopigania kutunzwa kwa misitu ya asili kwenye kisiwa cha Borneo nchini Malaysia. Borneo ni kisiwa kikubwa zaidi barani Asia. Filamu hiyo imetengenezwa na mtayarishaji huru wa filamu wa Kiingereza, Ross Harrison
Kimbia! Waislamu Wanakuja!
Mtazamo wa vyombo vikuu vya habari mara nyingi unaonesha “Waislamu” wenye sura moja kubwa, ambayo haikosi kuwa na ghasia. Kwenye kichekesho hiki kisicho na maana yoyote, Mchekeshaji wa ki-Pakistani Sami Shah anakuletea makundi makuu ya “waislamu”.
Ebola Haijafika Gambia, na Watu Wanashughulika Kuhakikisha Hali Inabaki Kuwa Hivyo
Watu 1,600 wamepoteza maisha tangu kulipuka kwa maradhi ya Ebola. Nchini Gambia, kampeni inaendelea kwenye mitandao ya kijamii pamoja na wimbo maalumu wa kujaribu kuelimisha watu kuhusiana na maradhi hayo
Ushiriki Mkubwa wa Umma katika Mafunzo ya Tetemeko la Ardhi Nchini Mexico
Mnamo Septemba 19, 1985, kwenye maeneo ya kati, Kusini na Magharibi mwa Mexico, hususani kwenye Wilaya ya Shirikisho, yalikumbwa na tetemeko kubwa, linalosemekana kuwa baya zaidi katika historia ya Mexico inayojulikana. Wakikumbuka miaka 29 tangu tukio hilo litokee, Katibu wa Ulinzi wa raia wa Wilaya ya Shirikisho aliandaa mafunzo ya...
Maktaba ya Digitali ya Tiba Asilia Nchini Ufilipino
Ikiwa imeanzishwa na mamlaka kadhaa za kiserikali, Maktaba Dijitali ya Elimu ya Tiba za Jadi Ufilipino (TKDL-Health) inalenga kuweka kumbukumbu na kufanya masuala ya tiba za jadi kuwa za kidijitali nchini humo. Jamii, ambazo nyingi ni zile za miliamni au majirani zao, zimekuwa zikitegemea miti na mazao mengine ya asili...
CPJ Yamtaka Obama Kulinda Haki ya Kutangaza Habari kwenye Enzi za Dijitali
Wakati serikali zaidi duniani zikizidi kuwalenga waandishi wa habari kwa udukuzi, Kamati ya Kuwalinda Waandishi inaitaka Serikali ya Obama kujisafisha
Wanabogu wa Togo Wamtania Rais Kufuatia Ujumbe wa Bango Barabarani
Mtu mmoja alitaka watu wajue kwamba alikuwa na shukrani kwa ukarimu wa Rais wa Togo Faure Gnassingbé. Wiki hii, bango kubwa liliwekwa jijini Lomé, Togo kusifia kitendo cha Rais kutoa chakula cha mchana kwa watoto. Bango hili linaloonekana hapa chini lina maneno haya kwa lugha ya Kifaransa:” Asante sana Baba Faure...
Majadiliano na Picha za Mkutano wa Highway Africa 2014
Mkutano wa Highway Africa 2014 ulifanyika kuanzia tarehe 7-8 Septemba, 2014 kwenye Chuo Kikuu cha Rhodes, Grahamstown, Afrika Kusini. Maudhui ya mkutano huo yalikuwa Mitandao ya Kijamii -kutoka pembezoni kwenda kwenda kwenye vyombo vikuu vy habari. Angalia picha na mzungumzo kuhusiana na mkutano huo hapa.