I am a Tanzanian, professionally a science Teacher specifically for chemistry and Mathematics. I fluently speak Kiswahili. As a Swahili speaker, its my duty to inform swahili speakers around the Globe with news which are hardly found in other news media but only in Global Voices, “Sauti za Dunia, Ulimwengu unaongea, wasikiliza”.
makala mpya zaidi zilizoandikwa na Albert Kissima kutoka Novemba, 2013
Onesho la Mitindo Nchini Japan na Kauli Mbiu ya Kusitishwa kwa Matumizi ya Nguvu Dhidi ya Wanawake
Umoja wa Wanawake wa Asia, shirika lisilo la kimaslahi linaloshughulika na haki za wanawake linaratibu onesho la mitindo linalobeba ujumbe wa Mtindo wa Kukabiliana na Mfumo Kandamizi kwa lengo la kuvuta hisia za watu kuhusiana na suala la matumizi ya nguvu dhidi ya Wanawake.
Mkusanyiko wa Makala za Kuvuliwa Madaraka kwa Mbunge Maarufu Nchini Tanzania
Ben Taylor aweka mkusanyiko wa makala zinazohusiana na kuvuliwa madaraka kwa Zitto Kabwe,mbunge maarufu na kijana wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Chadema. Zitto: […] alivuliwa nyadhifa zote rasmi na viongozi wakuu wa chama mapema siku ya ijumaa asubuhi. Zitto Kabwe hatakuwa tena Naibu katibu Mkuu wa chama wala...
Sera ya Taarifa ya Uwazi Yahitaji Kuboreshwa zaidi Nchini Japan
Pamoja na kuwa serikali ya Japan inajitahidi kupiga hatua katika uboreshaji wa sera yake ya uwazi, nchi hii bado ina safari ndefu, kwani imeshika nafasi ya 30 kati ya nchi 70, kwa mujibu wa orodha liyoandaliwa na Asasi ya Ujuzi Huru. Masahiko Shoji wa Asasi ya Ujuzi Huru nchini Japani aandika:...
India: Watu Zaidi ya Milioni 60 Wanaugua Ugojwa wa Kisukari
Ikiwa na watu zaidi ya milioni 60 wanaougua ugojwa wa kisukari [pdf] na wengine wanaokadiriwa kufikia milioni 77 walio katika hatihati ya kuugua ugojwa huu, nchi ya India inajikuta katika vita kali ya kukabiliana na janga la ugonjwa wa kisukari. Katika siku ya ugonjwa wa Kisukari Duniani inayoadhimishwa kila tarehe...
Global Voices Yasaidia Wahanga wa Haiyan Nchini Ufilipino
Kimbunga kijulikanacho kama Haiyan hadi sasa kimeshaua maelfu ya watu nchini Ufilipino. Wiki hii tunaongea na waandishi wetu wlioko nchini Ufilipino pamoja na mfanyakazi anayehusika na misaada kujua ni kwa namna gani tunaweza kutoa msaada wetu.
Filamu 14 za Mazingira zenye Kuvutia
TVE (Televisheni inayohusika na Mazingira) yaonesha video 14 bora za washindani waliofika fainali kwenye shindano la kimataifa la filamu bora ya mazingira. Washiriki kutoka sehemu mbalimbali za dunia wametengeneza filamu zinazochukua muda wa dakika 1 kwa kuzingatia mada zinazohusiana na mabadiliko ya hali ya hewa, maendeleo endelevu pamoja na bayoanuai....
Wimbo wa Mahadhi ya Kufoka Upendwao na Vijana nchini Tunisia
Ukiwa umetazamwa zaidi ya mara milioni 3 kwenye mtandao wa YouTube, wimbo wa Houmani umegeuka kuwa wimbo wa taifa kwa vijana wa Tunisia. Afef Abrougui anaeleza kwa nini,
Misri katika Harakati za Kujitafutia Makazi
Ni wapi mtu hujisikia kuwa yupo nyumbani? mwanablogu wa Misri Tarek Shalaby atoa maoni yake: Baadhi ya watu wanasema kuwa nyumbani ni pale palipo na kitanda chake, wengine wanadai kuwa nyumbani ni pale unapoweza kupata mtandao huru wa intaneti. naweza kusema kuwa nyumbani ni pale ambapo mishahara yako imehamishiwa.
Wahamiaji 87 Wafariki kwa Kukosa Maji Kaskazini mwa Niger
Mnamo tarehe 30 0ctoba, watu 87 waliokuwa wakijaribu kuifikia bahari ya Mediterania walifariki mara baada ya madereva waliokuwa wakiendesha magari waliyoyatumia kusafiria kuwatelekeza wahamiaji hao katika Jangwa la Sahara. Wahamiaji hawa walihangaika kutafuta msaada bila ya mafanikio. Simulizi ya kuhuzunisha kutoka kwa mmoja wa watu walionusurika aliyejulikana kwa jina la...
Tamko Kuhusu Mustakabali wa Ushirikiano katika Mtandao wa Intaneti.
Wawakilishi wa mashirika yanayoratibu miundombinu ya kiufundi ya huduma ya intaneti waliokutana huko Montevideo; Uruguay, wametoa tamko kuhusu mustakabali wa ushirikiano katika masuala ya Intaneti [es], ambapo walifanya uchanganuzi kuhusiana na changamoto zinazoathiri mustakabali wa mtandao wa Intaneti. Pamoja na mambo mengine, walizungumzia umuhimu wa upatikanaji wa mtandao wa intateti...