makala mpya zaidi zilizoandikwa na Albert Kissima kutoka Agosti, 2012
Mfumo wa Kipekee wa Kuwapa watoto Majina wa Nchini Myanmar (Burma).
Raia wengi wa Myanmar hawana majina ya ukoo. Je, umewahi kujiuliza wanajaza vipi fomu zinazowadai kujaza majina yao ya mwanzo na ya ukoo, au hata kujiuliza kuwa 'Daw' ina maana gani katika jina la Daw Aung San Suu Kyi? Hapa tutatazama mtindo wa pekee kabisa wa Mynmar wa kutoa majina.
Syria: Mafunzo ya Silaha na Namna ya Kupigana Katika Mtandao wa Intaneti
Waasi nchini Syria wameanza kutumia YouTube ili kupeana mafunzo hasa kupitia 'Free Syrian Army Help' yaani 'Msaada wa Jeshi la Kuikomboa Syria'. Chaneli hiyo ina picha za video zipatazo 80 zikiliezea mbinu kama vile vita ya uso-kwa-uso, jinsi ya kutengeneza mabomu ya kutupwa kwa mkono, na jinsi ya kuwavizia maadui.
Afrika ya Kusini: Yasherehekea Medali ya Kwanza ya Dhahadu Baada ya Miaka 8
Pongezi nyingi zimekuwa zikimimika kwa muogeleaji wa Afrika Kusini Cameron van der Burgh ambaye amechukua medali ya kwanza ya dhahabu baada ya nchi hiyo kupata matokeo mabaya katika mashindano ya Olimpiki ya mwaka 2008 yaliyofanyika jijini Beijing. Amekuwa mwanaume wa kwanza wa Afrika Kusini kushinda medali ya dhahabu katika mashindano ya uogeleaji ya Olympics.