Vyombo vya Habari Vyaususia Wimbo wa Kupigania Uhuru Ulioimbwa na Msanii Maarufu Nchini Macedonia

A still from Toni Zen's video clip "Under Control."

Picha Mnato kutoka kwenye video ya Toni Zen iitwayo “Under Control.”

Hata sio muda mrefu uliopita, Toni Zen alikuwa nyota mkubwa wa muziki wa kufoka foka nchini Macedonia, akipendwa sana na vyombo vya habari vilivyofuatilia kila alichokifanya. Tangu afyatue kibao chake kinachohusu uhuru wa kujieleza, hata hivyo, Zen anaonekana kubwagwa na vyombo vya habari vya ki -Macedonia.

Mara kadhaa akisifiwa na vyombo vya habari vya nyumbani kwa mwonekano wake nadhifu, akivutia kwa umbo la mwili wake kama lile la mlinzi mkuu wa waziri mkuu [wa zamani] – ambaye alionekana kwenye moja ya video za muziki wa Toni – na alikuwa mtu anayefuatiliwa sana na vyombo vya habari vya nchini hiyo nanchi nyingine wakati aliposhiriki kwenye toleo jingine la kipindi cha runinga cha Survivor, Zen alionekana kwenye kurasa za mbele za kwenye vipindi vya televisheni. Alionekana pia kama nyota wa watoto kwenye vitabu vya watoto , akifanyamatamasha makubwa kwenye kumbi kuu za kwenye jiji la Skopje .

Zen alikuwa alama maarufu ambayo ilikuwa gumzo la vyombo vya habari nchini humo mpaka ilipofika mwezi Machi 2013, ambapo msanii huyo alitoa video ya wimbo wake mpya , aliouita “Tumedhibitiwa” (Under Control), unaonekana hapa. Mwanamuziki huyo tangu wake huo hajaonekana kwenye vyombo vya habari vya Macedonia na maeneo ya jirani, ingawa wimbo wake umekuwa maarufu sana miongoni mwa mashabiki wake.

…Медиумски притисок
со бомбардирање реклами
вака се прави
„Не размислувајте сами!“

Слободата на говорот
затворена во шахта
во канализација
фрлена целата правда

Нè скараа нè степаа
од коренот нè сменија
фаќаат сеири
додека дигаат империја…

…Знам дека не е вака
како што ни зборат
ние не сме вакви
не држат под контрола

Се знае дека
сè е под контрола…

…Shinikisho la vyombo vya habari
Gharika ya matangazo ya biashara
Hivi ndivyo mnavyofanya
“Hamfikiri kwa kujitegemea!”

uhuru wa kujieleza
umefungiwa kwenye kwapa
kama haki
ikienda na maji

wametufanya tusielewane na tugombane sisi wenyewe
wametubadilisha kuanzia kwenye mzizi
na wanachekelea matatizo yetu
wakati wakijenga mahekalu yao…

…najua mambo hayo
si kama wanavyoyasema
hii sio sisi
wanatudhibiti

inajulikana
kila kitu kimedhibitiwa…

Wimbo wa Zen na video yake iliyoandaliwa kwa utadi inarejea moja kwa moja hali tete ya uhuru wa kujieleza na kujengeka kwa matabaka ya kijamii nchini Macedonia, huku sauti na picha vikirejea kazi za mchekeshaji wa Kimarekani George Carlin na mwandishi wa vitabu wa Uingereza George Orwell. Video ya wimbo wake imesifika sana na ilichaguliwa kuwa wimbo bora wa video wa mwaka 2013  na majaji wa maonesho maarufu ya mwaka yanayoitwa Zlatna Buba Mara. Watu wachache wameweza kuuona, hata hivyo, kwa sababu haujapata nafasi kabisa kwenye vyombo vikuu vya habari vya Macedonia. Shughuli za maonesho ya muziki ya msanii huyo zimekuwa zikisua sua na kwa sasa haonekani sana wenye matukio ya hadharani.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.