Global Voices inaungana na mashirika mengine zaidi ya 60 yanayojihusisha na uhuru wa habari kuiunga mkono kampeni ya Kamati ya Kuwalinda Waandishi kwa Haki ya Kutangaza katika Zama za Kidigitali , ikiulenga utawala wa Obama. Kufahamika kwa vitendo vya ufuatiliaji, kutishiwa na kunyonywa kwa tasnia ya habari kumeibua maswali kuhusu haki na usalama wa waandishi katika kutangaza habari katika zama hizi za kidigitali. Kufahamika kwa vitendo hivyo kadhalika inazilipua serikali zinazotafuta kubana zaidi vizuizi vya uandishi pamoja na mtandao wa intaneti.
Ingawa ombi hilo limeelekezwa kwa Obama, waandishi kote duniani wanaathirika, iwe moja kwa moja au kwa namna moja au nyingine. Taarifa kwamba shirika la Usalama wa taifa hilo na mashirika rafiki ya upelelezi yaliwafuatilia waandishi–ikiwa ni pamoja na taarifa kwamba Shirika la Usalama la Marekani (NSA) liliingilia mawasiliano ya Al-Jazeera–zinaleta athari mbaya kwenye vyombo vya habari. Kuvuka mipaka kiasi hicho kumetengeneza hatari kwa waandishi, hasa kwa kuzingatia matumizi ya vifaa vya kielekroniki .
Kufahamika kwa ufuatiliaji mkubwa wa majukwaa ya mtandaoni hivi karibuni nchini Misri naUingereza, kufuatiliwa kwa waandishi wa habari nchini Ethiopia, na kubughudhiwa kwa waandishi na wakosoaji wa serikali duniani kote (mara nyingi kwa mashtaka ya kudaiwa kuihujumu serikali) vyote vinathibitisha ukweli kwamba masuala haya yanayoibuliwa kwenye kampeni ya Haki ya Kutangaza hayana mipaka. Kuanzia Azerbaijan mpaka Zambia, serikali zinawalenga waandishi wa habari kwa kuingilia mawasiliano yao na kwa hakika vitendo hivyo havivumiliki kuachwa kuendelea. Kufahamika kwa vitendo vya Shirika la Usalama wa taifa Marekani, NSA vinaondoa uhalali wa Marekani kujaribu kudai vinginevyo.
“Nchini Pakistan, ambako uhuru wa kujieleza unachukuliwa kwa dhana ya Kimagharibi, kufahamika kwa vitendo vya kipelelezi kulikowezeshwa na Snowden kumeleta athari mbaya,” Sana Saleem, mkurugenzi wa kikundi cha haki za kidigitali nchini Pakistani Bolo Bhi na mwandishi wa Global Voices, aliandika kwenye kwenye makala ya hivi karibuni kwenye blogu aliyoiandika kwa ajili ya CPJ. “Kuanzia kwenye mwonekano wa sera hadi kwenye maelezo yanayotolewa kwa umma kuhusu uhuru wa habari na faragha, kutobolewa siri kulikofanywa na Snowden kumeimarisha hoja za serikali nyingi kueteta vtendo vya udukuzi.”
Hatua ya kwanza kwenye kampeni hii ni kufungua ombi hili la mtandaoni. Kampeni hiyo inadai masuala matatu makuu kutoka kwenye utawala wa Obama:
- Kutoa maelekezo ya kisera kwa mamlaka ya ki-Rais kuzuia udukuzi na kufuatiliwa kwa waandishi na mashirika ya habari.
- Kudhibiti mashitaka yanayosukumwa na uonevu na chuki yanayolenga kuwakomesha waandishi na kuwatisha wakosoaji wa serikali.
- Kuzuia kubughudhiwa kwa waandishi wa habari kwenye mpaka wa Marekani.
Makumi kadhaa ya vyombo vya habari kutoka ikiwa ni pamoja na Associated Press, Huffington Post na Vice News, pamoja na vyama vya waandishi wa habari kama vile Chama cha Waandishi wa habari za uchunguzi Uarabuni na Chama cha Waandishi Weledi [Society of Professional Journalists], na makundi ya kutetea haki za kidunia na kitaifa kama vile Amnesty, Human Rights Watch, na IFEX yanaunga mkono kampeni hiyo.
Waandishi maarufu duniani kote ikiwa ni pamoja na Christiane Amanpour, Arianna Huffington, Xiao Qiang na Ahmed Rashid nao pia wametia saini kuthibitisha wanavyounga mkono kampeni hiyo, pamoja na mamia ya waandishi wengine, wanablogu na wananchi wanaotambua kwamba vitendo vya ufuatiliaji wa mawasiliano na bughudha kwa waandishi vina madhara yanayovuka mipaka ya nchi moja moja.
Unawezaje kuunga mkono Kampeni hiyo ya CPJ ya #RightToReport [Haki ya Kutangaza] kwenye enzi za Dijitali?
- Tia saini wito maalum Haki ya Kutangaza kwenye enzi za Kidijitali
- Washawishi marafiki, wanachama na mtandao wako kutia saini wito huo maalum na unga mkono kampeni ya #RightToReport.
- Sambaza ujumbe wa wito huu maalum kwenye mitandao ya kijamii
- Fuatilia Ukurasa wa Facebook wa Right to Report ili kuendelea kupata taarifa zaidi
- Kama unawakilisha shirika linalotaka kushiriki kampeni hii, tuma nembo yako kwa RightToReport@cpj.org na tutaiongeza kwenye tovuti yetu
Tembelea ukurasa wa kampeni ya Right to Report inayoendeshwa na CPJ ili kujifunza zaidi kuhusu jitihada hizi na kujua namna unavyoweza kushiriki.