makala mpya zaidi zilizoandikwa na Albert Kissima kutoka Februari, 2017
Mwanablogu wa Algeria Merzoug Touati Anaweza Kutumikia Jela Miaka 25 Kwa Kufanya Mahojiano na Afisa wa Israel Kupitia Mtandao wa You Tube
Mahojiano yake yanahusu tuhuma za serikali ya Algeria kwamba mataifa ya nje yanachochea maandamano ya kupinga hatua iliyochukuliwa na serikali ya kubana matumizi. Mwanablogu Merzoug Touati anakabiliwa na makosa ya "kutoa taarifa za kiintelijensia kwa afisa wa mataifa ya kigeni."
Baada ya Mwanablogu Kuhukumiwa Adhabu ya Kifo, Kesi yake Kusikilizwa na Mahakama Kuu ya Nchini Mauritania
Mwaka 2014, Ould Mkhaitir alikamatwa na kuhukumiwa kwa kosa la "uasi wa dini" kufuatia kuchapisha maoni yake katika makala aliyozungumzia mfumo kandamizi wa kimatabaka wa nchini Mauritania.