makala mpya zaidi zilizoandikwa na Albert Kissima kutoka Novemba, 2012
Mkanganyiko wa Makubaliano ya OIC Kuanzisha Ofisi Nchini Myanmar
Shirika la Ushirikiano wa Kiislam (OIC) limependekeza kuanzisha ofisi nchini Myanmar kwa lengo la kukisaidia kikundi kidogo cha Waislamu nchini humo. Serikali ilishakubaliana na mpango huu lakini ilibadili uamuzi huu mara baada ya kutokea maandamano ya kupinga uamuzi huo katika maeneo mengi ya nchi.
Mwanzilishi wa Kikundi cha Kijeshi Kilichofutwa Nchini Pakistani Ajitolea Kuisaidia Marekani.
Wakati kukiwa na makelele na uharibifu mkubwa huko ukanda wa pwani ya mashariki mwa Marekani unaotokana na kimbunga kikubwa kijulikanacho kwa jina la Sandy, Hafiz Mohammad Saeed, mwanzilishi wa shirika la kijeshi lililofutwa la Lashkar e Taiba (LeT) na kiongozi wa Jaamat ud Dawa (JuD) ajitolea kutoa misaada ya kibinadamu kwa Marekani ili kufidia uharibifu.
Chile: Mahabusu wa Mapuche Wamaliza Mgomo wa Kutokula Uliodumu kwa Siku 60
Baada ya siku 60 za mgomo wa kutokula, mahabusu wanne wa Mapuche wamesitisha mgomo wao mara baada ya Mahakama Kuu ya Chile kukubaliana na baadhi ya madai yao. Juhudi hizi pia zimepelekea kuwepo kwa migowanyiko kiasi kuhusiana na mgogoro miongoni mwa watu wa Chile.
Uharibifu Nchini Syria Katika Picha
Wapiga picha wa Syria wanatumia mitandao ya kijamii kuweka taswira ya uharibifu katika maeneo mbalimbali na kwenye mitaa. Pamoja na ufinyu wa vitendea kazi vya utoaji wa habari, habari zinazotoka Syria zinaonesha hali ya kutisha ya uharibifu inayoikabili nchi ya Syria.